Dereva wa basi la Mtei Express auawa na madereva wa malori kutoka Rwanda

Dereva wa basi la Mtei Express auawa na madereva wa malori kutoka Rwanda

Hapa ni kuwa makini na kujifanya mjinga kuepusha shari ....binadamu tunatofautiana sana,kabla ya kumface mtu msome kwanza, kuta watu ni wamevurugwa Ile mbaya asee ,Sasa mtu humjui unaenda kuanzisha conflict nae ...Epuka conflict zisizo na maana kabisa
Ukiangalia hapo dereva ye angeendelea na safari yake au angereport kwa usalama wa barabarani kwa sababu Kuna vitu huezi solve mwenyewe pasipo kuleta madhara kama haya.
RIP
 
Hoja hapa si waliopigana, ni unyumbu wa wanaotazama wakirikodi. Unadhani hiyo tabia ya kutazama na kurikodi inaishia kwa wapiganaji tu, hata ukavamiwa na fisi akaanza kukurarua nyumbu watarekodi utafunwe kila kitu huku wakiambatanisha na emoji za masikitiko.
😁na emoji za masikitiko

Yaani fisi atarekodiwa mpaka anapoburuta na kutoweka.

Watanzania ni mazezeta kweli.
 
Ntakupa scenario moja:

Kuna Jamaa walikua wanapita sehemu wakasikia Mwizi Mwizi Jamaa wakaliunga mpaka pale kwenye wakamshushia vipigo heavy mpaka akakata roho baada ya kukata roho Jamaa wakaongeza kitu kingine wakamburuta yule Mwizi mpaka kituo cha Polisi kuwakabidhi Polisi kwamba huyu ni Mwizi tumemkuta sehemu anashambuliwa na Sisi tukamuongezea kipigo, Polisi wanawaambia sawa mwekeni pale baada ya hapo anzeni kufungua mikanda suruali na Mashati yenu mna kesi ya kujibu

Hivi mpaka hapo umenielewa namaanisha nini?
Ntakujibu kwa scenario moja.

Kuna jamaa walisikia mwizi mwizii wakaliunga mpaka eneo la tukio, walipofika wakachukua simu zao na kurikodi tukio zima la mwizi kuchomwa moto mpaka mwizi anakata roho, baadae wakarusha kwenye mitandao ikajulikana ni kijana mwanafunzi aliyeitiwa mwizi na mpenzi wake waliyegombana, mbaya zaidi ni ndugu wa karibu wa mmoja wa aliyekuwa anarekodi.

Hivi mpaka hapa umeelewa namaanisha nini?
 
Siku hizi ishi kama uko peke yako, jiepushe na sintofahamu yoyote ili roho yako iwe salama, Kuna watu wana stress sana kukuua ni mara moja halafu Kuna zile chuki za makundi Fulani, dereva wa Lori vs dereva basi au utakuta dereva gari binafsi vs dereva pikipiki... Maisha yahitaji uangalifu sana kipindi hiki, hivyo lazima uwe makini.
 
Hoja hapa si waliopigana, ni unyumbu wa wanaotazama wakirikodi. Unadhani hiyo tabia ya kutazama na kurikodi inaishia kwa wapiganaji tu, hata ukavamiwa na fisi akaanza kukurarua nyumbu watarekodi utafunwe kila kitu huku wakiambatanisha na emoji za masikitiko.
Obvious jamaa alipewa pigo moja tu, kitendo cha haraka. Basi limesimama dereva kashuka hamjui anaenda kufanya nini. Somo kuu hapa watu watumie busara kuhimili hasira zao, ukishindwa kuji control matokeo yake ndio haya.
 
Ntakujibu kwa scenario moja.

Kuna jamaa walisikia mwizi mwizii wakaliunga mpaka eneo la tukio, walipofika wakachukua simu zao na kurikodi tukio zima la mwizi kuchomwa moto mpaka mwizi anakata roho, baadae wakarusha kwenye mitandao ikajulikana ni kijana mwanafunzi aliyeitiwa mwizi na mpenzi wake waliyegombana, mbaya zaidi ni ndugu wa karibu wa mmoja wa aliyekuwa anarekodi.

Hivi mpaka hapa umeelewa namaanisha nini?
Wewe umeendeleza scenario kwa mtazamo wako
 
Wewe umewahi hata kuendesha Gari ukayaona madudu ya madereva barabarani au unaropoka ropoka tu, yeye kaenda kuzungumza nae km dereva mwenzie sio ugomvi na ubabe nyinyi ndio mnakuza mambo na kumfanya marehemu km ana makosa wakati alichokifanya kwa Usalama wa abiria ni sahihi au ulitaka wafe abiria zaidi ya 30 ndio ufurahi hivi kumbe kuna watu ni Mazuzu humu Jukwaani halafu wanajiona ni GT?
Sijawahi kuendesha gari wala kupanda. Unapaniki nini? Wewe ndio unajionesha ulivyo zuzu hata civilized conversation inakushinda.
 
