Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Hoja imeanzia mtu kasema hatua za mwanadamu ni kuzaliwa, ndoa na kufa. Wewe unaonaje?
Ndoa ni basic need kwa baadhi ya watu Kama Abrianna na Samcezar
Demi Huu ni mjadala tu, don't take it too personal maa'm, nimeelewa point yako kwamba ndoa sio basic need and i did not urgue further, sema to we are trying to understand kwamba hata kama ndoa sio basic lakini at some point tutawahitaji wanaume kwa namna moja au nyingine kwa hiyo ni muhimu asiachwe nyuma
 
I didn't take it too personal Madame, nilikuwa tu najaribu kuipata concept yenu ikashindikana kupenya akilini. Tuko pamoja
 
Actually ni 100 years to come
 

No, may be you didnt get me. Things won't get worse,unless tungekuwa kwa sasa hivi kwenye the same position boys and girls kielimu halafu ikaja campaign msomeshe mtoto wa kike,hapo results ofcourse ingekuwa girls watakua front na boys behind, ila kilichopo ni GAP, girls are behind kwenye mzani, na ndio basis ya 'msomeshe mtoto wa kike'. Encourage girls

Again kumsomesha mtoto wa kike haimaanishi mtoto wa kiume atabaki nyuma, kama nilivyokuambia unless kuwe na shift major shift/change kwenye system ambayo labda ita deter boys kuchukua education opportunities then ndio tutaobserve boys being left behind,otherwise basing on current trends this is not happening or going to happen, so we might as well encourage girls to get education,

ni kweli wanaume wengi wanakua intimidated na mwanamke msomi,ila hao hao baadhi hupenda mwanamke anaye wachallenge, nchi nyingine actually mwanamke mwenye degree ndie anayeolewa!

Kuhusu nafasi kuchukuliwa na wanawake,no problem, is what your qualifications got you there,not because you are a woman,infact unaonyesha kuna stereotype, sexism existing us women need to challenge...ole wenu mniite feminist...! 🤣
 
South Africa wameshaanza
Wanataka kuhalalisha Polyandry
Mke mmoja kuwa na Mume zaidi ya mmoja...

huko ndo tunaelekea tusipokua makini...

japo SA wazushi sana hii kitu hata wazungu hawana
 
Hii kitu ya haki sawa kwa wote, imechangia ongezeko la mashoga na wasagaji, mtoto wa kiume na wakike wote wanafanya majukumu sawa kwa sawa bila mipaka.

Matokea yake jike anakua jike dume hadi usagaji na dume anaona yeye ni sawa tu na mwanamke hadi ushoga.

Hii kitu ya usawa iangaliwe kwa umakini sana.
 
I completely understand you dear , Hii discussion ni ndefu na ni pana sana, recently wanawake wamekua front kuanzia kwenye biashara, maofisini,hata mashuleni, ukienda sokoni 96% ni akina mama ambao wanatafuta kwa ajili ya watoto wao, tena wanachakarika kweli, wanaume wako wapi? Kwa nini akina mama wanatafuta na kulisha familia? What went wrong? Ukienda maofisini asilimia kubwa ni akina mama, nafasi kubwa nyingi kwa sasa zimeshikikiwa na wanawake, watoto wengi ukizungumza nao watakwambia my mom does evetything for me, au atakwambia hapa nilipo nimefika kwa sababu ya jitihada za mama, hii ndio gap ninayoizungumza, these people should not left behind na tunahitaji kuona kizazi kile cha wanaume wenye kusimamia familia, wenye kuwajibika ndani ya familia na sio kuacha mzigo kwa mama, wanaume wenye kuchukua majukumu wanapowatia wanawake mimba, kama tumeamua kufanya women empowerment tusiwainue wanawake ili waje kutekeleza wajibu wa mwanaume kwenye jamii, bali tuwainue ili waweze kupata haki sawa na hawa wanaume

Naongelea misconcept ya hii kampeni ya kuwainua wanawake na mdhara yake, jamii inaamini kwamba mwanamke anasoma ili aje kufanya majukumu ya mwanaume, aje alishe familia, mpaka wanaoa siku hizi, mwanamke anaoa analipa mahari kabisa

Its okay kushiriki kwenye kuhudumia familia lakini its not okay jukumu zima la kuhudumia familia alibebe mama

Hata uwe na mshahara mkubwa kiasi gani au uwe na elimu kiasi gani,kuna muda unahitaji kudekezwa kama mwanamke, unahitaji kufanyiwa shopping au kuhudumiwa yaani that is nature, ila wanawake wa sasa maskini anahudumia familia, anamuhudumia mume, na bado anajihudumia mwenyewe
 
