Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Yesu kristo hakuzaliwa Tarehe 25 December. Hili ni moja kati ya mapokeo ya kitamaduni za kipagani zilizofanikiwa kuingia ndani ya kanisa la kikristo kwa kubebwa na Kanisa Katoliki.
 
Sikukuu ya Christmas ilichaguliwa kwa misingi ya kuendelea kuadhimisha sikukuu ya wapagani waliokuwa wakibadili dini
 
teh teeh teeeh eeeerh... .. .biblia ni moja na quran ni moja... .. . lakini kundi/dhehebu moja huona mafundisho yao ni bora kuliko ya wengine,

teh teh teh

torn between two equally-powerfull Gods,...is it possible?

wakristo na muslims wangekaa pamoja na kuunda dini moja,kidogo atheists wangelegeza msimamo

hatuwezi kuwa na Allah mwenye nguvu zote,pia tukawa na Jehovah mwenye nguvu zote pia.hiki ni kituko

teh teh teh
 

Hakuna mkanganyiko wowote katika hili, wala hakuna wauumini wa dini wanauulizia suala za kuzaliwa Yesu.Nyie ambao hii dini haiwahusu ndio mna viherere vya kuuliza maswali kama hayo.

Kuna mdau mmoja amekujibu vizuri sana, kuwa kinachosheherekewa ni KUZALIWA YESU, sio SIKU YA KUZALIWA YESU!

Nadhani huna takwimu za kutosha juu ya Ukristo duniani. Ndio dini inayoongezeka kwa kasi duniani kuliko dini ingine, na dhehebu la Catholic ndio linaloongoza. Kwa taarifa yako Idadi ya Wakatoliki tu duniani (achana na madhehebu mengine ya kikristo kama Lutheran, SDA, Angalican n.k) ni sawa na Waislamu (watoto wa mama mdogo) wote Ulimwenguni kot e(Shia na Sunni).

Ubarikiwe katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

..................................
 

mkuu labda hujaelewa lengo kuu la mleta mada.

tatizo siyo kusherekea christmas,tatizo ni kwanini iwe december 25.na siyo siku nyingine

halafu ile njia ni nyembamba kaka,ndiyo maana wacatholic wapo wengi njia Nene.
 
Kwani yesu alipozaliwa alizaliwa km Mungu au alizaliwa km Mwanadamu kama sisi? naomba nijibiwe hapo kwanza plz


Yesu alizaliwa kama binadamu wa kawaida na hata kufa kwake pia alikufa kama binadamu wa kawaida.

Kumbuka hili neno wakati wa mateso ya Yesu " Eloi eloi lama thabakithani " ( ruksa kusahihishwa kama nimekosea kuandika)
 


Thanks Mkuu kwa taarifa yako, Nashukuru kidogo umenipa mwanga wa kitu ambacho nilikua nakiuliza hapa.

Ila nina swali moja kwako, as per maelezo yako ni kwamba Yesu kazaliwa august (inavyosadikika) Je biblia inaposema Mariam alitokewa na malaika mwezi wa sita inamaanisha nini?

Manake kama kazaliwa August na mimba alipata mwezi wa sita hii inakuja as mimba alibeba kwa miezi miwili tu.

Once again, Thanks
 



Mkuu,

Sipo hapa kuupinga ukatoliki au uanglikana, Mimi ni mkristo na dhehebu langu ni Anglican,

Nimeuliza hilo swali kutokana na biblia inavyosema, kama kitu hukielewi ni bora kuuliza kuliko kukaa kimya (kuendeleza ujinga)

Ndio, tunasherekea kuzaliwa kwa Yesu na sio siku ya kuzaliwa kwa yesu, Swali langu linaulizwa ni kwanini walipanga tarehe 25 december? Hapo ndipo msingi wa swali langu ulipo.

Na mungu akubaliki sana.
 
mkuu labda hujaelewa lengo kuu la mleta mada.

tatizo siyo kusherekea christmas,tatizo ni kwanini iwe december 25.na siyo siku nyingine

halafu ile njia ni nyembamba kaka,ndiyo maana wacatholic wapo wengi njia Nene.


Thanks mkuu kwa kumrudisha kwenye mada.

Nashauri watengenezaji wa JF app waweke kitufe cha like kwenye hii App ili watu kama wewe mpewe haki yenu.
 

Hapo hamna maagizo au katazo tusifanye KUMBUKUMBU YA kuzaliwa kwake. au naona vibaya.
kwamba ni "maagizo pekee" haimaanishi tusifanya vitu vingine. Nithibitishie kuwa kufanya hivyo ni dhambi
 

Siyo kukumbuka siku ya kuzaliwa... ila tofauti ni hii; tarehe 25 december ni siku ya kukumbuka "KUZALIWA KWA YESU" unaona tofauti inapokuja?

tunasherekea kwamba Yesu "ALIZALIWA", na faida ya KUZALIWA kwake nadhani unaelewa
 
Hapo hamna maagizo au katazo tusifanye KUMBUKUMBU YA kuzaliwa kwake. au naona vibaya.
kwamba ni "maagizo pekee" haimaanishi tusifanya vitu vingine. Nithibitishie kuwa kufanya hivyo ni dhambi

