Dhana: Virusi vya Corona ni gonjwa la kutengeneza na atakayeumia zaidi ni mtu mweusi

Dhana: Virusi vya Corona ni gonjwa la kutengeneza na atakayeumia zaidi ni mtu mweusi

Kwa life style ya Dar huwa najiuliza inakuwaje homa ya ini haijashamiri sana. Ni Mungu ndio anaejua kwa kweli
Imekuuuma kwamba Dar haina homa ya ini, hata wazungu inawauuuuuma kwamba Corona imegoma kuingia Afrika..
 
Huu ugonjwa unapungua sana makali sehemu za joto ila sehemu za baridi kali ni hatari zaidi.
Kuna expanation ya ziada unaweza kutupa juu ya hili, maana nimevutiwa nalo. Ni kwamba virusi vinasambazwa na agents wapendao baridi au?
 
Imekuuuma kwamba Dar haina homa ya ini, hata wazungu inawauuuuuma kwamba Corona imegoma kuingia Afrika..

Kwamba Dar haina homa ya ini !!!!.....

Kwamba Corona imegoma kuingia Africa 😂

Mkuu wewe ni next level aseee. salute
 
Nadhani kuna baadhi ya mabalaa Mungu anasemaga tu Hawa jamaa wasiyapitie, no matter what, nafikiria mlundikano wa kwenye mwendo kasi jioni, full kugusana na mi jasho halafu eti bado tunadunda tuu kitaaa,

Sent using Jamii Forums mobile app

True dat mkuu yaani kwa life style yetu ilibidi hivi vitu viwe worse
 
Imekuuuma kwamba Dar haina homa ya ini, hata wazungu inawauuuuuma kwamba Corona imegoma kuingia Afrika..
mdau hajatoa ushauri, anazungumzia tu ukweli wa mambo yalivyo, hayo ya kusema kwamba inamuuma nadhan ni wewe unayesema
One minute!!! Unasema dar haina Homa ya ini??

Sent from my BKK-AL10 using Tapatalk
 
Kwa life style ya Dar huwa najiuliza inakuwaje homa ya ini haijashamiri sana. Ni Mungu ndio anaejua kwa kweli
Nilivyosikia ni kuwa 90% ya adults wanaokuwa exposed wanapona bila kujijua kutokana na Kinga zao za mwili, 10% acute na baadhi wachache ndio wanakuwa Chronic ambao ndio hao tunaona wanaougua homa ya ini.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa life style ya Dar huwa najiuliza inakuwaje homa ya ini haijashamiri sana. Ni Mungu ndio anaejua kwa kweli
Nawashangaa watu wanavyosema homa ya corona waniogoopaa wakati kuna uzi unatembea wa kula masihara najisomea nasema ukimwi tupa kule hili gonjwa la Ini sasa ina maana watu hawajauelewa huu ugonjwa na maambukizi yakee au dharau kupima kwenyewe hakuna hata anaejishighulisha ni wachache sana elimu inahitajika kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ufafanuzi wako mzuri
JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.

Leo hii dunia nzima inaishangaa Afrika kwa mambo mawili makuu : La kwanza ni umaskini wake, na pili jinsi lilivyojikita katika mambo ya Imani . Bara pekee lenye idadi kubwa ya watu wanaoishi kwa kuamini kitu kinachoitwa Mungu kwasasa ni Afrika tu. Jambo ambalo huwezi kuliona katika bara lingine lolote duniani.

Leo hii tutaona sababu za kibiblia ni kwanini tupo hivi, ili na wewe ujue ni wapi unapopaswa usimame..katika nafasi yako Afrika.

Watu wasioamini Mungu, wala wasioisoma biblia wanatafsiri umaskini wa waafrika ni kutokana na uvivu wao, na ujinga wao, lakini ukweli ni kwamba zipo jamii zenye watu wavivu kuliko hata waafrika, lakini bado wanao maendeleo makubwa zaidi yetu,.

Vilevile licha ya biblia kutuonyesha kuwa maendeleo makubwa tangu zamani yalianzia katika bara la Afrika lakini historia pia inathibitisha hilo kwamfano yale mapiramidi yalio kule Misri, na Ethiopia hadi leo hii hakuna Uinjilinia wowote umewahi kufikia ile teknolijia..Hiyo ni kuonyesha kuwa sio kwamba waafrika ni wajinga kama wanavyofikiriwa..

