Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

Mimi ni mbumbu kabisa kwenye sheria lakini kila nikiaangalia maoni kwenye nyuzi mbali mbali hapa JF nasikitika sana kwa jinsi ambavyo mpaka sasa watu wengi hawajaona nini kinaenda kutokea. Kwa sababu ukifuatilia toka mwanzo kuanzia mtiririko wake toka maamuzi ya pingamiizi la kukosewa mashtaka, trial within trial ya Adamoo na hii ya mwisho juzi ambayo ndio funga kazi ya kutumika sheria ambayo haipo kabisa Tanzania basi wenye maono tunasubiri "formalities" zikamilishwe na si vinginevyo. Ukiona timu mbili zinacheza uwanjani halafu mpira ukifika kwa refa anausogeza kila saa kwa wachezaji wa timu mojawapo badala ya kuukwepa basi tegemea timu inayosogezewa mpira kila saa na refa kushinda hata kama ni dhaifu kiasi gani itashinda tu hata kwa penalti ya mchezaji aliyekwatuliwa katikati ya uwanja refa atasema ni penalti na mpira utawekwa kwenye hatua kumi na mbili.

Kuna ngoma ngumu huwa nazikumbuka sana wakati huo nilikuwa nazisikia nikiwa mdogo na zitaishi muda mrefu sana ujao nitazitaja japo chache najua wahenga wenzangu wataongezea nilizosahau au kurekebisha nilipokosea. Waliotangulia mbele za haki RIP kwao.
Lugakingira, James Mwalusanya, Koroso, Anthony Bahati, Chipeta, Nasoro Mzavas, Nyalali na wengineo.
 
Mkuu, S.M.P2503, wewe unakwenda mbali sana kutaka kujua kwamba kesi hii ni Isidingo toka mwanzo, na kwa sababu hiyo, haya unayoweka hapa usitegemee kamwe kwamba kesi itafika huko, haifiki.

Toka mwanzo hawajajisumbua na kesi hii isiwaonyeshe kuwa ni majuha, pamoja na kwamba ujuha wao upo nje nje kwa anayetaka kujua anauona bila shaka yoyote.

Hii kesi imeletwa kama 'formality' tu ya kuonyesha kesi ilifika mahakamani, lakini lengo likishakuwa limeamuliwa toka mwanzo, kwamba watuhumiwa watapatikana na hatia.

Hayo unayoyaandika hapo juu hakuna yeyote wa kuwalazimisha yafanyike, na hata wakiruhusu , yatafanyika kwa taratibu zao, ambazo jibu litakuwa ni wanalolitaka wao.
 
Inawezekana mawakili wa utetezi wako sahihi ukilinganisha na taarifa zilizotolewa huko nyuma BBC.

Walisema wenzake na Mbowe walishahukumiwa ila Mbowe alikimbilia mafichoni, lakini mpaka Sasa hakuna mahali mahakama au hakimu wametajwa kwamba walishaipokea hi kesi na hivyo vielezo vikafanyakazi Kama BBC ilivyotangaza.

Hi kesi ingekuwa ilishaongelewa mahakama yoyote isingemsumbua jaji naona inakuwa hii.

Penye Nia ovu lazima mazingira yatajionyesha tu. Ila kwa sababu ni mambo ya sheria tuachie mahakama.
 
Samia hana ubavu wa mabavu kumfunga mbowe na haitatokea. Subiri muone mwisho wa haya maigizo hewa.
 
Haiyumkiniki wewe ni Kingai, Mahita, au japo binamu yao [emoji16][emoji16]:

View attachment 2006223

Unasomeka vyema sana kutokea kwenye uzi huu:

Makosa ya IGP Sirro akiwa ofisini yaanze kukusanywa, Hana kinga kikatiba

Cc: Superbug
Sio kila anayepingana na ujinga wenu basi ana undugu na Mahita au Siro, bali huwa hamjitambui na wala hamueleweki mnataka nini, kila jambo kwenu ni baya tu, Alipokuwa anaongoza Jakaya mlimtukana sana, alipokuja Hayati Magufuli, mkasema Jakaya alikuwa mzuri eti mkaanza na kumlilia! alipokuja Mhe Mama yetu, mkampongeza mwanzoni na kuanza kumponda hayati aliyetutoka, na mkasema mama anaupiga nwingi! mlipoona mmekubaliwa baadhi ya hoja zenu mkataka kumpandia kichwani! akawastukia na kugundua sio watu wazuri, mkaanza kumponda tena!! eti afadhali ya hayati aliyemtangulia!! sasa mmeanza ujinga wa kupinga kila kitu! hata hamjulikani huwa mnataka nini!! habari ndii hiyo, wewe kaa na dhana yako ya kushambulia mawazo ya watu hayawasaidii, badilikeni ki fikra.
 

😁😁

 
Mkuu huyo Jaji wa Kitengo yuko kazini na hukumu yake mfukoni sisi tunaonyeshwa sinema tu lakini mchezo ulishachezwa siku nyingi sana. Mbowe SI GAIDI!
Your browser is not able to display this video.



 
Kilichoharibu hiyo kesi ni yale maneno ya wanene wa nchi na idara zake nyeti kabla ya kesi kuanza kutajwa na kusikilizwa...
 
Walishaaminishwa Mkuu na vikaragosi visema uongo vinavyopenda kujipendekeza kwamba ushahidi tulionao Mbowe HACHOMOKI!! Sasa imekula kwao nyuso ZIMEWASHUKA!!! AIBUUU!!!

Kilichoharibu hiyo kesi ni yale maneno ya wanene wa nchi na idara zake nyeti kabla ya kesi kuanza kutajwa na kusikilizwa...
 
Uzi unaongelea kesi wewe unaongelea majungu.
 
Such happenings should have be expected for something that is "Pre-meditated".
 
Kuna siku itafika ambayo hatuijui Siro na kikosi chake mmoja wao atakiri kwa kinywa chake kwamba walimbambikia Mbowe kesi ya ugaidi. Nani kati yetu akiwahi kufikiri kwamba Maalim Seif aliporwa ushindi Zanzibar kwa maguvu? Juzi kiongozi mwandamizi wa Ccm kwa kinywa chake kakiri mbele ya hadhara huo wizi.
Mungu ana njia nyingi za kufumbua watu macho.
 
Huyu Tiganga namjua baba yake mzazi, ipo siku tu
 
Huwa najiuliza Hawa vijana tunawafundisha Nini ili kesho wawe viongozi wanaoipenda nchi yao.

Badala tuwajenge kupambana na hoja tunawafundisha mambo ya mitaani kwenye serikali na mahakama. Madhara yake linazaliwa taifa la waongo, chuki na wababe.

Hivi viongozi wa dini hawawezi kumshauri rais kwa sababu wao wanapata shida kutangaza mema, ukweli lakini watu wengine wanaharibu kwa kulinda vyeo vyao.

Tunamsikia mama anasema mahakama zitende haki lakini wengine ni Kama wameweka pomba masikioni. I'll kulinda heshima ya mahakama mawakili na majaji waungane pamoja wazitengeneze hizi sheria zikae vizuri.
 
Ni wazi mahakama haitakuwa tayari kufanya uchunguzi wa kina.
 
Central pana CCTV camera pale??? Bombay la maji hamna itakuwa CCTV camera??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…