Dhana ya Kuinuana Kiuchumi baina ya Wanafamilia; Kuna haja unapompa ndugu yako Mtaji wa biashara umtoze riba ili kuongeza uwajibikaji?

Changamoto usipompa mtaji utakaomwezesha kufanya kazi na kujikimu italazimu kila tatizo unapigiwa simu wewe tu kusaidia, kwahiyo nilidhani unapowainua wawili, watatu inakupunguzia mzigo. Bahati mbaya wenzako hawa feel maumivu yako, kwani unajikuta umejinyima kuweza kumpa mtaji
Ni kweli mkuu ila waweke chini ongea nao waambie jinsi ilivyo, na ikiwezekana ukitaka kumpa mtaji ita ndugu wote waweke chini unawaambia Kua ndio mtaji wa mwisho akiuua basi ni shauri lake

Wakati mwingine ni Bora Lawama Kuliko Fedheha mkuu
 
Ndugu wa hivi wengi hawana msaada mbeleni na ni wabinafsi sana. Ukijitoa sana kuwasaidia wanaona ni wajibu wako siku ukifulia ndio utaona dharau na rangi zao. Jambo la msingi mpe mtaji lakini mkubaliane akiupoteza huna deni kwake na ukaze hasahasa.
Ninavyojua hata wakifanikiwa kwenye biashara watakutaka tu wewe ndio utatue changamoto zote. Tengeneza mazingira rahisi kwako na usisahau kujiwekea mazingira yako mazuri mbeleni.
 
Usemacho ni sahihi Mkuu, undugu kweli lawama.

Nitazingatia ushauri wako
 
Ni kweli mkuu ila waweke chini ongea nao waambie jinsi ilivyo, na ikiwezekana ukitaka kumpa mtaji ita ndugu wote waweke chini unawaambia Kua ndio mtaji wa mwisho akiuua basi ni shauri lake

Wakati mwingine ni Bora Lawama Kuliko Fedheha mkuu
Nimemwambia tayari, sitaweza kumpa mtaji mwingine akiua niliompa
 
Uzee ni majukumu.....
Hahaha.....upo sahihi, unaweza kuwa kijana kutokana na majukumu ukajikuta ushazeeka.

All in all, muda wa kujiandalia uzee ni sasa
 
Kiroho Riba ni mbaya kwa ndugu yako wa damu mkuu
Sisi kikwetu ndugu hatukopeshani tunasaidiana, mwenye uwezo na roho nzuri huwasaidia wenzake waliokwama. Hayo mambo ya riba kwa ndugu wa damu ndiyo nimeyasikia leo.
 
Vipi unamsaidia ndugu then kila baada ya muda anapoteza mtaji uliompa, hauoni umefika muda wa wao kuwa na kitu kama rejesho fulani ili ajihisi kuwajibika kwa mtaji uliompa? Ili aongeze umakini
 
Nimemwambia tayari, sitaweza kumpa mtaji mwingine akiua niliompa

Tatizo jingine ni wazazi , wao wanajua umempa mtaji mara tatu na hakuna cha maana alichofanyia. Badala ya kumkanya muhusika juu ya mwenendo wake mbaya wanaanza kumkingia kifua ili umsaidie tena kisa ndugu yako. Upuuzi wa hivi huwa sikubali. Mwisho wa siku namchanganya muhusika na hao wazazi wake ambao wanashindwa kumkanya mtoto wao
 
Vipi unamsaidia ndugu then kila baada ya muda anapoteza mtaji uliompa, hauoni umefika muda wa wao kuwa na kitu kama rejesho fulani ili ajihisi kuwajibika kwa mtaji uliompa? Ili aongeze umakini
Tatizo ni wewe unayempa ndugu mtaji mara tatu anauunguza alafu unalalamika, tena ukijua kabisa hana nidhamu ya pesa. Kwa hiyo akitoa rejesho ndo hatokula mtaji?
 
Vipi unamsaidia ndugu then kila baada ya muda anapoteza mtaji uliompa, hauoni umefika muda wa wao kuwa na kitu kama rejesho fulani ili ajihisi kuwajibika kwa mtaji uliompa? Ili aongeze umakini
Kuna familia zina shida...laana sio laana bora hata ww unawapa riba
 
Back
Top Bottom