Lakini Biblia inatuambia kuwa ni yeye Mungu mwenyewe ndiye aliyeifanya Afrika kuwa duni kuliko mataifa yote ulimwenguni. Na hiyo yote ni kwasababu ya miungu yao na sanamu zao..Ukisoma Kitabu cha Isaya sura ya 19 chote na Ezekieli sura ya 29 vinaeleza unabii juu ya bara la Afrika. Hatuwezi kuandika aya zote hapa kwa nafasi yako unaweza ukazisoma..lakini tutaangalia baadhi ya aya..

1. Awali ya yote biblia ilishatabiri kuwa waafrika watawaliwa:

Tusome

Isaya 19:4 “Nami nitawatoa hao Wamisri na kuwatia katika mikono ya bwana mgumu; na mfalme mkali atawatawala; asema Bwana, Bwana wa majeshi”.

Sasa kumbuka sehemu nyingine biblia inapoitaja Misri ujue inawakilisha bara zima la Afrika..

Ilishatabiri kuwa juu ya utawala wa wakoloni, wa kibepari..

2. Vilevile ilishatabiri kuwa itachukuliwa utumwani, kama vile wana wa Israeli walivyochukuliwa utumwani:

Ezekieli 29:12 “Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
13 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Mwisho wa miaka arobaini nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hizo kabila za watu, ambazo walitawanyika kati yao;
14 nami nitawarejeza Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi, hata nchi ya kuzaliwa kwao; NA HUKO WATAKUWA UFALME DUNI.
15 UTAKUWA DUNI KULIKO FALME ZOTE; wala hautajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale tena juu ya mataifa”.

Unabii, huo ulitimia, Afrika ilianza kuangia utumwani na kutawaliwa kuanzia karne ya 16 na mpaka kufikia karne ya 19, utumwa ulikoma, hiyo ni miaka 400 kama vile wana wa Israeli walivyokaa Misri. Na Mungu alishasema itakuwa duni kuliko mataifa yote.

Lakini Kwanini Mungu aliruhusu hivyo? Je analipiza kisasi au anawachukia waafrika?

Jibu ni hapana sura hizo mbili zinatuonyesha Mungu alimua kufanya hivyo kwa watu wa Afrika kwasababu ya miungu yao, na sanamu zao, na uchawi wao, na uganga wao, na upigaji ramli wao (Isaya 19:3), ambavyo vimefaraka naye.. aliwadhoofisha kwa makusudi ili wajue kuwa hivyo vitu haviwezi kuwasaidia na kwamba wakati umefika sasa Mungu anawahitaji waafrika wamtumike yeye.

Kama tu leo hii, Mungu ameliadhibu bara hili lakini bado unaona waganga na uchawi bado ni mwingi, angaliacha katika mafanikio yake liwe kama mabara mengine yaliyofanikiwa duniani unadhani lingekuwaje? ndio lingekuwa chanzo cha machukizo yote ya ulimwengu mzima kotekote..rohoni na mwilini…Uchawi uliokuwepo kuanzia Misri(ambayo ipo ndani ya Bara la Afrika) ulikuwa ni wa viwango vya juu sana..walikuwa na uwezo wa kubadilisha fimbo kuwa nyoka. Mungu asingeukomesha saa hii ungekuwa umefikia viwango gani?

Hivyo Mungu ametupiga ili tumgeukie yeye hiyo ndio sababu kuu..Na jambo hilo ni kweli limezaa matunda, kwasababu leo hii Neema ya Mungu kweli ipo Afrika, idadi kubwa ya watu waliomaanisha kumtafuta MUNGU ipo Afrika, Hapo ndipo Mungu alipotuponyea..

Kitendo cha sisi kuchukuliwa utumwani, na kutawaliwa na mabepari, kulitufanya sisi tumtafute Mungu wa kweli.

Soma hapa biblia inavyosema..

