Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Ni kweli ulichoandika Mkurugenzi. Tumeiga mambo ya magharibi yanayo mwinua sana mtoto wa kike badala ya kuwachukulia watoto wote sawa. Muda mrefu nimekuwa na shaka jinsi tunavyombagua mtoto wa kiume ( I need to declare my interest). Mimi ni mzazi na tuna mtoto mmoja wa kiume.

Lakin inashangaza kuona mtoto wa kike anaengwa sana kiasi unashindwa kuelewa kama watoto wa kiume ni watoto wanaotakiwa kwenye taifa hili au la! Ni muda umefika sasa, Taifa litilie maanani kuwajenga watoto wote bila ubaguzi, ama sivyo tutakuwa na taifa la ajabu. Mungu aliporuhusu ziwepo jinsia mbili hakufanya kwa bahati mbaya. Jinsia zote ni muhimu na zinategemeana! Mungu alinusuru taifa letu hizi sera za akina Alice Bailey.
Boys need to be taught to be even Bolder mana mabinti sikuhizi hawakamatiki..
 
Jumuiya na asasi za kijamii pamoja na mm mwenyewe tusipokuwa makini tutaanza kampeni ya kumuinua mtoto wa kiume

Kwa miaka hii ya karibun kumeibuka haki sawa za kijinsia na hapo ndpo mtoto wa kike anapopewa kpaumbele Sana kuliko wa kiume

Usasa na wanawake wanaojiita wanaharakat wametufanya tuucheze huu wimbo wao nakumsahau mtoto wa kiume

Ongezeko la mashoga n kubwa Sana mitaani na wanaharakat wanasema n haki yao

Nje ya mada hivi Bibi @hellenkijobisimba kaolewa?
Hellen kijo bisimba alifiwa na mumewe..... ni mjane
 
Ujasiri ni suala zuri..
Shida ni mitazamo ya feminists its smtimes taken to the extremes...

and kijamii kuna binti ananyimwa shule ama fursa siku hizi?.
Wanawake wanatafuta haki zipi?.

Mtoto wa Kiume kweli naye aangaliwe aendelee kujengewa ujasiri na kujiamini zaidi pia
Isiwe mtoto wa kike tu
Unajua nature inam'beba zaid mtoto wa kiume maana yeye yuko na ujasiri tangu akizaliwa na huwa imejengeka hivyo, hili suala la kumuinua mutoto wa kike na kufanya kuwa kama mtoto wa kiume limetafsiriwa vibaya na hao feminists. Lakini kama mzazi mwenyew mtoto wa kike ni lazima umjenge mwanao wa kike kuwa na ujasiri lakini kutambua mipaka yake ni hipi ..maana yuko kwenye ulimwengu ambayo unam'beba zaidi yeye kuliko uyo wa kiume. Kuweza kubadili hili suala ni gumu sana. Maana ni mipango ya muda mirefu hivyo ni jukumu la kila mwenyew mtoto kama ni Me au Ke kuwajenga katika hali ya kuweza kuamini misimamo yao wenyewe.
 
Unajua nature inam'beba zaid mtoto wa kiume maana yeye yuko na ujasiri tangu akizaliwa na huwa imejengeka hivyo, hili suala la kumuinua mutoto wa kike na kufanya kuwa kama mtoto wa kiume limetafsiriwa vibaya na hao feminists. Lakini kama mzazi mwenyew mtoto wa kike ni lazima umjenge mwanao wa kike kuwa na ujasiri lakini kutambua mipaka yake ni hipi ..maana yuko kwenye ulimwengu ambayo unam'beba zaidi yeye kuliko uyo wa kiume. Kuweza kubadili hili suala ni gumu sana. Maana ni mipango ya muda mirefu hivyo ni jukumu la kila mwenyew mtoto kama ni Me au Ke kuwajenga katika hali ya kuweza kuamini misimamo yao wenyewe.
Ni kweli
Na ndio hapo ili kuzuia madhara ni vyema wavulana nao wasiachwe nyuma..ili kubalance hio effect..mana kwa sasa mtoto wa kike hanyanyaswi..

