Chaguzi mbali mbali huwa ni kipimo cha uongozi katika jamii. Chaguzi za vyama vya siasa huwa ni kipimo cha uongozi kwa viongozi wanaomaliza muda wao au kwa wagombea wanaotegemewa kuleta maendeleo katika njia ya mabadiliko au mwendelezo wa misingi ya kile kilichokuwa kinafanywa na uongozi unaomaliza muda wake.
CHADEMA mpaka sasa imeaihirisha chaguzi zake za viongozi wakuu zaidi ya mara moja kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi!. Kwa sasa chaguzi tumeambiwa zitafanyika kuanzia tarehe 16/09/2014.
Nimeguswa na utayali, uwezo, uadilifu na kikubwa zaidi, sababu kuu za mgombea Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa-Bara, Prof Abdallah Safari.
Prof. Safari ameainisha mambo makuu matano anayoenda kupambana nayo kama atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa-Bara.
1) Ukanda
2) Udini.
3) Ubaguzi wa rangi na jinsia.
4) Kuondoa umasikini, ujinga na Maradhi.
5) Ubadhirifu
Usipoyachunguza maneno/sababu anazozitaja unaweza kusema ni maneno/sababu za kawaida kabisa, lakini ukichunguza katika mantiki ya hoja pana utapata maswali fikirishi ambayo ndiyo yatakuwa akisi la CHADEMA kama chama cha kisiasa nchini hasa ikichukuliwa kuwa, Prof. Safari mpaka sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Ieleweke kuwa, unaposema unaenda kupambana na jambo fulani ina maana umeliona lipo ndiyo maana ukatafuta silaha za kwenda kupambana nalo. Kama una akili timamu huwezi kwenda kupambana na adui ambaye hayupo!
Prof. Safari anaposema ameombwa kugombea ili kupambana na dhana/matatizo ya ukanda na udini ndani ya CHADEMA, kwa lugha nyingine anatuambia kuwa ndani ya CHADEMA kuna ukanda na udini!. Kama hakuna, kuna umuhimu gani wa kumchagua kiongozi anayetaka kupambana na matatizo ambayo hayapo!.
Kubwa zaidi, kiongozi makini katika chama au taifa lisilo na dini au ukanda hawezi kuchaguliwa kwa msingi wa dini au ukanda. Prof. Safari anapotaka achaguliwe kwa misingi ya dini au ukanda ina maana anaingia kwenye ulingo wa kisiasa ndani ya chama ambacho mchezo wake ni udini na ukanda. Hii inanipeleka kwenye msingi wa hoja yangu inayouliza, ni kweli ndani ya CHADEMA kuna udini na Ukanda
Kama udini na ukanda upo ndani ya CHADEMA, ataweza kuuondoa kama akichaguliwa hasa ikichukuliwa kuwa, mpaka sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama.
Kwa mantiki hii, anataka kutueleza kuwa Mzee Said Arfi alishindwa kuuondoa au hakuuona baada ya kuwepo kwenye nafasi hiyo.
[video=youtube_share;dqrIQV6x8eU]http://youtu.be/dqrIQV6x8eU[/video]
Unaweza kutokubaliana na Mwl. Nyerere lakini huwezi kukataa mantiki ya hoja yake aliposema, chama au nchi endelevu haiwezi kumchagua mtu kwa msingi wa dini yake, au sehemu anayotoka nchini. Chama au nchi inayofanya hivyo inakuwa imefirisika kifikra na kimtazamo.
Ni kweli CHADEMA imefirisika kifikra na kimtazamo? If CHADEMA is about fair and equal opportunities for all, why Prof. Safari is playing religion and zone card?
[video=youtube_share;pKscF5wA5jM]http://youtu.be/pKscF5wA5jM[/video]
Tutasikia na kuona mengi kabla ya uchaguzi wa viongozi wakuu ndani ya CHADEMA!.