Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

Limetupiliwa mbali halikupokelewa shukrani kwa utetezi
 
Mama naye ni bonadamu huenda alipewa taarifa zilizipikwa kwa ustadi wa Siro, huenda naye akili ikamrudi baada ya kuona mwenendo wa kesi halisi.
 
Umeandika kwa hisia kali sana mkuu. Nawaza hapa kuhusu imani iliyokuwepo katika jamii zetu za Kiafrika.

Kuna imani kwamba majoka yanapokua makubwa sana katika namna ya kutisha basi huwa yanapaishwa juu kupitia baharini ili yasiangamize wanadamu
 
Hicho ndicho Jaji alipaswa kufanya. Ni muhimu haki kuonekana ikitendeka.

Mawakili wa utetezi wangeweza kupata ushahidi huo Tigo, Airtel, Vodacom, au Halotel for the sake of justice.
Na bahati nzuri askari wamekiri kwamba walikuwa wanawasiliana wenyewe kwa wenyewe toka huko Rau madukani Mpaka Dar... ni kuiomba mahakamani itoe order kwa makampuni ya mitandao na mawasiliano ku release hizo metadata toka huko moshi... mienendo yote itajulikana tu...

Kama Hilo haliwezekani, magari ya polisi yana kitabu cha mizunguko , ni kiasi cha kuomba hicho kitabu kujua kwamba lilitoka wapi kwenda wapi...

Pia gari lazima lijaze mafuta vituo vya mafuta, huko pia kuna cctv za kutosha ...

Ukija njiani kuja huku mbweni, au hata kwenda posta, kuna nanma nyingi tu kupata hizo data za ushahidi wa kisayansi..,

Hii kesi - utetezi wajumlishe sayansi na mazagazaga mengineyo... Pandora box lilisha funguliwa na prosecution kwa kumleta yule wa Tigo kuongelea miamala na wao utetezi lazima walete mtu wao ili tuione hiyo simu ilipokuwa inafanya hiyo miamala ilikuwa wapi- ndio umuhimu wa metadata...na tutajua tu siku hiyo huyo Mbowe pia alikuwa wapi... ni masuala ya ulinganifu tu... Sayansi ya simu za mikononi na metadata- yapaswa sasa zinyambuliwe ipasavyo- si mambo haya ya makaratasi na diary hadi mahakamani....
 
Kupokelewa kwa mtuhumiwa kituo tofauti au kutopewa chakula kwa wakati,bado hakufuti kosa la msingi kama limethibitika kutendwa na mhusika hizi zingine ni chenga kama za mpira, cha msingi na kinacholeta ushindi ni magoli.
Tuache porojo kama tuhuma ni ya kweli tusubiri mwisho wa kesi.
 
Samia suluhu Hassan atakuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa Rais, na Rais wa Kwanza Kuingiza nchi kwenye upinzani na Rais wa kwanza kumfunga kiongozi wa chama cha upinzani kifungo cha maisha.
 

Hoja hizi ni za msingi na majibu yake yatatuelekeza kuliko haki:



Bila majibu stahiki kwenye haya haipo kesi.

Huo ndiyo ulio utawala wa sheria.

Tuache porojo tutoe majibu stahiki pasipo uongo, hadaa, ghiliba, na janja janja.
 

Mawakili wetu wasomi waione message hii.

Tunataka haki. Wamfunge Mbowe kama ni mhalifu lakini si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…