Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

View attachment 1722734

Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linamchunguza dereva wa basi la wanafunzi, Yohana Mwambene, kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka mitano.

Dereva huyo anatuhumiwa kufanya kitendo hicho kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya St. Anne Marie Academy iliyopo Mbezi kwa Msuguri

Dereva huyo amekuwa akiwabeba wanafunzi wanaosoma shule hiyo.


Chanzo: Mwananchi
Hii shule tatizo ni mmiliki tu unampa mtu aliyefeli shule kusimamia taasisi kubwa kama hii
 
Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana. Ni nyakati ambazo wanadamu wameshaachana na matumizi ya fahamu badala yake waanaenenda kama wanyama.

Ni nyakati ambazo zimejaa mashaka, hofu ,wasi wasi na majuto kuliko furaha. Ni nyakati ambazo uaminifu na utu vimekuwa vitu adimu sana kiasi kwamba watu wema wanaonekana wajinga na jamii inawashangaa.

Kuishi nyakati hizi na kubaki salama kunahitaji bahati pamoja na kudra za muumba pekee maana mioyo ya watu imejaa chuki na visasi ili hali nyuso zao zinatabasamu na kucheka.
Umeandika kwa hisia na logic sana mkuu
 
Back
Top Bottom