Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

ninyi kama mnaona ni muhimu mnatoa kwa kusimamia mstari gani, yatupasa tuwasaidie, manake mjue tunaokolewa na kusamehewa kwa Neema tu wala si kwa matendo yetu wandugu, msije kujisifu na hizo sadaka zenu. mmepotea na ni dhihaka kwa Mungu. unapotoa sadaka unamdhihaki Mungu kwa kafara ya thamani sana ya Damu ya Yesu Kristo aliyoitoa pale msalabani, ni dhiaha na ni dhambi na ni kulilisha upepo hakuna chochote utapata.

Ebr 12:24 SUV​

na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Yesu alifanyika sadaka iliyotolewa na Mungu mwenyewe kuwa ukombozi kwa wanadamu, kama Mungu alitoa sadaka kwanini wewe usitoe sadaka?
 
Apo naona sadaka ndio imepewa kipaumbele
 
Sadaka ya pesa Si lazima, ila ni muhimu kushukuru Kwa mdomo au Kutoa, ni wewe utakavyoongozwa na Mungu .

Muhimu ni kujua kuwa, zipo dhambi huwezi malizana nazo binafsi sirini.

Amen
Yote yawezekana kwa Mungu.. Yoote yan hakuna hata moja linaloshindikana.Ni moyo wa toba tuu na kujutia yale ulioyakosa.

Halaf ujue huwez jutia na kuona umekosea kama Mungu hajakuongoza kufanya hivyo
 
Huyu ni muumini mpya. Hapo sio tu mtumishi bali muumini yoyote amepewa jukumu la kuwatoa huko gizani na kuwaleta nuruni.

Kisha afundiahwe sala na namna ya kumtegemea Mungu peke yake na kutubu dhambi zake hukohuko. Ila kwa mara ya kwanza ataelekezwa na kuongozwa.

Tatizo lililonishanganya ni aina ya dhambi ulizozitaja zinafanywa na wakristo na watumishi wengi wakubwa kwa wadogo wa kisasa mfano zinaq ni dhambi yao pendwa. Kikubwa watu waelekezwe na wafundishwe namna ya kumalizana na Mungu wao wenyewe. Kutaka wamwendee mtumishi ni dini za kikuhani za agano la kale.

Nimekuelewa kwa mtu mpya sio mwenyeji.
Hata Kwa mwenyeji pia ni hivyo.

Ikiwa u mtumishi na unafanya Oral sex na mkeo Kwa kutojua au unajua,

Mkitubishana wawili chumbani haitoshi.

Ikiwa hutaki kuamini, wewe ni mtumishi, ingia katika maombi, Muulize Roho mtakatifu aseme ikiwa nilichoandika amesema Yeye au la!!

Ubarikiwe.
 
Yeah!......Kuna dhambi ambazo muhusika mwenyekwe ni vigumu kuomba na kusikilizwa maana maagano aliyonayo hayaruhusu hayo, mfano uchawi/ushirikina, uuaji hapo lazima mtumishi amuongoze muhusika sala ya toba na kumtakasa kwa damu ya Kristo.
"Endapo haujui ukweli" hapo ni sawa, ila wewe tuseme ulikua unaujua ukweli then labda ukaenda kinyume na Mungu (ukawa mchawi and the so), kwa dhehebu langu unatakiwa ubatizwe tena na kukiri dhambi zako. There after you are good...unatoka ukiwa kiumbe kipyaaa.
Or else kama ulikua hujui ukweli, umehubiriwa vizuri ukauelewa ukweli, then ni lazima uombewe maana you understand nothing
 
Sadaka ya pesa Si lazima, ila ni muhimu kushukuru Kwa mdomo au Kutoa, ni wewe utakavyoongozwa na Mungu .

Muhimu ni kujua kuwa, zipo dhambi huwezi malizana nazo binafsi sirini.

Amen
Kwenye biblia mtumishi hakuna sadaka ya maneno. Watu wanatakiwa kutoa chochote.
Ndio maana Mungu alitoa wigo wa kuleta hata shomoro, kama huwezi kuleta ng'ombe. Shomoro alikuwa ndege mdogo na asiye na thamani sokoni.

Nafikiri watu waendelee kusisitizwa kutoa sadaka (pesa au vitu) hata kama ni 50TSH. Maana sadaka ni kitendo sio maneno.
 
Mtu aliyesamehewa anaweza kurudi dhambini Kwa uamuzi wake,

Inaitwa kurudi matopeni, dhambini,

BIBLIA imeandikwa, Wala SITA lifuta Jina lako katika kitabu Cha Uzima,

Kumbe uelewe kuwa, Jina Linaweza andikwa na kufutwa vilevile.

Kusamehewa dhambi, Si kudumu katika Dhambi, Bali kuzitubia.