Mfuasi mwaminifu wa Kristo hufanya yale yaliyoagizwa na Bwana wake wala hajitafutii mambo mengine tofauti na yale yaliyoagizwa. Hivyo hayo huitwa mapokeo na kumbuka Bwana Yesu alikemea mapokeo rejea Mathayo 15:8,9
 
Mfuasi mwaminifu wa Kristo hufanya yale yaliyoagizwa na Bwana wake wala hajitafutii mambo mengine tofauti na yale yaliyoagizwa. Hivyo hayo huitwa mapokeo na kumbuka Bwana Yesu alikemea mapokeo rejea Mathayo 15:8,9

Sijui unaongea vitu gani wewe, kuna mahali Yesu ameagiza kwenye Biblia watu waimbe kwaya makanisani?? mbona kuna kwaya.. elewa si kila kitu kinachofanywa kimeagizwa kwenye biblia.. we katika vitu ulivyofanya leo kuanzia asubuhi mpaka sasa kuna mahali Biblia imesema ufanye...

nimekuambia niambie mahali ambapo imekatazwa, unaleta vitu visivyohusiana
 

Ukipiga mahesabu imeonyesha tunaazimisha tusicho kijua maana inasemekana Tammus ndo alizaliwa tarehe iyo mtt wa kambo wa nimrod
 
Siyo kukumbuka siku ya kuzaliwa... ila tofauti ni hii; tarehe 25 december ni siku ya kukumbuka "KUZALIWA KWA YESU" unaona tofauti inapokuja?

tunasherekea kwamba Yesu "ALIZALIWA", na faida ya KUZALIWA kwake nadhani unaelewa

Thanks Mkuu, Je unaweza sema sababu ambazo zilipelekea kuchagua december 25 kuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu?
 
Mfuasi mwaminifu wa Kristo hufanya yale yaliyoagizwa na Bwana wake wala hajitafutii mambo mengine tofauti na yale yaliyoagizwa. Hivyo hayo huitwa mapokeo na kumbuka Bwana Yesu alikemea mapokeo rejea Mathayo 15:8,9


Mkuu nakubaliana na wewe ila kwa machache pia napingana na wewe kwa mengi, Biblia haijasema tupande ndege lakini tunapanda, Biblia haijasema tuoge lakini tunaoga, kuna mambo mengi sana Yesu hajasema lakini tunafanya.

Cha muhimu ni kujua na kuyashika mafundisho yake.

Back to the topic!
 
Ukipiga mahesabu imeonyesha tunaazimisha tusicho kijua maana inasemekana Tammus ndo alizaliwa tarehe iyo mtt wa kambo wa nimrod

Thanks Mkuu,

Je unaweza toa japo kidogo historia ya huyo Tammus mtoto wa nimrod ili watu wajue kipi kilijili mpaka tarehe 25 iwe christmass?
 
mwezi wa sita wa nyakati hizo sio,mwezi wa sita wa wakati huu,enzi hizo hakukuwa na kalenda hii yetu kalenda yao ilikuwa tofauti na hii,na pi tar 25 ni ya kubuni hata mwezi ni wa kubuni,tunasherekea xmass kwa sababu ya kukumbuka ukombozi wa wanadamu kupitia yesu,kwa hiyo hata ingebuniwa siku ya leo ni saw tu sisi tunakumbuka ukombozi wa yesu,kusema kwamba sijui s
ni siku ya mfalme gani alikufa hata kama ni sawa sisi.hatumkumbuki huyo.mfalme tunamkumbuka yesu.kwa hiyo siju sio tija sana ni siku ya kubuni ila kumbukumbu ndio muhimu,kwa kuwa hatujui siku halisi watu wamebuni,so tunamkumbuka yesu sisi katukomboa.
 
Kwani Yesu alisherekea birthday yake tarehe ngapi? mwenye kumbukumbu please
 
Ni kweli kaka, ila kujifunza na kutaka kuelewa kitu kwa undani zaidi sio dhambi.

Kinachonisukuma ni kutaka kujua hasa ni lini kristo alizaliwa ili kujua maana halisi ya hii Christmass ambayo tunasheherekea kila tarehe 25 december kila mwaka.
Kadiri nielewavyo 24-25 desemba kulikuwa na mabadliko ya muda wa mwanga kuongezeka na hivyo kusherehekewa kipagani kama siku ya jua kushinda kiza. Ukristu ili kuondo a imani za kipagani, ikumbukwe ku0ngoka kwa Konstantini mfalme kulikuwa na changamoto zake na faida kwa ukristo wakati huo. Moja ya changamoto ilikuwa tafsiri ya Sabato kutoka kuwa jumamosi na kuwa jumapili, baadhi ya sherehe za kipagani kukristishwa ikiwamo christmas na ufungamanisho wa ukristo na utawala. Faida ahueni ya mateso kwa wakristo.
Kitheologia Kristo ni mwanga wa dunia kuja kwake kunafukuza Giza au shetani na ndo sababu ya Krismas kuwa tarehe ya kuanza kuongezeka kwa muda wa mwanga. Leo hii tunaweza kuona si sawa lakini kalenda ya leo, Augustinian inatofautiana na ya wakati huo Julian. Tukifuata Biblia twaweza kubishana mpaka kesho kuhusu umuhimu wa kuendeleza mabadiliko ya Konstantini. Je wakristo wa leo wanapata mateso sana kiasi cha kutoachana na mabadiliko hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…