Dereva wa UDOM akamatwa kwa madai ya kummwagia Kemikali Afisa Mtendaji

Dereva wa UDOM akamatwa kwa madai ya kummwagia Kemikali Afisa Mtendaji

Umeachana na mumeo Tena inawezekana chanzo ni wewe.

Umepata bwana na umezaa nae. Maana mtoto ana miezi sita na ndoa ilivunjika mwaka juzi.

Bado unataka kumfilisi mtalaka wako eti mgawane mali.
Kuna matatizo yakujitakia.
Kweli Kabisa huu ni wizi, mtendaji Huku unafanya dhuluma ya Mali ili kumnyoosha huyo mwana Mume, Hana Hata Soni Wakati ana mwanamume mwingine, huyo mwanamume mpya awe makini
 
1688123483320.png

Dereva wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Lusajo Makiwelu anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwamwagia kemikali watu wawili akiwemo mtalaka wake, Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita (jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alipozungumza na Mwananchi jana Juni 29, akisema lilitokea juzi wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani jijini hapa.

Amesema wamemshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kummwagia mtalaka wake tindikali.

"Ni kweli taarifa hizo zipo tulipata taarifa hizo na tulifanya ufuatiliaji hiyo jana( juzi) majira ya usiku na huyo mtuhumiwa tayari ametiwa mbaroni, kwa sasa tunaendelea na mahojiano" ameeleza Kamanda Martin Otieno

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Witness ambaye ni ofisa Mtendaji wa kijiji cha Idedelomkazi Wilayani Mufindi mkoani Iringa, amesema mkasa huo ulimkuta aliposhuka kituo cha Maghorofani akitokea Mafinga Mkoani Iringa alipokuwa akisubiri usafiri wa kumpeleka atakofikia.

Amesema alikuja mkoani Dodoma kuleta wito wa Mahakama ya Mwanzo ya Mafinga kwa aliyekuwa mumewe ambaye walitenganishwa na mahakama hiyo.

"Safari yangu ilianza saa 3:00 asubuhi na gari ya Shabiby nikitokea Mafinga lengo likiwa ni kuleta wito Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma.

"Safari ilienda vizuri hadi nilipofika kituo cha mabasi Maghorofani niliposhuka kusubiri daladala au bajaji ili niende kukabidhi wito huo,” amesema.

Amesema akiwa katika kituo hicho, alipita mwanaume mmoja ambaye hakumfahamu akiwa ameshika kichupa mkononi kilichokuwa na kimiminika na mara baada ya kumsalimia alimwagia usoni.

“Alichofanya ni kunisalimia tu dada habari na kabla sijamjibu akanimwagia tindikali. Kwa muda nilipanwa na pumzi lakini nikajitahidi nikaomba msaada kwa watu waliokuwa pembeni na kituo hicho,” amesema.

Amesema madereva bajaji na bodaboda walimsaidia na kumfikisha kituo cha polisi, ambapo alipewa PF3 na kisha walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako amelazwa.

Witness amesema alikuwa akimpelekea Makiwelu wito wa mahakama uliolenga kugawana mali walizochuma pamoja baada ya ndoa yao kuvunjwa na Mahakakama ya Mwanzo ya Mafinga mwaka juzi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Baraka Mponda amesemaa walimpokea mama huyo na mtoto wake wa miezi 6 juzi jioni waiwa wamejeruhiwa usoni kwa kumwagiwa kemikali.

Dk Mponda amesema majeruhi hao walifika wakiwa kwenye maumivu makali, mama akiwa ameathirika maeneo ya usoni, shingoni na begani na usoni kwa upande wa mtoto.

Amesema majeruhi hao wameendelea kupatiwa matibabu zaidi hospitali hapo.

MWANANCHI
 
hii habari haijitoshelezi imeegemea upande mmoja wa kumtetea mwanamke ila mzembe ni mmwagaji tindikali kukamatwa tena na polisi maana akibanwa p…mbu atamtaja aliyemtuma.

lakini we mama kama mliachana mali unataka upeleke wapi ?
 
Umeachana na mumeo Tena inawezekana chanzo ni wewe.