Wewe umeendeleza scenario kwa mtazamo wako
Hata wewe Scenario yako imetokana na mtazamo wako.

Mitazamo ndo hudefine mtu ni wa aina gani. Mwoga, jasiri, hodari, dhaifu, anayejali, asiyejali n.k

Mfano, tukiwa jamii yenye mtazamo wa kuogopa kusaidia watu ili tusiingie kwenye matatizo tunakuwa jamii yenye watu aina ya .............. malizia mwenyewe boss.
 
Wewe ni bwege sana Mimi ningekua pale kwanza yule Jamaa alieua angekua marehemu Muda huu na lile Lori lingekua mkaa screpa Muda huu na wakati huo nyinyi makameraman wa kujitegemea mmesharusha Video zangu Dunia nzima
 
Obvious jamaa alipewa pigo moja tu, kitendo cha haraka. Basi limesimama dereva kashuka hamjui anaenda kufanya nini. Somo kuu hapa watu watumie busara kuhimili hasira zao, ukishindwa kuji control matokeo yake ndio haya.
Yote mawili yalishindikana, kuzuia mauaji na kuzuia wauaji kuondoka?
 
Wewe ni bwege sana Mimi ningekua pale kwanza yule Jamaa alieua angekua marehemu Muda huu na lile Lori lingekua mkaa screpa Muda huu na wakati huo nyinyi makameraman wa kujitegemea mmesharusha Video zangu Dunia nzima
OK boss. Una nguvu mno, ila binafsi hata kutafuta camera tu kwenye smart phone yangu wakati mwingine napata tabu.
 
Yote mawili yalishindikana, kuzuia mauaji na kuzuia wauaji kuondoka?
Babu Sisi ndio wale Gari ukifanya fyoko dereva akishuka na Sisi tunashuka kwenye Bus na Wewe kuangalia lolote likitokea kikinuka tunapambana pamoja maana barabarani mambo ni mengi hio ilikua Bahati mbaya tu kwake marehemu labda dereva alibeba Wanawake tupu kwenye Bus huwezi jua
 
Inawezekana.
 
Wakati mwingine,kuna mambo ya kufikilia kabla ya kuweka taarifa hadharani.
1. Hivi,ni kweli wauwaji ni madereva wa Rwanda?

2. Je,basi zima,makonda na abilia wote,mtu anashushwa,wa kumshusha anaonekana ana hasira,na chuma mkononi,watu wakakaa tu kumuangalia,mpaka anapigwa na kukata moto! Basi alibeba mazombi tuuu.

3. Kuna haja ya watu wengine kuchunguzwa afya ya akili. Dereva huwezi kusimama kwenda kumpiga mtu,huku tena yeye alikuwa nyuma yako. Ni wazi pengine uliendesha vibaya.

4. Video siku hizi,ni kweli zina umhimu na kusaidia kuujua ukweli. Lakini,ebu fikilia kama ni mwanaume karekodi,mwenzie anauliwa,yeye anachukua picha tu!!! Naona na MV Bukoba ingezama leo,wengi wangeanza na hilo.
Hakuna aliyekuwa anajua dereva anaenda kufanya nini, pili hakuna aliyejua derevawingine atafanya nini. Tatizo utakuta aliye chukua video alikuwa mbali na mlango na alikuwa upande wa dirishani. Mpaka aombe kutoka Kwa abiria mwenzie, apite kwenye uwanda WA wazi, stoke nje , tukio lingekuwa lina msubiria kama vile yeye ni mwamuzi wa Hilo pambano
 
OK boss. Una nguvu mno, ila binafsi hata kutafuta camera tu kwenye smart phone yangu wakati mwingine napata tabu.
Sio nguvu sipendi kuona mtu anaonewa kibwege na wakati Mimi nipo hapo hapo alieonea lazima nimwadabishe km hajaja kubebwa akiwa kilema basi na yeye amfuate alipoenda marehemu na ule mlori ungekua ushawaka moto zamani sana shenzi na hivi natembeaga na Bunda la kiberiti tukichimba Dawa nishtue kimoja halafu Safari iendelee wala nisingehangaika kutafuta duka ninunue kiberiti
 
Hakuna aliyekuwa anajua dereva anaenda kufanya nini, pili hakuna aliyejua derevawingine atafanya nini. Tatizo utakuta aliye chukua video alikuwa mbali na mlango na alikuwa upande wa dirishani. Mpaka aombe kutoka Kwa abiria mwenzie, apite kwenye uwanda WA wazi, stoke nje , tukio lingekuwa lina msubiria kama vile yeye ni mwamuzi wa Hilo pambano
Aliechukua Video ni dereva mwingine wa Lori au Bus aliekua anapita pembeni na yeye tukio kalikutia katikati au hujaona hio clip?
 
Back
Top Bottom