Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Yesu ajazaliwa Christmas ilo linajulikana sema dini yetu hii ni ya kipagani inaendana na mafundisho ya ki binaadamu ndio maana huwezi tofautisha na ushoga. Hakuna Mungu huku alikozaliwa yesu kwenyewe hakuna Ukristo iweje uwepo Roma ambapo hajawahi hata kufika?
 
Humu ndani mada kama hii huwa haipendwi kwa hiyo usishangae ikifungwa soon. Niliwahi kuleta mada kama hii kutoa elimu kwa upotoshaji mwingi unaofanywa kuhusu Christmass lakini topic ikaishia kufungwa. Lakini sio mbaya ujumbe ulifika na wengi wamepata elimu hii. Kiukweli hakuna ushahidi wowote wa maadiko kuhusu tar.25 dec kama ndiyo tarehe aliyozaliwa Yesu Kristo. Isipokuwa tarehe hiyohiyo 25 dec. ilikuwa ni sikukuu ya kipagani ya wababeli wakisherehekea kuzaliwa kwa mwana wa mungu wao Tamuz aliyeaminika kuwa mwana wa Nimrod ambaye alipokufa aliaminiwa kuwa alienda kwenye jua na mionzi ya jua ikamtia mimba malkia wa babeli aliyeitwa semiramis ndipo akamzaa tamuz( mungu mwana wa jua). Hii habari ya Nimrod kuishi kwenye jua ilienezwa na malkia baada ya mumewe kufa na baadae malikia akawa mjamzito. ili kuepuka hatia na aibu ya kuzaa nje ya ndoa ilibidi uongo utungwe kwa ustadi mkubwa kuwa Nimrod hakufa bali alienda kuishi kwenye jua na mionzi yake ndio iliyomtia mimba malkia semaramis na kumzaa mwana aliyepewa jina la tamuz. Hivyo wababeli na baadae rumi ya kipagani waliendelea kusherehekea siku ya kuzaliwa mungu mwana jua aliyeitwa tamuz katika tarehe 25.Dec. Hiyo ilikuwa sikukuu kubwa enzi hizo na katika siku hiyo wafalme walipewa mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa. rejea Yeremia 52:31-34.

Jambo la kusikitisha ni kuifanya sikukuu ya kipagani kuwa ni sikukuu ya kuzaliwa Mwana wa Mungu Mkuu Yesu Kristo. Kama ni kufuru, kizazi hiki kimepitiliza.
 

Tuanza kujibu swali moja moja..
Kuhusu mwezi wa sita (kwenye red hapo) unachojaribu kusema ni kuwa malaika alimtokea mwezi wa sita (kwa siku za leo tungesema june) so unadhani mpaka mwezi wa 12 mtoto atakua na miezi 6.. nimeona pia cc: LITONO nae amenguka kwenye huo mtego..

Miezi sita hapo siyo mwezi wa sita (june) au mwezi wa sita wa mwaka. ukitaka kueleweza anzia mlango wa 24 (luka 1:24) "Hata baada ya siku zile mkewe Elizabeth alichukua mimba akatawa MIEZI MITANO akasema..."

mwandishi anaendelea na tukio hilo la mstari wa 24, (limetenganishwa tu na mstari wa 25), ...baada ya kutawa miezi mitano, mwezi wa sita malaika akamtokea mariam.. kwa maana nyingine baada ya miezi 6 kupita tokea amtokee elizabethi" kwa kiingereza inasema in the sixth month..
kwa hiyo hapo uelewe kuwa siyo mwezi wa sita wa mwaka, ni mwezi wa sita baada ya tukio la eliza.. na ndio maana tunasema Yesu na Yohana mbatizaji wamepishana miezi 6.
 

