Dhana ya "kusaidiana" maisha na mwanamke katika utafutaji ni ya wanaume dhaifu na wajinga sana

kama umesomeshwa na familia yako na blah blah whatever kaolewe na familia yako shida iko wapi. Kutwa mmekazana na mapost ya "natafuta mume" jamani what the f.ck si mkaolewe na familia zenu zilizowasomesha ili muwe mafeminist maviburi na madumejike majuaji. Kila mtu ashinde mechi zake ebo
 
Utakuta jitu halijawahi kuwa kwenye ndoa linakupa wosia mrefu kuhusu ndoa😂😂.
jf ni kama kijiwe cha kahawa, mtu hana influence yoyote yupo tu kashiba kande anakuja kushauri mambo ya ndoa.
Huu mtabdao huwa unafurahisha sana
 
Anawanyoosha kwa faida ya vijana wengine
viijana gani?
Halafu vijana wanaofanya kazi hawashindi Jf wapo kariakoo huko wanapambana na kubeba mizigo sokoni.
Humu wengi hawana kazi, sasa unafikiri vp hata kuoa hata kujilisha kwako ni shida? Huoni vijana wnye nyege wanatongoza watu ambao hawajawahi hata kuwaona? Hiki ni kijiwe cha wahuni vijana waliopo humu ni 1%
 
Nikisoma sifa ze mke mwema kwenye METHALI 31

Sijaona mahali Mungu anasema mke akae nyumbani kama kubwa jinga anamsubiri tu mumewe.

METHALI 31:16
16. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

METHALI 31:24
24. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
 
Utakuta jitu halijawahi kuwa kwenye ndoa linakupa wosia mrefu kuhusu ndoa😂😂.
jf ni kama kijiwe cha kahawa, mtu hana influence yoyote yupo tu kashiba kande anakuja kushauri mambo ya ndoa.
Huu mtabdao huwa unafurahisha sana
haya sawa sina influence
 
Ngoj nianze mazoez ya kukaa tu nyumbani ili nije kudumu kwenye ndoa 😌
 
Ahsante sana mkuu.🙏🏻
Mungu akubariki
Akuongeze
Atunze familia yako
Akuweke juu juu juu siku zote

Nb ili mtu aelewe umeandika nini ni hadi awe mwanaume.
 
Ungemalizia kwa kutoa "recommendations" za nini kifanyike ungekua umetisha sana.
 
Hivi ndugu mleta uzi umewahi kufikiria siku ukawa kitandani mgonjwa huwezi kutoka kwenda kwenye shughuli zako za kila siku, biashara yako imefirisika au umepoteza kazi?

Kama huyo mkeo unayemsifia cha uvivu kakaa tu nyumbani anakusubiri uumletee ataweza kuvumilia na kusaidia kama hajishughulishi?

MWANZO 2:18
Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mwanaume awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa."

Hatukatai jukumu ka kuitunza familia ni la mume ila Mungu anataka mke awe msaidizi wake
 
Wanaume wasiojiamini, wasioenda shule na wasio elimika ndio huogopa Wake zao kufanya kazi.

Kwenye Dini, hakuna mke wa Nabii mkubwa yeyote ambaye alikuwa hafanyi kazi.

Muhammad mwenyewe mkeww mkubwa Bi. Khadija alikuwa mfanyabiashara na anapesa kuliko Muhamad mwenyewe.

Yesu alikuwa anahudumiwa na wanawake wafanyabishara akiwemo Mariam Magdalena.

Sifa mojawapo kuu ya mke mwema ni kufanya kazi. Kasome mithali 31.

Vigezo vya kuoa mke katika uislamu ni vitatu
1. Dini(Iman yake kwa Mungu)
2. Uzuri wake.
3. Mali zake.

Wanawake wote waliolelewa vyema na wanaojitambua ambao kimsingi ndio Wake Wema hawawezi kuolewa na mwanaume mjinga na Mpumbavu ambaye hataki wao wafanye kazi.

Ndio maana binti zetu tunawapeleka shule wakasome na kuelimika ili wasije kujikuta wanakutana na wanaume wapumbavu wasiojitambua na wasiojiamini.
Wapo wanawake wanawaza kuwa Marais, majaji, mawaziri, wakurugenzi alafu kuna mwanaume mmoja mjinga kwa umaskini wake wa fikra anawaza mawazo ya kizamani na kitoto ati Mwanamke asiwe na mchango ndani ya familia na jamii.

Kuhusu Usingle Mother,
Mwanamke yeyote aliyetoka familia kubwa yenu hadhi, na Mwanamke aliyesoma na kujitambua au hata ambaye hajasoma lakini anajitambua hawezi kuendana na kuishi na mwanaume Mpumbavu mwenye akili kama mada hii ilivyowasilishwa.

Kila mtu(Mwanamke na mwanaume) anayohaki ya kujitegemea ili awe Huru.

Wanaume waoga ndio pekee wanaogopa wanawake wenye vipato, wenye elimu, na wenye kujua haki zao
 
Tatizo ni kuchukua mwanamke mwenye malengo makubwa pengine kukuzidi. Una kipato cha kawaida, umeajiriwa na laki saba yako kwa mwezi, unaenda kuoa mwanamke ana degree sijui masters na ana malengo makubwa maishani, lazima msaidiane. Ila kama ukitaka comfort, chukua binti ambaye kuachiwa elf 10 mezani ya kupika kwake ni jambo kubwa mno na karidhika na hayo maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…