Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Umepata wapi hili
Maana tunachotaka ni kile Mungu anachoagiza katika neno lake na sii hisia za mtu.
Hakuna ambaye yupo tayari kupotea. Dhambi zote ni sawa na inapaswa zitubiwe.
Kama kuna iliyotofautishwa kwa mujibu wa neno la Mungu ni dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu.
Sasa haya makosa mengine yanayopangwa mafungu mafungu ni wapi yameainishwa katika neno?
Tuanzie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudi kusoma thread, nimeweka maandiko,
 
Nakubal kamanda
 
HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi
Yohana 5:45
Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
 
Kama kuna mtu angekua amewahi kufa na kufufuka kutuelezea yaliyojiri baada ya kwenda huko ingekua noma sana. Mnaabudu watumishi kuliko wanavyostahili
 
Kama kuna mtu angekua amewahi kufa na kufufuka kutuelezea yaliyojiri baada ya kwenda huko ingekua noma sana. Mnaabudu watumishi kuliko wanavyostahili
Soma " Live Kutoka kuzimu - Rabbon"
 
Imeandikwa tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu navwa haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote, haijasema ukienda kuombewa kwa mtumishi fulani, utoe na sadaka.
Msamaha wa Mungu tunaupokea bure kwa njia ya imani ya Yesu Kristo. Hakuna msamaha leo hii unaopatikana kwa kutoa sadaka, huo ni wizi na udanganyifu tu.
Yesu Kristo alikwisha lipa gharama ya dhambi za wanadamu wote. Hatuhitaji tena kutoa sadaka au dhabihu kwa ajilibya maovu tunayofanya.
Mwanadamu utatoa sadaka gani itakayozidi ya Yesu kujitoa uhai wake mwenyewe ili wewe usamehewe?
Kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zako ni kuidharau dhabihu ya Yesu kwamba haitoshi. Yaani hivyo vihela vyako unavifanya kuwa bora kuliko damu au uhai wa Yesu uliotolewa kwa ajili yetu?
Leo tunatoa sadaka kama shukrani tu ya wokovu tuliopewa bure, sio kwa ajili ya kutafuta msamaha wa dhambi.
Njoo kwa Yesu upokee msamaha wa dhambi zakobzote bure, kwa njia ya imani tu
 
Hujaelewa thread. Rudia tena kusoma Hadi mwisho.
 
Mchawi akitubu mwenyewe anasamehewa, Damu ya Yesu Ina samehe wote,

Ila kujitenga na maagano ya kuzimu ya shetani ya kichawi Ili yasimfuatilie tena, mtumishi lazima ahusike.

Msibishe.
Mzee unachopaswa ni kuijenga imani yako kupitia kushirikiana na wengine na kuunganika katika maombi ya pamoja, thats why ukishatoka kwenye hayo masuala ni ngumu kusimama mwenyewe kwani unaiuwa haujajua kuomba

Lakini sio unachosema ya kuwa mpaka mchungaji awepo kuvunja maagano, ni wewe binafsi kuvunja hayo maagano

Ikiwa unang'ata na kupuliza yataendelea kujirudia
 
Ubarikiwe.
 
Cain alipomuua Abel ilikuwa wivu tu. Sasa Cain alipohukumiwa kwenda kutangatanga huko duniani. Mnadhani nyie ni kizazi gani? Kama unahangaika wewe ni wa Cain, na hayata-isha. Kama unakula kivulini wewe ni wa Abel kula na kunywa raha milele, wenye wivu wajinyonge.
Haya mambo sometimes mi naona siasa tu hizi.
 
Neno la Mungu ni HALISI.

BIBLIA ni Pumzi ya Mungu katika maandishi.

Ubarikiwe.

Amen
 
Kati ya hizo 10 ulizoandika, huyo mtumishi unayeenda kutubu kwake, ana mojawapo
 
Rudi kusoma thread, nimeweka maandiko,
Unajua fundisho la kikristo kibibilia liko hivi.
Mdhambi huziungama dhambi zake kwa Mungu hadharani lakini kisiri na kubatizwa ambapo sasa hilo humfanya kuwa mmoja wa waamini aliyepokea vipawa vya roho mtakatifu.
Sasa ndani ya waamini kama mtu atahafilika na kutenda ndivyo sivyo inaelekezwa :
Moja, jamba la dhambi alilofanya ikiwa wewe mwamini umemwona mfuate na kumweleza error yake akitubu , umempata laa hakutaka kutubu, mchukue ndg mwine pamoja nawe na akitubu mmempata.
Lakini akikaidi liharifu kanisa(uongozi).
Ataitwa na kuulizwa na akikubali kughairi uovu wake mmempata lakini akikaidi basi mhesabuni kama mmataifa kwa maana kwamba mmemkabidhi kwa shetani amfundishe.
Sii kwamba mmemfukuza kwa Mungu kwani mtu huyo baada ya kipigo anaweza kurudi kutengeneza na kumrudia Bwana.
Hakuna mahali katika ukristo palipoagizwa muamini kwenda kwa kasisi kufanyiwa upatanisho kwa kulipa chochote kama mbadala wa dhabihu.
Dhabihu ni moja tu iliyokwisha tolewa nayo ni damu ya mwana kondoo Kristo Yesu.
Yanayozidi hapo yanatoka kwa wale makristo ambao maandiko yanakiri yatawapoteza wengi hata yamkini( kama ingeliwezekana) wateule.
Uzuri mteule haiwezekani kwake kupotezwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikirudi kusoma thread na comments zangu ZOTE Kwa utulivu, Wala hata hakipo Cha kubishana, zaidi ya kutii na kulifanyia KAZI.

Soma Kanisa la kwanza lolivyoenenda kitabu Cha Matendo ya mitume, watumishi walivyoshiriki kulijenga Kanisa nk nk, ,,
 
Ikirudi kusoma thread na comments zangu ZOTE Kwa utulivu, Wala hata hakipo Cha kubishana, zaidi ya kutii na kulifanyia KAZI.

Soma Kanisa la kwanza lolivyoenenda kitabu Cha Matendo ya mitume, watumishi walivyoshiriki kulijenga Kanisa nk nk, ,,
Hakuna dhabihu iliyopelekwa kwa hao mitume kwa ajili ya upatanisho.
Kama ipo nionyeshe nipate kupona.
Mimi ni mwanafunzi daima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaelewa thread. Rudia tena

Hujaelewa thread. Rudia tena kusoma Hadi mwisho.
Nimeelewa sana. Kwenye post yako umeweka orodha ya dhambi ambazo unasema mtu akizifanya hataweza kusamehewa mpaka amwone mtumishi wa Mungu, tena akiwa na sadaka ya ukombozi. Mimi nasema hivi, hiyo sio kweli. Mtu yeyote akiamua kumrudia Bwana Yesu, hata kama awe amefanya maovu ya namna gani, Bwana Yesu ATAMSAMEHE BURE, bila ya kuhitaji kuombewa na mtu mmoja. Neno la Mungu linafundisha kuwa, mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu, naye ni YESU. Kama mpatanishi ji Yesu tu, huyo mtumishi anayetaka watu wakamwone ni wa kazi gani?
Tunapokea msamaha wa dhambi bure kwa njia ya imani tu. Hiyo sadaka ya ukombozi ni ya kazi gani wakati Yesu alishajitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu wote, pamoja na hizo ulizozitaja.
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa dhabihu ya Yesu haiwezi kumfanya mtu akasamehewa dhambi ya uzinzi au ushoga? Mwanadamu atatoa shilingi ngapi ili izidi thamani ya uhai wa Yesu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…