Kasome kisa cha Sauli (Paulo) baada ya kutokewa na Yesu njiani na kupigwa upofu.
Yesu alimtuma Anania kwenda kumuwekea mikono Paulo na kumwambia cha kufanya.
Matendo ya mitume 9: 1-19
tupatie mstari ndugu, wapi imeandikwa kwenye Biblia.
Matendo ya Mitume 9 1
<br>Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
Matendo ya Mitume 9 2
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Matendo ya Mitume 9 3
Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
Matendo ya Mitume 9 4
Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
Matendo ya Mitume 9 5
Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
Matendo ya Mitume 9 6
Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.
Matendo ya Mitume 9 7
Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.
Matendo ya Mitume 9 8
Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
Matendo ya Mitume 9 9
Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
Matendo ya Mitume 9 10
Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.
Matendo ya Mitume 9 11
Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Matendo ya Mitume 9 12
naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
Matendo ya Mitume 9 13
Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
Matendo ya Mitume 9 14
hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
Matendo ya Mitume 9 15
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
Matendo ya Mitume 9 16
Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
Matendo ya Mitume 9 17
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 9 18
Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
Matendo ya Mitume 9 19
akala chakula, na kupata nguvu.
Kasome mwenyewe kisa cha Kornelio yule muitalia, alipotokea na malaika aliambiwa apelekw watu kule Yafa akamlete Simoni Petro ili amwambie cha kufanya..............umejiuliza kwanini malaika hakufanya hilo jukumu yeye, Ila alimpa maelekezo amtafute Petro ?
Matendo ya mitume 10:1-31
Nenda kasome kisa cha yule towashi kutoka hapo Kushi (Ethiopia) na Filipo, kumbuka yule towashi alikuwa akisoma chuo cha nabii Isaya Ila hakukielewa (yaani Isaya 53:1-), Ila ilibidi Roho Mtakatifu ampeleke Filipo ili akamweleweshe na kumbatiza yule towashi.
Mpaka hapo unaona Mungu hutenda kazi kupitia watumishi wake.
Matendo ya mitume 8:25-38