Asante sana uliyewakilisha hoja hii
Nilikuwa natafuta muda wa kuandika mada hii ila kabla sijafanya hivyo wewe umefanya na umeweka vizuri zaidi kuonyesha utashi wako
Jambo hili likinyamaziwa ni bomu litakaloangamiza wengi
Na sina uhakika kama wanaosimamia hili hawajui madhara yake ya baadae
 
Lengo langu sio kuongelea udini lakini nikiangalia juhudi za dini ya kiislamu kupambana ili mwanaume abaki kuwa kichwa katika jamii dini hi ikosahihi japo Mimi ni mkiristo jina tu Ila naamini katika uweza wa Mungu pekee

Haya Mambo ya haki sawa ni bomu ambalo litakapolipuka Hali itakuwa mbaya na hili halihitaji maelezo

Na yote kwa yote huu ni mpango wa shetani Kama ilivyo ajenda zake kuhakikisha anauteka ulimwengu kwa kutumia jinsia ya kike(refer bustanini Edeni)

Yajayo yanasikitisha mno
 

Mnhhh, ndio kuna wanawake wanachakarika kulisha familia zao, cha kushangaza hutaki wapate elimu waongeze ufanisi katika sehemu zao za uzalishaji.,..

..tunapigana vita ya kiuchumi so i understand this pose a challenge to us, and in order to survive things might continuosly change,in this economic hardship women came to 'kujiongeza' kwa hio tumeona wanawake hawakai tena nyumbani, ,walikua wanakaa nyumbani sababu conditions zilikuwa zinawa - 'favour', ..i assume kizazi cha wanaume wenye kusimamia familia kilipotea baada ya kuanza kupigana vita ya uchumi,(mimi sikuwepo kizazi kilichopita) ila environment conditions favours women to take opportunities to survive....na kama jobs/biashara ndio ku survive then it make sense kuchukua elimu ili kufanya hizo kazi kwa ufanisi............................................sio vizuri ku dwell into the past,its gone...environment our ancestors had is not the same as ours...

.. kushiriki kwenye kuhudumia familia, utafanyaje bila kuwa na shughuli ya kukupatia kipato? iwe unahudumia fully au kidogo still lazima uwe na kipato,kipato ni kazi ama biashara which both need education kufanya kwa ufanisi..............

..kuhusu kuhudumiwa kila mtu na experiences zake ,kuhudumia kila siku bila kuonyeshwa appreciation hata kwa kidogo then its a problem,ila hii sio sufficient kusema mtoto wa kike asisomeshwe!
 
You are right, watoto wa kike wapate haki ya elimu sawa na wa kiume lakini tunahitaji kuelimisha vizazi vyetu juu ya majukumu ya asili ya kila jinsia ili kuondoa huu mzigo anaobaki nao mwanamke na kuondoa hii mentality ya kumsomesha mtoto wa kike ili aje a replace majukumu ya mwanaume
 
Kuna nipango ya hovyo hovyo kweli inatekelezwa :
Kujenga shule maalumu za wasichana as if currently adui namba moja wa binti ni mvulana. Really! Na akihitimu aje kuishi na hao wavulana (former adui) huku mtaani /kazini.
Leo Ufaransa imekuwa moja ya taifa linaloidhinisha IVF kwa ajili ya LESBIAN COUPLES NA SINGLE MOTHERS. Shtuka ili uelewe.
Wasichana wanaaminishwa kuwa wanaweza kuishi bila ya mwanamume, ali mradi tu and hela, na mwanaume anaona jamii inamwekea masharti kibao, hivyo hakuna haja ya kuoa.
Huyu atakamuliwa manii, yanaandikwa Quick Way, na huyu ananunua anayapeleka kwa Dr. kisha anakuwa mjamzito in a quick (not proper) way.
Note : Bila ya kujenga responsible future fathers and mothers, haya tunayoyaita maendeleo yatakuwa uchafu mtupu.
 
Mimi sioni kama kuna tatizo mana gap bado ni kubwa wanaume wasomi walioelimika ni wengi tofauti na girls
 
Pamoja nimehamisha watoto wangu kutoka hapo kwenye shule yake sababu ya upuuzi wao wa menejimenti ya shule Ila ameandika jambo la msingi sana.
 
Mwandishi japo upo upande wa pili, nikupe hongera kwa kuliona hili , tukiachana na masuala mengine ya kijamii KWA upande wa Elimu naomba fursa zitolewe tu kwa wote na wakikwama wote wabembelezwe Kama upande wa pili wanavyobembelezwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…