Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Sadaka ni ibada, ukiwaambia watu wasitoe sadaka ni sawa na kuwaambia wasifanye ibada.Wandugu nyote msomao humu, msiwasikilize hawa manabii wa uongo. jueni neno hili moja tu kwamba, TUMEOKOLEWA KWA NEEMA, WALA SI KWA MATENDO YETU, MTU YEYOTE ASIJE AKAJISIFU. hakuna sadaka yeyote inayoweza kutolewa ili usamehewe dhambi, Yesu anasamehe dhambi bure. hata ukiamua kutoa sadaka usitoe kwasababu umesamehewa, toa kwamba unamtolea Mungu kwa kawaida tu, Mungu angekua anathamini wenye sadaka peke yake, basi kina bakhresa peke yake ndio wangefika mbinguni. MUNGU HANUNULIKI, HAHONGWI, hizo mnazohonga wanakula hao manabii na mitume wa uongo na wake zao, ndio maana wamejenga hadi mahotel kutokana na sadaka zenu. wanatembelea magari ya milioni 400 kuja kanisani kusalisha na kukusanya sadaka toka kwa watu ambao hawajui wakirudi church watakula nini,wagonjwa, wenye shida, wanamchangia mafuta kila siku yeye anaishi kama mfalme ila kondoo wanaishi kama mbwa tu.
Be careful....