kuna kizazi kinatengenezwa hapa mabinti kitakua kero; hawa wa leo cha mtoto

mzazi utamjenga ila anayokutana nayo huko duniani?.
Lazima kuwe na jitihada za makusudi ili wanawake nao pia wabalance

'jambo lolote hata liwe zuri kiasi gani kama halina kiasi ni dhara kubwa'
 
Wewe kwa mfano utakubali mwanao wa kike aongozwe na mwanaume badala ya kujiongoza mwenyewe? Hapa naongelea kwa mtizamo wa kujenga mtoto wa kike ujasiri na kujiamini.
Ukiielewa mada vizuri utaelewa kinachozungumzwa, hapa tunazungumzia upotoshwaji unaofanywa na hawa wanaharakati, kumjengea mtoto ujasiri na uwezo ni jukumu la jamii nzima bila kujali wa kike au wa kiume, jamii kwa sasa imeweka focus kubwa kwa mtoto wa kike na huyu wa kiume amesahaulika, vipaumbele vingi kuanzia kwenye elimu mpaka ajira vimewekwa kwa mtoto wa kike matokeo yake watoto wa kiume wamebaki nyuma, kiini cha hii mada ni kuhakikisha watoto wote wanapata fursa sawa bila kujali jinsia
 
Wait..... Kuna siku ya mtoto wa kiume siku hizi au nimesoma vibaya?!
 
Unajua nature inam'beba zaid mtoto wa kiume maana yeye yuko na ujasiri tangu akizaliwa na huwa imejengeka hivyo, hili suala la kumuinua mutoto wa kike na kufanya kuwa kama mtoto wa kiume limetafsiriwa vibaya na hao feminists. Lakini kama mzazi mwenyew mtoto wa kike ni lazima umjenge mwanao wa kike kuwa na ujasiri lakini kutambua mipaka yake ni hipi ..maana yuko kwenye ulimwengu ambayo unam'beba zaidi yeye kuliko uyo wa kiume. Kuweza kubadili hili suala ni gumu sana. Maana ni mipango ya muda mirefu hivyo ni jukumu la kila mwenyew mtoto kama ni Me au Ke kuwajenga katika hali ya kuweza kuamini misimamo yao wenyewe.
Umeshasema nature! Binadamu hatupaswi kuingilia mifumo ya asili!
Wanawake walipaswa kupewa tu upendo na huruma vya kutosha. Vingine vinavyoendelea n kumuinua shetani!
 
Wait..... Kuna siku ya mtoto wa kiume siku hizi au nimesoma vibaya?!
Yes siku ya mtoto wa kiume ipo, ila sijajua ni kwa nini haipewi kipaumbele tena haijulikani kabisa, ili kuwasaidia vijana wetu inabidi tuanze kuipa kipaumbele siku ya mtoto wa kiume
 
Kwa nyakati zijazo zitakua nyakati ngumu sana kwa watoto wa kiume, pengine hawatapata elimu bora, hawatauzika kwenye soko la ajira na pengine watakua hawana confidence mbele ya wanawake since they have been neglected
Sasa watakachofanya baada ya hili ni kitu Cha hatari
 
Ni kweli, mimi naona hili jambo la kuwainua watoto wa kike litakuja kuwapa shida haohao watoto wa kike kwa sababu watakosa waume bora wa kuwao, taifa litakosa respobsible men in future na kutakua na gap kubwa sana kati ya wanaume na wanawake maana hawa wa kiume watakua wamesahaulika

Watakosa ujasiri mbele ta watoto wa kike, kwa namna hiyo tutakua na kizazi ambacho hakina balance kati ya mwanaume na mwanamke

Mwisho kabisa, mwanaume ni kichwa ndani ya familia, na familia ni component ya taiafa, hii familia ikikosa mwongozo mzuri basi taifa litakua halina mwongozo mzuri pia, tutakua na taifa lenye wananchi wa hovyo kabisa

Ni wakati wa serikali kuingilia kati, kuweka mchakato wa usawa kati ya watoto wa kiume na wa kike
Leo unaongea madini balaa
 
Note: Andiko hili lilitolewa May 16, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kiume Duniani.

