Dhana ya kuoa mtumishi mwenzake ili wasaidiane kimaendeleo imemponza

Dhana ya kuoa mtumishi mwenzake ili wasaidiane kimaendeleo imemponza

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Hamna aliojua mwanzoni kwamba it will end into tears, ila nyie mabinti wa Machame Mungu anaona.

"Kwa sababu wote tulikuwa wa tumishi tulikubaliana mshahara wake ufanya maendeleo ya familia na wa kwangu utusaidia kwa substance ya kila siku, vikoba na mikopo tuliokopa yote kununulia plot ya kujenga nyumba mpaka tukahamia kwa miaka 7 yote ilisimamiwa na mshahara wa Mrs wangu, ndo anaejulikana kwenye vikoba na saccos za kukopesha vifaa vya ujenzi"

Ndoa ni kama gari mbovu inafikia hatua unaichoka kuitengeneza unaamua kuipaki ukilazimisha unaweza kupata hata ajali barabani au kutumia gharama kubwa zaidi.

Mwaka huu ndoa yao imekuwa beyond repairable inabidi watengane na wagawane mali walizochuma wote, ila chakushangaza Ngosha hajapewa chochote kwasababu ushahidi uliopo unaonyesha kwamba ni pesa ya mwanamke ndo iliotumika kufanya maendeleo yote na hati ya nyumba iko kwenye majina ya mwanamke.

Kiufupi ni kwamba huyu mtumishi mwenzangu iko 51 yrs hana nyumba au vitu vya ndani kwasasa, itabidi aanze kutafuta upya kama fresh graduate.

Mimi nimemshauri akubaliane na matokeo aanze new mindset mambo ya mahakama itampotezea muda bure na kumpa psychological torture.
 
Use brain Heriel,

Mkuu hati ya nyumba iko kwenye majina ya huyu mwanamke ilimlazimu baada ya kununua kiwanja aibadili aiweke kwenye majina yake ila apate mkopo mwingine wa kufanya finishing jamaa yangu hakusutuka kabisa, sasa hivi ndio ameanza kuona makosa when its too late
 
Mwanaume unaoa mwanamke ili akusaidie kulea familia?Lazima una udumavu wa akili.Oa mke umpendaye ili muishi kwa mapenzi na amani.Siyo ili aje akusaidie au achangie kujenga nyumba.
Kinacho sababisha hayo yote ni kipato duni cha watumishi kwa mfano unapokea take home 500k unaishi Dar kweli hiyo pesa utaweza kutoboa kimaisha unalazimika kutafuta mwenzako mwenye mshahara kama huo, hamna mwanaume anaependa kusaidiwa na demu ila tu ndo hivyo
 
Kinacho sababisha hayo yote ni kipato duni cha watumishi kwa mfano unapokea take home 500k unaishi Dar kweli hiyo pesa utaweza kutoboa kimaisha unalazimika kutafuta mwenzako mwenye mshahara kama huo, hamna mwanaume anae penda kusaidiwa na demu ila tu ndohivo
Tupo wote. Lakini unapooa ni vema kuangalia mbali zaidi ya "kusaidiwa" na mwanamke. Kwa utamaduni na asili yangu, nikioa ili nisaidiwe ni aibu sana. Sijalibadilisha akili mwangu. Bibie wangu hata kama ana kazi na mshahara, huo ni wake na watoto. Simuulizi chochote. Akiamua atoe. Akikataa ni sawa. That's the benefit of being a man with a gun, fella!
 
Mwambie ngosha the don kidulula sugu atulie tuli.

Akapange singo rum asubiri pension yake. Ikitoka ata 55 kwa hiari aje runzewe atulie.
Ngosha tayari kasha pata single room ila ule mtoto mkubwa mwenye 11yrs inabidi aondoke nae kwasasa iko shule ya bweni ila wakifunga itambidi apate mschana wakazi au aoe tena, otherwise atamshinda kulea.
 
Hivi hatujifunzi tuu, Hizo mali hata jina lako usiandike, tafuta namna, hizi ndoa za dini za kuletwa ndio zimetufikisha hapa, na bado, soon Tutaona umuhimu wa ndoa za mikataba hasa kwa sisi wavuja jasho wa kiume
Mwanaume oa ili mwanamke atimize matakwa yako na sio utimize matakwa yake
Kama ni kazi muachishe afanye kazi yako akiwa kama mwangalizi na sio mmiliki.
 
Hivi hatujifunzi tuu, Hizo mali hata jina lako usiandike, tafuta namna, hizi ndoa za dini za kuletwa ndio zimetufikisha hapa, na bado, soon Tutaona umuhimu wa ndoa za mikataba hasa kwa sisi wavuja jasho wa kiume
Nadhani ndoa ni makubaliano kama mikataba mingine tatizo ni sie wanandoa hatuaminiani wala hatupendane tunaishi kiunafiki tu.
 
Back
Top Bottom