Isaya 19:20 “Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.
21 Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza.
22 NAYE BWANA ATAPIGA MISRI, AKIPIGA NA KUPONYA; NAO WAKIRUDI KWA BWANA, ATAKUBALI MAOMBI YAO NA KUWAPONYA.
23 Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
24 Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia;
25 kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki, akisema, WABARIKIWE WATU WANGU MISRI; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu”.

Unaona, Mstari wa 21 unatuambia waafrika watajulikana na Bwana, watamtumikia kwa dhabihu na matoleo.. Lakini vilevile anasema atapiga na kuponya… na mstari wa 25 Mungu anasema, WABARIKIWE WATU WANGU MISRI.

Hivyo suala la umaskini wa Afrika, limeruhusiwa kabisa kwasababu hii, ili tumrudie yeye kwasababu anatupenda..

Umaskini wetu umesababishia utajiri wa Imani kwa Mungu..na ndio maana biblia inasema..

Yakobo 2:5 “…..Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao”?

Hivyo itakuwa ni jambo la kushangaza, Mungu amekuweka wewe na mimi katika nchi kama hizi, halafu bado huielewi sauti ya Mungu inataka nini kwako hutaki kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu anayekupenda… Unaishi katika nchi ambazo utasikia injili kila kona ya barabara inahubiriwa,..lakini bado unapuuzia na kudhihaki, mataifa mengine wanaagiza wamishionari kutoka Afrika wawapelekee Neno la Mungu, lakini wewe unaichezea neema hii…Sasa hata hichi ukikikosa, ni nini basi utakuwa nacho ndugu?

Kumbuka hata hivyo neema hii nayo haitadumu huku milele, hivi karibuni Mungu atairejeza Israeli ilipoanzia, biblia inatabiri hivyo, na hapo ndipo mataifa yote ulimwenguni yataurudia upagani waliokuwa nayo mwanzoni na kwa pamoja sasa yatafanya kazi na mpinga-Kristo, ili baadaye yaje kuungana kuishambulia Israeli katika vita ile kuu ya mwisho ya Harmagedoni.. (Neema ni kama jua linachomoza upande huu na kuzama upande ule hivyo sio ya kudumu..ni kitu kinachohama..mataifa mengine Neema ya kuisikia injili haipo kabisa..yaani ile nguvu ya kuvutwa haipo…muda wao ni kama ulishapita..Na sisi muda wetu unakaribia kuisha, na neema hii itahamia Israeli..huku itakuwa kuamini injili ni ngumu kama ilivyo mataifa ya magharibi sasahivi)

Lakini sisi tulioipokea neema ya kumwamini YESU KRISTO na sio mtu mwingine yeyote, tutakuwa tumeshakwenda kwenye unyakuo kama haijahamia Israeli..Lakini wewe ambaye unaupenda ulimwengu huu, ambaye bado unaipenda miungu ya ukoo wenu, unakwenda kwa waganga, unapiga ramli, unadharau injili ya msalaba ambayo unapewa leo bure bila malipo yoyote..basi ujiandae tu na kupigwa na mkono wa Bwana kila siku, na baadaye kuishia katika ziwa la moto..

Hizi ni nyakati za hatari, na kila siku tunaona mabadiliko ya dunia..muda huu ni wa nyiongeza tu, Unyakuo ni wakati wowote, parapanda italia wafu watafufuka.. Je! Umejiweka tayari..Jibu lipo moyoni mwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Sijaona eneo umeelezea huo utafiti wako au umeelezea nadharia yako kisayansi

2. Hakuna ugonjwa unaitwa Ebora

3. Wizara ya Afya ilishatoa matangazo yanayoelezea dalili na njia za kujikinga kwenye vyombo vya habari.

4. Huna jipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaonekana hufuatilii kbs vyombo vya habari vya kimataifa mkuu
Kichwa chahusika, huu ni utafiti wangu, japo kuwa kuna mtu atasema umetoa wapi chanzo cha taarifa, sasa hata uko unakotaka kuamini ni watu kama mimi tu, na ikiwezekana nimewazidi baadhi ya mambo.