Umepata bwana na umezaa nae. Maana mtoto ana miezi sita na ndoa ilivunjika mwaka juzi.

Bado unataka kumfilisi mtalaka wako eti mgawane mali.
Kuna matatizo yakujitakia.
Wanawake hawana akili kabisa ..kuachana tu maumivu tosha unataka ukachukue na mali za mtu khaaa.
 
Amesema wamemshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kummwagia mtalaka wake tindikali.
hii habari haijitoshelezi imeegemea upande mmoja wa kumtetea mwanamke ila mzembe ni mmwagaji tindikali kukamatwa tena na polisi maana akibanwa p…mbu atamtaja aliyemtuma.

lakini we mama kama mliachana mali unataka upeleke wapi ?
Aliyekamatwa ni mume..na sio aliyemwaga Tindikali.
 
Ila watu wanapofikia siyo kabisa, kinachonisikitisha ni hadi mtoto kuwa muathirika wa ukatili huo. Huyo mwanaume ni katili wa kupitiliza, yaani huu ni zaidi ya ukatili, imeniuma sanaaaaa.
Punguza kuwaza kwa kutumia hisia kijana, una uhakika huyo jamaa ndo kammwagia tindikali?? Binti anasema hafahamu ni nani, pamoja na kusalimiwa nae mmwagiaji bado hakumtambua.

Apo kampa mzigo tu jamaa na huku hatujui historia yake huko atokako ikoje, mahusiano na huyo mzazi mwenzie yakoje.
Kwenye hiyo habari hamna mahali kaongea ndgu, baba wa mtoto n.k

Na hapo dkt kasema alipelekwa hospitali juzi....
 
Tatizo la siku hizi watu wengi tuko closed minded sana mtu unaamini kitu fulani kikishindikana unasema haiwezekani. Usiogope changamoto usiogope kuanza upya. Unaanza upya lakini una Faida ya kuwa na uzoefu. Hii ni changamoto kubwa kwa sababu Vijana wengi hawajapitia Jando. Kuna mstari wa biblia unasema usitumie uwezo wako wa kufikiri pekee bali mshirikishe Mungu. Ukitumia uchambuzi wa kiphilosophia wa huu mstari wa biblia,utagundua kwamba tumeambiwa tuwe wajinga katika maisha tupokeee kila kitu kama tulivyo.Usijiwekee kwamba kitu fulani hakiwezi kunitokea au sitakubali. Ukifanya hivyo utaingia kwenye Majaribu ambayo itabidi uuwe au hata ufanye mambo ya kutisha. Ni muhimu sana kupokea changamoto na kuzitafutia uchambuzi. Kwa kukaa chini na kufikiri. Yaani kuna watu walivurugwa na wake zao, ndugu zao na watoto wao na bado wakasimama. Just imagine mwanaume unapambana na Maisha ndugu wanakuombea mabaya Wazazi wameshafariki, Mke naye hayuko upande wako watoto ndo kabisa wanajiharibia maisha ili wakukomoe ila bado upo strong. Kuna Fogo mmoja ni rafiki anaishi maisha haya na mambo yanaendelea. Anapambana na Kazi na biashara zinasimama na zinazidi kukua. Ukitumia uwezo wako wa kufikiri katika maisha utafocus kwenye mambo yasiyo na msingi.
Hii ni mbinu ya ku-ignore tatizo la msingi, na kufanya ionekane tatizo ni wanaume tu, kama vile wanaume ni watu ambao hawapaswi kuvurugwa, bila kuzingatia matendo ya mwanamke.

Mwanamke anazalishwa na mwanaume mwingine, kisha anakuja kudai mali za mwanaume wake wa zamani, mnaona ni sawa tu, as long as sio wewe
 
Mtoto ana miezi 6 na ndoa yao ilivunjika tangu mwaka juzi hii inamaanisha kuwa mtoto si wake kazalishwa na mwanaume mwingine huko na kama haitoshi bado anamganda X wake ili wagawane Mali qmmke
Huyo kazalishwa na kaachwa, maana mwanaume mwenye akili timamu unaruhusuje mkeo aende huko kwa ex wake na mwanao mdogo wa miezi 6.
 
Back
Top Bottom