Dhana ya Kuinuana Kiuchumi baina ya Wanafamilia; Kuna haja unapompa ndugu yako Mtaji wa biashara umtoze riba ili kuongeza uwajibikaji?

Utagombana nao tu...
Unajua kitu napata wasiwasi ni kuona kesho ya watoto wake. Yaani mtu akiwa hohehae sasa atashindwa hata kusomesha watoto wake vizuri pamoja na kuwaandalia kesho yao vizuri. Bahati mbaya anashindwa kujitambua
 
Ukimpa mtaji ndugu ili ajitegemee ni jambo jema maana unajipunguzia mzigo japo kuna ndugu wasiojitambua ukimpa anakula tu.

Ukimpa mtaji mara 2 halafu atafune tu(baada ya kujiridhisha ametafuna) mi naona bora umuache kwanza apate leson vinginevyo atajua vipo vya kuchota tu na kutumia heri lawama kuliko hasara.
 
Asante mkuu.
Ndugu yangu alinipambania toka nikiwa form 1 mpaka nafika chuo kikuu yuko na mimi. Tena akiwa anafanya kazi ya 120,000 per month. Ndio mana hata sina muda wa kumfuatilia sana. Hanywi pombe wala kuwa marafiki wa hovyo
Hongera mno,

Huyu ndugu yangu, akiwa hana hela anatulia na kujifanya anamawazo chanya lakini akizipata ni mwendo wa kunywa na michepuko tu
 
Unajua kitu napata wasiwasi ni kuona kesho ya watoto wake. Yaani mtu akiwa hohehae sasa atashindwa hata kusomesha watoto wake vizuri pamoja na kuwaandalia kesho yao vizuri. Bahati mbaya anashindwa kujitambua
Ikiwa mwenyewe hawezi kukisimamia hapo ni shida....
 
Mtaji huu wa tatu, kabla sijampa aliniomba tukakutana akanieleza vizuri biashara anayotaka kuifanya. Akajieleza sana namna atakwenda kuizalisha na kupata faida, baada ya kumpa zikapita wiki 3 malalamiko yameanza. Manake hana muda mrefu anakwenda kumaliza mtaji tena
 
Ikiwa mwenyewe hawezi kukisimamia hapo ni shida....
Unajua kuna Muda wanaume wengine huhisi hata baada ya miaka 10 ijayo ataendelea kuwa na nguvu zake zile zile alizokuwanazo akiwa na miaka 25.
Wanashindwa kujua kuwa Uzee unakaribia
 
Unajua kuna Muda wanaume wengine huhisi hata baada ya miaka 10 ijayo ataendelea kuwa na nguvu zake zile zile alizokuwanazo akiwa na miaka 25.
Wanashindwa kujua kuwa Uzee unakaribia
Ni kweli usemayo, kubwa kutokujitambua
 
Uwape mtaji? Kwani wewe ulipewa na nani?
Ndo hapo tangu mwanzo alipokosea kuwapa mtaji yeye, jukumu la kuwapa mtaji lilikuwa la wazazi wako iwapo ulitaka kuwasaidia ungewapa wazazi wako ndo wawape na kuwapa maonyo ya displine Kama wazazi na wakiwa wanawajibika kwao, wewe ulitakiwa uwe nao Kama ndugu yao bila kujishughulisha na mipango yao na kama kusaidiana ugesaidiana nao kwenye mambo yanayokuhusu, na siku zote ukiwa na hela usipende kujionyesha unazo sana na unaweza kubeba majukumu ya mwingine ila sisemi usisaidie ndugu unachotakiwa kufanya nikusaidia msaada mtu anayejutia hali yake kwa matendo na siyo kwa maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…