Mimi napingana na wewe!!
Hii mindset yako imejengwa na wanawake wenyewe kwamba wao wamekuja ndani ya ndoa kuzaa tu.
Labda nikuulize, nini kilichokua kina wafanya babu zetu na baadhi ya baba zetu wengi kuoa wake wengi???
Ule ndio ulikua utamaduni wetu kabla dini hazijaja kutubadilishia kanuni ya mke mmoja mume mmoja.
Kwa za a hizi, nakubaliana na wewe kwamba kama umetambua wajibu ya mwanaume ni kutafuta mkate wa kila siku kwa ajili ya familia yako, basi lazma utambue pia wajibu wa mwanamke ni upi katika familia.
Kama mimi ntahusika kuleta chakula ndani, kusomesha watoto, kuwajengea makazi familia yangu, kumvisha mke wangu, kuwavisha watoto wangu, kulipa bili zote za home including ving'amuzi nk nk, basi hata huyu mke inabidi asimame kidete kwenye nafasi yake kama mke, ikiwa ni kunihakikishia tangu nimeamka asubuhi nimeandaliwa vizuri, watoto wapo Safi, tunakula na kunywa kwa wakati, nyumba inakua Safi na hapo hata kiwi awe na msaidizi (house girl) kwasababu yupo full kwenye majukumu yake.
Sasa kwa maisha tuishiyo sasa, wanawake pia wanakwenda makazini. Muda anaotoka kazini huenda unafanana na wako. Huenda pia kazi yake ina majukumu mengi kuliko yako. Sasa kama wewe unafanya majukumu yako ya nyumbani yooote, je huoni kwamba muda wake yeye mwingi unaishi kazini kwake (ambako wewe huna faida nako)
Kwa hiyo mimi naona, kama ameajiliwa, atachangia tu maendeleo ya nyumbani atake asitake, kinyume cha hapo akae nyumbani ili kila mtu afanye wajibu wake kwenye familia.
NB kuoa wake wengi ilikua ni kukusanya nguvu kwa ajili ya kufanya kazi kujenga familia na kuleta heshima ndani.