Dereva wa STL 9898 Landcruiser Uwe Muungwana

Dereva wa STL 9898 Landcruiser Uwe Muungwana

Ujumbe ukufikie popote ulipo, waliolala makaburini hawakujitakia, ni mapenzi ya Mungu, kitendo ulichofanya Kola makaburini leo tarehe 19.4.2022 saa 12:26 jioni siyo cha uungwana.

Umesimamisha gari lenye namba tajwa na kuchepuka kukojoa kwenye eneo la makaburi bila hata haya, tumekupiga picha kwa kila ulilofanya pale, wengi tumeshindwa kukuelewa kama una akili timamu au ulikwenda kufanya ushirikina.

Mtu mwenye akili timamu hawezi kuthubutu hata kutema mate katika eneo kama lile, lakini huenda kwasababu ya kibri, dharau, majivuno ya uhai ulio nao ukaona waliolala makaburini ni wa kuwakojolea, mbaya sana, mbaya sana, mbaya saaaana!!!
Bila Shaka wewe ulikuwa hayo maeneo ya hiyo Dispensary au hapo night club barabara ya Bigwa. Mungu anamuona huyo dereva.
 
Makaburini hakuna chochote kilichomo zaidi ya mifupa ya wafu. Mtu hawezi kujikojolea kisa kuogopa kukojoa juu ya ardhi,. Unashauri angekojoa wapi????

JESUS IS LORD
Miji yetu, hata hapo alipotaja mleta mada pamejaa mabaa kila hatua 50, si angeenda huko?
 
Inawezekana unachuki binafsi na hiyo dereva,kuna je mwiliwako ni automatic kwamba unaweza ku u tune unavyotaka?hujaona watu wakidondoka,kujisaidia bila kupenda?je amebanwa eneo hisika angefanyaje?
Binafsi huwa nakojoa kwenye tairi, nafungua mlango wa gari nakojolea tairi. Hii kukojolea kaburi sio poa.
 
Kama kweli alikojoa kwenye Kaburi Aisee Alichofanya Ni kitu Cha ovyo Binafsi Naheshimu Sana Makaburi ya Wafu Nashangaaga Sana Watu Huwa Wanayakalia na Kukanyaga Wakienda Kuzika
 
Kama kweli alikojoa kwenye Kaburi Aisee Alichofanya Ni kitu Cha ovyo Binafsi Naheshimu Sana Makaburi ya Wafu Nashangaaga Sana Watu Huwa Wanayakalia na Kukanyaga Wakienda Kuzika
Yeye ndiyo aliyezikwa Apo naskia
 
Mods napendekeza kuwe na uzi sticky kwa ajili ya watu kama hawa na uitwe "tuwaumbue" au "aibu yako" maana huko mitaani tunakuta na watu waio na ustaarabu kabisa.
Mimi viusafiri vyangu viwili vina camera mbele na nyuma,zinarekodi muda wote gari ikiwa imewashwa,hivyo matukio yote yanayotukia barabarani huwa yanarekodiwa,na ni mengi ya hovyo sana nakutana nayo na naamini ni wengi pia wanakutana nayo,hivyo tukiwa na uzi unaozungumzia hilo naamini utasaidia kuwawajibisha watu na kubadili tabia za hovyo.
 
Ujumbe ukufikie popote ulipo, waliolala makaburini hawakujitakia, ni mapenzi ya Mungu, kitendo ulichofanya Kola makaburini leo tarehe 19.4.2022 saa 12:26 jioni siyo cha uungwana.

Umesimamisha gari lenye namba tajwa na kuchepuka kukojoa kwenye eneo la makaburi bila hata haya, tumekupiga picha kwa kila ulilofanya pale, wengi tumeshindwa kukuelewa kama una akili timamu au ulikwenda kufanya ushirikina.

Mtu mwenye akili timamu hawezi kuthubutu hata kutema mate katika eneo kama lile, lakini huenda kwasababu ya kibri, dharau, majivuno ya uhai ulio nao ukaona waliolala makaburini ni wa kuwakojolea, mbaya sana, mbaya sana, mbaya saaaana!!!
picha
 
Sioni ajabu na hio huwa ni unconscious, labda useme kilichofanyika ni ushirikina ila kama kukojoa tu, ni mistakes za unconsciousness among us.
 
Back
Top Bottom