Hakuna mtu/mkristo yeyote anayesema kuwa 25 ndiyo tarehe aliyozaliwa Yesu, utakua tu hujaelewa kama ambavyo watu wengi hawaelewi... hakuna mtu anayejua tarehe aliyozaliwa Yesu, hilo tunalifahamu.

kuhusu tahere 25. Ni kukumbuka siku ya kuzaliwa Yesu AU siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU.
to make it simple.... Wote tuna uhakika kuwa alizaliwa (nadhani hata ww unakubali) siku ndio hatujui, kwa hiyo tumeamua kutafuta siku moja ya Kuadhimisha au kukumbuka kuwa alizaliwa MASIHI (Mkombozi wetu) kwa sababu tuna uhakika kuwa kuna siku alizaliwa...

kwa mfano kama ingekua ni tarehe labda 10 october.. Je ungejali?? au pia ungekuja na theory nyingine

Labda kwa kukusaidia kama ww huamini katika kusherekea Christmas sio tatizo, wala sio amri wala sio shida, endelea tu na maisha,
Lakini pia hakuna sehemu yeyote inasema kuwa ni dhambi, sasa kwa nini wewe unakasirika na watu ambao wao wanasherekea
 



Mkuu hapo nimekuelewa, labda tatizo lipo kwa waandishi wa biblia ya kiswahili, ukisoma hapo vizuri unaweza kuchukua ni mwezi wa sita wa kalenda.

Mkuu nina swali kwako, Je kuna tofauti gani kati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa na kukumbuka siku ya kuzaliwa?

Nimeuliza hivyo kwa sababu as per our life ni kwamba huwa tunasheherekea siku ya kuzaliwa pamoja na kukumbuka mpaka pale inapofika tarehe husika na siku husika.
 


Mkuu, tunaadhimisha kwahiyo unataka kusema kuwa tunaadhimisha siku ya kuzaliwa Kristo ambayo sio siku halisi ya yeye kuzaliwa?

Yaani kwa ufupi unajaribu kusema tinasherekea siku ya Uhuru ambayo sio siku halisi ambayo tulipata uhuru.

Je wewe wadhani kwanini waliamua tarehe 25 december na sio tarehe nyingine?

Kuna mchangiaji hapo juu kasema kuwa hiyo tarehe ilikua ni sikukuu ya kipagani ya warumi/wababeli, Je wewe unakubaliana nae?
 


Mkuu napingana na wewe kwa hilo, Ushoga ni tabia ya mtu kwahiyo kuihukumu jamii mzima hapo unakua hujaitendea hali jamii husika.

Ushoga kila sehemu upo, ukienda kwa wakristo upo, waislamu upo, wabudha upo na dini nyinginezo pia upo.

Kitu cha muhimu ni kuwaheshimu tu na kuwaacha waishi kwa amani huku wakipata haki zao za msingi bila kuwabagua.

Biblia inahubiri upendo hata kwa adui zako. Nawe naomba hata kama unachukia mashoga na wasagaji ila endelea kuwaombea kwa mungu huenda ipo siku wataacha.
 
Unaumwa.
 

Mkuu kama unaamini kwamba Bikra Mariam alibeba mimba bila kujamiana na mmewe kwa hiyo hakuna ajabu kuzaliwa kabla ujauzito haujafika miezi Tisa.
 
Mkuu kama unaamini kwamba Bikra Mariam alibeba mimba bila kujamiana na mmewe kwa hiyo hakuna ajabu kuzaliwa kabla ujauzito haujafika miezi Tisa.

tatizo kubwa ni KWANINI YESU AZALIWE TAREHE 25 DECEMBER(na tusheherekee) WAKATI HAKUNA UTHIBITISHO WA AINA YEYOTE KUTOKA KWENYE BIBLIA?
na kinachofanya watu wahoji juu ya kuzaliwa kwake hiyo tarehe 25 december ni kwasababu hiyo tarehe kwa hapo zamani wababeli walikuwa wanasheherekea juu ya kuzaliwa kwa mungu JUA/sun god...
katika siku ya JUMAPILI/sundey﹉
 

Soma 1 Wakorintho 11:23-26: maagizo pekee aliyotuachia Bwana Yesu ni kula mkate na divai kama kumbukumbu ya mwili wake na damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Verse 26 inasema " kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hadi ajapo."

Acheni kujifariji kwa mafundisho ya uongo yasiyotokana na Biblia Takatifu. Bwana Yesu hakuona umuhimu wowote wa kusherehekea kuzaliwa kwake kwani alikuwepo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Hata yeye wala mitume wake hakuna aliyesherehekea birthday ya Yesu, ninyi mwaitoa wapi?