Mbarikiwe.
Tunashinda dhambi pale tunapompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu sio kwa kujitahidi kwetu, bali kwa kuwezeshwa. Yesu akiingia huivunja ile tamaa au nguvu ya dhambi na unawekwa huru, pia hukupatia Roho Mtakatifu ili akuongoze kwenenda sawasawa na Neno lake. cha kwanza ni kuokoka, hapo ndipo jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima na kwasababu umejikabidhi mikononi mwa Yesu, unaweza kuteleza lakini jina bado lipo kitabuni, haimaanishi leo linafutwa, kesho linaandikwa tena, keshokutwa linafutwa mtondogoo linaandikwa tena NO, cha muhimu ni wewe kujikabidhi mikononi mwa Yesu ili uwe mwana wa Mungu, ukiwa mwana wa Mungu umeshapata Mwombezi, Yesu kristo ambaye siku zote hutuombea kwa Baba kama advocate wetu ili tuendelee kudumu katika yeye au pale tunapofadha dhambi baada ya kujikabidhi kwake Yesu ndio husimama kama advocate.

1 Yoh 2:1-6​

Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

hii haimaanishi sasa tunaweza tu kutenda dhambi kwasababu Neema ipo au mwombezi yupo, Nooo, hatutakiwi kutenda dhambi kwasababu utendapo dhambi umeshafungua mlango mashetani kuingia, magonjwa kuingia na matatizo mengi. shetani haingii kwako bila wewe mpendwa kumruhusu. kila siku tunaishi tukiteleza, ila kwasababu tumejikabidhi mikononi mwa Yesu Mungu hatuoni sisi, anamwona Yesu kama ngao yetu, ndio maana anatuita watakatifu.

shida ni kwa wale wasiookoka, ambao hawajakabidhi maisha yao kwa Yesu, mfano ni wale wasabato wasioamini kuokoka, au ndugu zetu wanaosali kwa maria. hawana mwombezi na sio watoto wa Mungu, kwasababu wote waliompokea ndio aliwafanya kuwa watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio JIna lake. hata wewe unaweza kuwa na watoto, wakifanya dhambi huwezi kuwatupa, unawasaidia, ila wale ambao sio watoto wako mara nyingi wakikukosea unajua watajuana na wazazi wao. hata ninyi msiookoka mkiteleza (kwani sisi sote wanadamu ni wadhaifu ndio maana tunatakiwa kujitakasa kila siku) baba yenu ni ibilisi ambaye alishahukumiwa, hamjaamua kujikabidhi kwa Yesu awe mwokozi na mwombezi wenu.
 
Yeah!......Kuna dhambi ambazo muhusika mwenyekwe ni vigumu kuomba na kusikilizwa maana maagano aliyonayo hayaruhusu hayo, mfano uchawi/ushirikina, uuaji hapo lazima mtumishi amuongoze muhusika sala ya toba na kumtakasa kwa damu ya Kristo.
tupatie mstari ndugu, wapi imeandikwa kwenye Biblia.
 
Apo naona sadaka ndio imepewa kipaumbele
Si Kweli,

Nenda bila sadaka ikiwa huna, tubu Kwa moyo mnyofu, utafunguliwa.

Nia ya ujumbe ni watu wa Mungu wajue zipo dhambi huwezi Fanya na ukatubu sirini ikaishia hapo.

Amen.
 
Hata Kwa mwenyeji pia ni hivyo.

Ikiwa u mtumishi na unafanya Oral sex na mkeo Kwa kutojua au unajua,

Mkitubishana wawili chumbani haitoshi.

Ikiwa hutaki kuamini, wewe ni mtumishi, ingia katika maombi, Muulize Roho mtakatifu aseme ikiwa nilichoandika amesema Yeye au la!!

Ubarikiwe.
Tatizo biblia imetaja uzinzi. Sasa uzinzi ufanyweje au kwa uchafu wa kiwango gani ni uzinzi.

Hakuna fungu la maandiko linaunga mkono unachofundisha. Mambo ya kiroho na imani lazima yawe na evidence angalau kwenye maandiko. Faith is evidence.

Ukristo wa kisasa unamapokeo mengi ambayo ni matokeo ya mawazo ya watu kwa mgongo wa mafunuo.
 
Huu mpango ulikuwepo hata kipindi cha Waisraeli, mtenda dhambi alienda kwa wazee na makuhani kutubu ili apatanishwe na Mungu

Kipindi cha mitume pia ilikuwa hivyo, hii ndio sababu Mungu ya kuweka viongozi kwenye ibada, mojawapo ya kazi zao ni kumwongoza mtenda dhambi ajutie kosa lake, kumsaidia nini kilimfanya ateleze, kusali pamoja naye na kumpa mashauri asirudie dhambi zake
mitume wepi, na umeitoa wapi hiyo kwenye Biblia? mbona mnatumiwa na shetani aisee?
 
Sadaka inayoitaka Mungu ni ile ya kutoka moyoni, sio mabaki ya pesa yako ndo utolee sadaka. Ndo maana hata yule mama mzee kwenye Biblia alietoa senti mbili, Yesu alisema alitoa zaidi kuliko wale wote hata matajiri.

Marko 12:42-44
[42]Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

[43]Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

[44]maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
 
Tatizo biblia imetaja uzinzi. Sasa uzinzi ufanyweje au kwa uchafu wa kiwango gani ni uzinzi.