Unajua, Afrika, tunashida sana, JF, story nyingi ni migegedo tu, lakini amini amini nakwambia, huyo Kirusi Corona akiingia hapa, tutadondoka kama kumbikumbi, yawezekana mimi sio mfuatiliaji mzuri wa habari, sijasikia chochote kuhusu preventive measures, kutoka katika Wizara ya Afya au Mambo ya Ndani, kupambana dhidi ya gonjwa hilo hatari la Corona, endapo litaingia hapa Tanzania, kupitia nchi jirani au Airport, kama serikali ina mikakati gani na imejipanga vipi endapo Corona itaingia Bongo! Au tunasubiri gonjwa liingie kwanza ndio tuanze kukimbizana.

Wabongo, tunaponeaga chupuchupu sana, dhidi ya haya magonjwa ya milipuko, huwa hatuna historia ya kuyapata, kama ebora nk, japokuwa Ebola ipo jirani, Congo na Uganda kama sijakosea, imagine Kipindupindu tu, kilivyotutoa jasho,

Tahadhari, najua viongozi wetu wamejisahau, wapo kupambana na wakina Zitto Kabwe na Lissu,mambo ya uchaguzi nk, Corona ikiingia hapa Tanzania, tumekwisha vile biashara zetu zinahusiana na China, Kariakoo yote ni Beijing, Shanghai na Guangzhou, tumekwisha wazee, nawambieni kweli, nimemaliza lengo langu ni kuwakumbusha.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa chahusika, huu ni utafiti wangu, japo kuwa kuna mtu atasema umetoa wapi chanzo cha taarifa, sasa hata uko unakotaka kuamini ni watu kama mimi tu, na ikiwezekana nimewazidi baadhi ya mambo.

Unajua, Afrika, tunashida sana, JF, story nyingi ni migegedo tu, lakini amini amini nakwambia, huyo Kirusi Corona akiingia hapa, tutadondoka kama kumbikumbi, yawezekana mimi sio mfuatiliaji mzuri wa habari, sijasikia chochote kuhusu preventive measures, kutoka katika Wizara ya Afya au Mambo ya Ndani, kupambana dhidi ya gonjwa hilo hatari la Corona, endapo litaingia hapa Tanzania, kupitia nchi jirani au Airport, kama serikali ina mikakati gani na imejipanga vipi endapo Corona itaingia Bongo! Au tunasubiri gonjwa liingie kwanza ndio tuanze kukimbizana.

Wabongo, tunaponeaga chupuchupu sana, dhidi ya haya magonjwa ya milipuko, huwa hatuna historia ya kuyapata, kama ebora nk, japokuwa Ebola ipo jirani, Congo na Uganda kama sijakosea, imagine Kipindupindu tu, kilivyotutoa jasho,

Tahadhari, najua viongozi wetu wamejisahau, wapo kupambana na wakina Zitto Kabwe na Lissu,mambo ya uchaguzi nk, Corona ikiingia hapa Tanzania, tumekwisha vile biashara zetu zinahusiana na China, Kariakoo yote ni Beijing, Shanghai na Guangzhou, tumekwisha wazee, nawambieni kweli, nimemaliza lengo langu ni kuwakumbusha.

Nawasilisha.
Existence of nature...Mungu ni fundi ingawa tahadhari inatakiwa sn!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna expanation ya ziada unaweza kutupa juu ya hili, maana nimevutiwa nalo. Ni kwamba virusi vinasambazwa na agents wapendao baridi au?
Kwa mujibu wa watafiti virusi vya corona vinakuwa imara na vinaishi muda mrefu zaidi kwenye sehemu za baridi ukilinganisha na sehemu zenye joto ambapo virusi vinakuwa dhaifu na vinaishi muda mfupi. Kwa kipindi hiki China ni msimu wa baridi ndiyo maana virusi vinasumbua ila kuanzia mwezi wa tano joto litaongezeka na litasadia kupunguza makali na uimara wa virusi kuishi muda mrefu na maambukizi yataanza kupungua muda huo.
 
Mafua kwa Mwafrika aka Ngozi nyeusi hayafui dafu...labda wategeneze Corona mpya so hii.
Mleta mada anashindwa kujua kwamba Mwafrika ni namba nyingine katika kuambukizwa magonjwa na kustahimili maaambukizi. Waulize Kimeta, SARS nk viliishia wapi? Mungu ibariki Afrika
 
Back
Top Bottom