Kuanzia mwaka 2018, Dr Jerome wa Trinidad and Tobago alifanikiwa kuitambulisha tarehe 16 May ya kila mwaka kama siku maalum ya kutambua mchango wa mtoto wa kiume katika jamii. Tangu mwaka 2012 UN ilipotambulisha tarehe 10 October ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa kike Duniani, swali liliibuka kwa nini tunatenga watoto? Kwanini tuna siku ya mtoto wa kike na hatuna siku ya mtoto wa kiume?

Ndugu zangu mtakubaliana na mimi kwamba katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia matabaka makubwa katika makuzi na malezi ya watoto wetu wa kike na wa kiume na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya WATOTO WA KIUME. Jitihada za lazima zisipofanywa na wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kumrudisha mtoto wa kiume katika nafasi yake madhara yanaweza kuwa makubwa sana. Naomba leo tukiwa tunaadhimisha siku ya mtoto wa kiume duniani niwakumbushe madhara machache tu kati ya hayo ili tuweze kujua na kutambua wajibu wetu;

1. Kwa sasa zaidi ya 20% ya watoto wa kiume wanaacha shule kati ya umri wa miaka 15 - 24. Wengi wao wanaenda kuwa madereva boda boda au watumishi kwenye migodi na mashambani. Wengi wa vijana hawa wanaishia kupata vilema vya maisha kama sio kufa kabisa kutokana na ajali nyingi za bodaboda na hivyo kupokonywa haki yao ya kuishi maisha kamilifu.

2. Watoto wetu hawa wa kiume hawakuwahi kushiriki katika mila wala desturi zozote kandamizi dhidi ya wanawake, hivyo hawaelewi kwa nini mtoto wa kike anapendelewa. Wakiendelea kuishi hivi watajenga chuki dhidi ya wanawake, na kwa kuwa bado 70% ya viongozi wataendelea kuwa wanaume, tutarudi tulikotoka kuwa na wanaume wasiothamini uwezo wa wanawake kwa kuwa wao hawakuthaminiwa katika makuzi yao walishuhudia wanawake wakipendelewa na hivyo wataona ni fursa ya kurudisha kisasi.

3. Watoto wetu wa kiume tusipowaandaa kujua namna ya kuishi na hawa watoto wa kike tunaowajenga kwa sasa tutashuhudia ndoa nyingi kuvunjika, watoto wengi kulelewa na single parent, wanaume kutokujua majukumu yao kwenye familia. Mwisho wa siku hawa watoto wa kike tunaowajengwa kwa nguvu zote watakosa support kutoka kwa watoto wetu wa kiume.

4. Kuongezeka kwa ukatili wa kijinsia, watoto wetu wa kiume watakaposhindwa kushindana kwa hoja na watoto wa kike tutashuhudia na tayari tumeshashuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto wetu wa kike kwa kuwa wako empowered na watoto wetu wa kiume hawajui namna ya kuishi nao. Hivyo watoto wa kiume wataendelea kutumia UBABE ili tu uwanaume wao uweze kuonekana.

5. Kuongezeka kwa vitendo vya ujambazi na matumizi ya madawa ya kulevya. Waathirika wakubwa wa madawa ya kulevya ni watoto wetu wa kiume na pia wao ni rahisi mara 20 zaidi ya watoto wa kike kufungwa jela. Mtoto aliyekosa makuzi sahihi ukua akiwa hatari kubwa kwa jamii iliyomzunguka. Tukiendelea kuwatenga watoto wa kiume vitendo vya ujambazi, unyang'anyi, ubakaji, utapeli n.k. vitaongezeka na hivyo kuendelea kumpoteza mtoto wa kiume na kuhatarisha maisha ya jamii inayomzunguka.
ii
6. Kwa sasa kuna nia madhubuti kabisa ya kumwinua mtoto wa kike kielimu na kumpatia fursa mbalimbali za kumkwamua kiuchumi. Fursa hizi watoto wa kiume hawapati na hivyo wengi wakikosa kazi utawakuta VIJIWENI hata ukitoka nyumbani kwako leo angalia njia nzima unayopita utaona makundi ya watoto wa kiume wenye nguvu na hari lakini hawana kazi za kufanya. Hii inasababisha wakose vipato na hivyo kutegemea kuishi kwa kubangaiza au kutegemea watoto wa kike.