Hakuna fungu la maandiko linaunga mkono unachofundisha. Mambo ya kiroho na imani lazima yawe na evidence angalau kwenye maandiko. Faith is evidence.

Ukristo wa kisasa unamapokeo mengi ambayo ni matokeo ya mawazo ya watu kwa mgongo wa mafunuo.
So wewe ni mtumishi unayeamini, muumini anaweza MKULIMA mke wa Jirani na akatubu kimya kimya na akasamehewa?

Roho mtakatifu anakushuhudia hiyo ni sawa?
 
Si Kweli,

Nenda bila sadaka ikiwa huna, tubu Kwa moyo mnyofu, utafunguliwa.

Nia ya ujumbe ni watu wa Mungu wajue zipo dhambi huwezi Fanya na ukatubu sirini ikaishia hapo.

Amen.
HAKUNA KITU KAMA IKO
 
Yesu alifanyika sadaka iliyotolewa na Mungu mwenyewe kuwa ukombozi kwa wanadamu, kama Mungu alitoa sadaka kwanini wewe usitoe sadaka?
Ukisikai sadaka, jua maana yake ni kafara. Yesu alitoa kafara ya Damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi. na hilo ndilo agano jipya, ndani ya Damu ya Yesu Kristo. sasa kama Yesu Kristo alitoa kafara la dhambi zangu, mimi natoa kafara la nini sasa ninapoenda kutubu? Mungu awasaidie muelewe.

Mt 26:28, imeandikwa: kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

hii mistari tunaweka hapa ikawahukumu mioyoni mwenu hadi siku mtakapogeuka na kufuata njia za kweli za Mungu, kwa Jina la Yesu.
 
Sadaka inayoitaka Mungu ni ile ya kutoka moyoni, sio mabaki ya pesa yako ndo utolee sadaka. Ndo maana hata yule mama mzee kwenye Biblia alietoa senti mbili, Yesu alisema alitoa zaidi kuliko wale wote hata matajiri.

Marko 12:42-44
[42]Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

[43]Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

[44]maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Unaongea sahihi kabisa.

Yesu hakukataza sadaka.

Kiwango Cha sadaka, Moyo wako uamue Kwa kadri utavyoozwa na Roho mtakatifu.

Amen
 
Katika Dini Yetu Sisi Mungu Hupokea Toba Haraka Kwa Kukaa Peke Yako Na Muumba Wako Kutubu Pasi Ya Kumshirikisha Mtumishi Wa Mungu Binadamu Mwenzako Ambaye Na Yeye Ni Mzinzi Na Muasherati Oral Sex Sio Dhambi Katika Dini Yetu Ila Tunaambiwa Tu Ni Vizuri Kuepuka Hasa Hasa Kunyonya Papuchi Maana Unaweza Pata Maradhi Ila Kama Huhofii Nyonyaneni Kama Inawapa Faraja Kwenye Ndoa Yenu Karibu Kwenye Uislamu Dini Isiyo Na Manabii Wa Hovyo Hovyo Kutoka Uyole
 
So wewe ni mtumishi unayeamini, muumini anaweza MKULIMA mke wa Jirani na akatubu kimya kimya na akasamehewa?

Roho mtakatifu anakushuhudia hiyo ni sawa?
Ndio inawezekana vizuri, Mungu anaangalia roho yako kaka...anaangalia kama umeikana na kutubu dhambi yako. Ndo maana yuko tayari kukusamehe dhambi yako wakati wowote utakapomuita na kuungama dhambi husika.
Mungu hana limit ya dhambi za kusamehe, na as long as dhambi zote ni sawa...WEWE TUBU PEKE YAKO, UKIWA CHUMBANI, ITAJE DHAMBI YAKO KWA MANENO NA UIKIRI NA KUIUNGAMA.
 
Sadaka inayoitaka Mungu ni ile ya kutoka moyoni, sio mabaki ya pesa yako ndo utolee sadaka. Ndo maana hata yule mama mzee kwenye Biblia alietoa senti mbili, Yesu alisema alitoa zaidi kuliko wale wote hata matajiri.

Marko 12:42-44
[42]Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

[43]Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

[44]maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
wewe hujaelewa mjadala. mleta mada amesema ukifanya dhambi hizo zlizoorodhesha, huwezi kusamehewa hadi uende kwa mchungaji akuombee na ukiwa na sadaka. hajataja mstari wowote. hapa hatuongelei sadaka kiujumla. swali letu kwake, Damu ya Yesu Kristo ilimwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi, sasa sadaka twende nayo ya nini? siku zingine sadaka ni muhimu kutoa ila pale unapotubu unaenda na sadaka kutubia ya nini wakati Yesu alishalipa gharama ya dhambi zako? unalipia dhambi, kitu gani cha thamani utampa Mungu akusamehje dhambi nje ya Damu ya Yesu? ndio hawa manabii wa uongo wanajaribu kuuambia umma.
 
Back
Top Bottom