Mtu aliyesamehewa anaweza kurudi dhambini Kwa uamuzi wake,
Inaitwa kurudi matopeni, dhambini,
BIBLIA imeandikwa, Wala SITA lifuta Jina lako katika kitabu Cha Uzima,
Kumbe uelewe kuwa, Jina Linaweza andikwa na kufutwa vilevile.
Kusamehewa dhambi, Si kudumu katika Dhambi, Bali kuzitubia.
Mbarikiwe.
Tunashinda dhambi pale tunapompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu sio kwa kujitahidi kwetu, bali kwa kuwezeshwa. Yesu akiingia huivunja ile tamaa au nguvu ya dhambi na unawekwa huru, pia hukupatia Roho Mtakatifu ili akuongoze kwenenda sawasawa na Neno lake. cha kwanza ni kuokoka, hapo ndipo jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima na kwasababu umejikabidhi mikononi mwa Yesu, unaweza kuteleza lakini jina bado lipo kitabuni, haimaanishi leo linafutwa, kesho linaandikwa tena, keshokutwa linafutwa mtondogoo linaandikwa tena NO, cha muhimu ni wewe kujikabidhi mikononi mwa Yesu ili uwe mwana wa Mungu, ukiwa mwana wa Mungu umeshapata Mwombezi, Yesu kristo ambaye siku zote hutuombea kwa Baba kama advocate wetu ili tuendelee kudumu katika yeye au pale tunapofadha dhambi baada ya kujikabidhi kwake Yesu ndio husimama kama advocate.
1 Yoh 2:1-6
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
hii haimaanishi sasa tunaweza tu kutenda dhambi kwasababu Neema ipo au mwombezi yupo, Nooo, hatutakiwi kutenda dhambi kwasababu utendapo dhambi umeshafungua mlango mashetani kuingia, magonjwa kuingia na matatizo mengi. shetani haingii kwako bila wewe mpendwa kumruhusu. kila siku tunaishi tukiteleza, ila kwasababu tumejikabidhi mikononi mwa Yesu Mungu hatuoni sisi, anamwona Yesu kama ngao yetu, ndio maana anatuita watakatifu.
shida ni kwa wale wasiookoka, ambao hawajakabidhi maisha yao kwa Yesu, mfano ni wale wasabato wasioamini kuokoka, au ndugu zetu wanaosali kwa maria. hawana mwombezi na sio watoto wa Mungu, kwasababu wote waliompokea ndio aliwafanya kuwa watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio JIna lake. hata wewe unaweza kuwa na watoto, wakifanya dhambi huwezi kuwatupa, unawasaidia, ila wale ambao sio watoto wako mara nyingi wakikukosea unajua watajuana na wazazi wao. hata ninyi msiookoka mkiteleza (kwani sisi sote wanadamu ni wadhaifu ndio maana tunatakiwa kujitakasa kila siku) baba yenu ni ibilisi ambaye alishahukumiwa, hamjaamua kujikabidhi kwa Yesu awe mwokozi na mwombezi wenu.