Watoto wetu wa kiume wamekuwa wavivu, hawajiongezi, hawajui majukumu yao, wengi wanapenda kulelewa, hawafanyi vizuri kwenye mitihani yao mashuleni n.k. lakini je NANI WA KULAUMIWA?

Leo ni siku nzuri sana tunaposherehekea hii siku ya mtoto wa kiume duniani wanajamii wenzangu tujiulize, nini mchango wetu katika kumpoteza mtoto wa kiume ? Na je nini kifanyike ili tuanze kurekebisha haya makosa?

Naomba nimalize kwa kunukuu msemo wa Frederic Douglas usemao " It is easier to build strong children than to repair broken men ". Watoto wa kiume wana haki sawa na watoto wa kike kupata Elimu bora, Fursa za kujikwamua kiuchumi na Kuendelezwa vipaji vyao.

Imeandikwa na
Ni Frederick Douglass na siyo "Frederic Douglas".

Mkurugenzi ungeandika Kiingereza tuone kama kweli na wewe upo fluent na hii lugha maana mnapenda sana kuchukua pesa nyingi za mitihani ya majaribio kutoka kwa Wazazi wanaotaka watoto wao watoto waanze hiyo shule halafu mnawakataa kwa kisingizio hawakidhi vigezo, na pesa mnabaki nayo. Shameless money grabbers na huyo mumeo pastor feki! Nyie ni majambazi na hamna huruma mnajificha kwenye kivuli cha Ukristo.
 
Ni Frederick Douglass na siyo "Frederic Douglas".

Mkurugenzi ungeandika Kiingereza tuone kama kweli na wewe upo fluent na hii lugha maana mnapenda sana kuchukua pesa nyingi za mitihani ya majaribio kutoka kwa Wazazi wanaotaka watoto wanaotaka watoto waanze hiyo shule halafu mnawakataa kwa kisingizio hawakidhi vigezo, na pesa mnabaki nayo. Shameless money grabbers na huyo mumeo pastor feki! Nyie ni majambazi na hamna huruma mnajificha kwenye kivuli cha Ukristo.
Mkuu mimi sio mkurugenzi bali nimenukuu andiko kutoka kwa Mkurugenzi, nimelileta hapa kama copy and paste ili tuweze kujadili na kujifunza

Asante pia kwa sahihisho
 
Mkuu mimi sio mkurugenzi bali nimenukuu andiko kutoka kwa Mkurugenzi, nimelileta hapa kama copy and paste ili tuweze kujadili na kujifunza

Asante pia kwa sahihisho
Ujumbe umefika lakini kama huyo "Mkurugenzi" anaingia humu na kusoma. Wanawakataa watoto halafu hapohapo anatokea Mwalimu aliyesimamia mitihani ya majaribio anakwambia yupo tayari kuwapa wanao tuition ili wafikie "viwango" vya shule yao na hatimaye wakubaliwe utadhani ni shule moja ya hadhi ya juu sana. Ukweli huyo "Mkurugenzi" hata Kiingereza ni cha kuunga unga, achilia mbali walimu wao choka mbaya
 
Wapiganie wenyewe Kama ambavyo mtoto wa kike amepigania kufikia hapa.
Kibao kimegeuka....wapitie yale yale aliyopitia mtoto wa kike. Wamasai wanaita Karma[emoji3]
80% ya shughuli za haki sawa mwanaume ndie amefanya zifanikiwe.......

Kama ukibisha nitakuuliza swali moja, kama wanawake ndio walipigania then mbona hatukuona resistance ya mwanaume......?!
 
Back
Top Bottom