Jambo la msingi ni kumbukumbu ya mauti yake kwani hilo ndilo kusudi lake kuu lililometa hapa duniani na kuutwaa mwili huu wa dhambi ili afe kwa ajili yetu wadhambi.

Someni maadiko yawaweke huru acheni kusikiliza hadithi za uongo zitawapoteza.
 

Soma 1 Wakorintho 11:23-26: maagizo pekee aliyotuachia Bwana Yesu ni kula mkate na divai kama kumbukumbu ya mwili wake na damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Verse 26 inasema " kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hadi ajapo."

Acheni kujifariji kwa mafundisho ya uongo yasiyotokana na Biblia Takatifu. Bwana Yesu hakuona umuhimu wowote wa kusherehekea kuzaliwa kwake kwani alikuwepo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Hata yeye wala mitume wake hakuna aliyesherehekea birthday ya Yesu, ninyi mwaitoa wapi?

Jambo la msingi ni kumbukumbu ya mauti yake kwani hilo ndilo kusudi lake kuu lililometa hapa duniani na kuutwaa mwili huu wa dhambi ili afe kwa ajili yetu wadhambi.

Someni maandiko yawaweke huru acheni kusikiliza hadithi za uongo zitawapoteza.
 
teh teeh teeeh eeeerh... .. .biblia ni moja na quran ni moja... .. . lakini kundi/dhehebu moja huona mafundisho yao ni bora kuliko ya wengine,
 
teh teeh teeeh eeeerh... .. .biblia ni moja na quran ni moja... .. . lakini kundi/dhehebu moja huona mafundisho yao ni bora kuliko ya wengine,

Hayo yote yalijulikana tangu awali ndio maana Bwana Yesu alitusihi tujiepushe na manabii wa uongo...kwa kuwa nao hutumia Biblia ila kwa kupotosha.
 
Hayo yote yalijulikana tangu awali ndio maana Bwana Yesu alitusihi tujiepushe na manabii wa uongo...kwa kuwa nao hutumia Biblia ila kwa kupotosha.

kwani manabii wa uongo wapoje?
na wewe unaamini vipi hapo ulipo manabii wake ni wa kweli?
 

Huna haja ya kuuliza watu, wewe sheherekea X-mass mwezi wa pili au wa tatu kama unavyoamini
 
Huna haja ya kuuliza watu, wewe sheherekea X-mass mwezi wa pili au wa tatu kama unavyoamini


Mkuu, Heshima kwako,

Kama tukiwa sote na tabia ya kula kitu bila kujua kimetokana na nini basi hii Dunia isingefika hapa tulipo, Dunia inahitaji watu wanaojua kuhoji na kudadisi mambo mbalimbali yaliyotokea, yatakayotokea na yanayotokea.

Si kwakua kitu hatukijui basi tukae kimya, Japo dini huwa zinazuia kuhoji kitu ambacho kina sintofahamu ila ni vyema kutatua tatizo mapema kabla halijawa kubwa. Hizi contradictions ndizo ambazo zinafanya waumini wa hizi dini kupungua kadri siku sinavyoenda.
 
Kwani yesu alipozaliwa alizaliwa km Mungu au alizaliwa km Mwanadamu kama sisi? naomba nijibiwe hapo kwanza plz
 
Ni kumbukumbu. Yesu hakuzaliwa Desemba 25. Ilikuwepo Rome dini pinzani ya Mithra ambao mtume wake,Mithra alizaliwa Desemba 25.Wakristu wakasema Yesu kazaliwa Desemba 25 ili kuwavuta waumini wa dini ile. Baadaye ile dini ikafa na Wakristu wakavunja hekalu lao na kujenga St.Peter's Basilica. Kwa sababu ile dini ya Mighra,hekalu lake lilikuwa limejengwa pale pale ambapo sasa bivi ipo St Peter' Basilica.. Yesu kazaliwa 888. Tarehe 8,mwezi wa nane,August,mwaka wa nane AD8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…