Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana. Ni nyakati ambazo wanadamu wameshaachana na matumizi ya fahamu badala yake waanaenenda kama wanyama.
Ni nyakati ambazo zimejaa mashaka, hofu ,wasi wasi na majuto kuliko furaha. Ni nyakati ambazo uaminifu na utu vimekuwa vitu adimu sana kiasi kwamba watu wema wanaonekana wajinga na jamii inawashangaa.
Kuishi nyakati hizi na kubaki salama kunahitaji bahati pamoja na kudra za muumba pekee maana mioyo ya watu imejaa chuki na visasi ili hali nyuso zao zinatabasamu na kucheka.