Mimi ni mbumbu kabisa kwenye sheria lakini kila nikiaangalia maoni kwenye nyuzi mbali mbali hapa JF nasikitika sana kwa jinsi ambavyo mpaka sasa watu wengi hawajaona nini kinaenda kutokea. Kwa sababu ukifuatilia toka mwanzo kuanzia mtiririko wake toka maamuzi ya pingamiizi la kukosewa mashtaka, trial within trial ya Adamoo na hii ya mwisho juzi ambayo ndio funga kazi ya kutumika sheria ambayo haipo kabisa Tanzania basi wenye maono tunasubiri "formalities" zikamilishwe na si vinginevyo. Ukiona timu mbili zinacheza uwanjani halafu mpira ukifika kwa refa anausogeza kila saa kwa wachezaji wa timu mojawapo badala ya kuukwepa basi tegemea timu inayosogezewa mpira kila saa na refa kushinda hata kama ni dhaifu kiasi gani itashinda tu hata kwa penalti ya mchezaji aliyekwatuliwa katikati ya uwanja refa atasema ni penalti na mpira utawekwa kwenye hatua kumi na mbili.
Kuna ngoma ngumu huwa nazikumbuka sana wakati huo nilikuwa nazisikia nikiwa mdogo na zitaishi muda mrefu sana ujao nitazitaja japo chache najua wahenga wenzangu wataongezea nilizosahau au kurekebisha nilipokosea. Waliotangulia mbele za haki RIP kwao.
Lugakingira, James Mwalusanya, Koroso, Anthony Bahati, Chipeta, Nasoro Mzavas, Nyalali na wengineo.