Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
20210311_132713.jpg


Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linamchunguza dereva wa basi la wanafunzi, Yohana Mwambene, kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka mitano.

Dereva huyo anatuhumiwa kufanya kitendo hicho kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya St. Anne Marie Academy iliyopo Mbezi kwa Msuguri

Dereva huyo amekuwa akiwabeba wanafunzi wanaosoma shule hiyo.


Chanzo: Mwananchi
 
Hizi shule zetu za school basi walivyo na njaa, wanashindwa kumpa overtime mwalimu kwa ajili ya kuwasindikiza watoto wote hadi wamalizike?

Halafu madereva wengi ni 20's wana mihemko na nyege MSHINDO(Hawajaoa) kwahiyo ni rahisi sana kuwabaka watoto..

Serikali inabidi iweke msisitizo na traffic wakamate gari la shule lisilokuwa na matron ndani.
 
Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana. Ni nyakati ambazo wanadamu wameshaachana na matumizi ya fahamu badala yake waanaenenda kama wanyama.

Ni nyakati ambazo zimejaa mashaka, hofu ,wasi wasi na majuto kuliko furaha. Ni nyakati ambazo uaminifu na utu vimekuwa vitu adimu sana kiasi kwamba watu wema wanaonekana wajinga na jamii inawashangaa.

Kuishi nyakati hizi na kubaki salama kunahitaji bahati pamoja na kudra za muumba pekee maana mioyo ya watu imejaa chuki na visasi ili hali nyuso zao zinatabasamu na kucheka.
 
Nadhani hii Ni fursa mwa mabinti kusomea udereva wa hizi school bus.

Bora kumpa Binti aendeshe school bus kuliko mwanaume. Na ninaiona ni fursa ya wazi sidhani Kama Kuna mdada akiomba kazi atakosa.
Kwan mdada hawazi kumnajisi mtoto wa kiume??

Hujawah sikia mdada anamchukua mtoto wa kiume na kufanya nae yjinga?

Dunia imeharibika, suluhisho ni kuwa wahudumu ndan ya hilo bus
 
Huu mchezo wa kingese wa madereva kukaa peke yao na watoto kwenye gari bila kua na mdada (awe kama matron) kwenye gari sio wa kuvumilika. Kila bus liwe na dereva Ila na mdada wa kuwaongoza watoto.
The easiest na kupunguza gharama za uendeshaji madereva wa school buses wawe wanawake.
 
Wale watoto wa mwanzo (alfajiri) wanaopitiwa na gari mapema kigiza kikiwepo huwa ni victim wa madereva na wale wadogo wanateswa na wale wakubwa. Wazazi waangalie hilo.

Kuna member humu alisema aliwaona wanafunzi kwenye school bus wakinyonyana ndimi siti ya nyuma kabisa. Kaa chini na mwanao atakueleza mengi kama sio yake basi ya wanafunzi wenzake.
 
Back
Top Bottom