Madam Abrianna,
Uko sahihi kabisa. Kampeni ya kumwinua mtoto wa kike/ mwanamke na kumshusha mwanaume ni mpango mkubwa na madhara yake ni kuharibu kizazi cha mwanadamu.
Ni mpango unaotekelezwa na wakuu wa giza watumishi wa shetani wanaoitawala dunia.
Isaya alitabiri haya yapata miaka 700 kabla ya ujio wa Kristo.
Isaya 3: 12 Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
Kwa hio sio jambo la bahati mbaya au linalotokea by chance. Wenye jukumu la kutatua tatizo ni wakuu wa dini lakini nao wako busy na sadaka, siasa na umaarufu.
Biblia pia iko wazi kuhusu matokeo matokeo yake. Ndoa zitavurugika, wanawake hawataolewa na wanaume ndio hivyo watakuwa mashoga nk.
Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.