Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Kwa hiyo unataka kusema udin , na ukabila wa chadema sio kweli ni propaganda za CCM . Hata mapungufu yenu wenyewe mnasingizia ccm . Ccm inahusikaje kwenye ubaguzi wenu wa waziwazi?
Ndugu,
Hata mimi pia huwa ninawashangaa sana baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA. Kila matatizo ndani ya CHADEMA wanadai yanasababishwa na CCM.

Mimi nadhani hizi ni hoja za kuukimbia ukweli wanaoufahamu vizuri. Madai kama hayo yanapaswa kusemwa na wakosefu wa fikra pana au walevi wa fikra pana, otherwise, wanataka tuamini kuwa wao pia ni walevi wa fikra pana au wakosefu wa fikra pana.
 
Chaguzi mbali mbali huwa ni kipimo cha uongozi katika jamii. Chaguzi za vyama vya siasa huwa ni kipimo cha uongozi kwa viongozi wanaomaliza muda wao au kwa wagombea wanaotegemewa kuleta maendeleo katika njia ya mabadiliko au mwendelezo wa misingi ya kile kilichokuwa kinafanywa na uongozi unaomaliza muda wake.

CHADEMA mpaka sasa imeaihirisha chaguzi zake za viongozi wakuu zaidi ya mara moja kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi!. Kwa sasa chaguzi tumeambiwa zitafanyika kuanzia tarehe 16/09/2014.

Nimeguswa na utayali, uwezo, uadilifu na kikubwa zaidi, sababu kuu za mgombea Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa-Bara, Prof Abdallah Safari.

Prof. Safari ameainisha mambo makuu matano anayoenda kupambana nayo kama atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa-Bara.
1) Ukanda
2) Udini.
3) Ubaguzi wa rangi na jinsia.
4) Kuondoa umasikini, ujinga na Maradhi.
5) Ubadhirifu
Usipoyachunguza maneno/sababu anazozitaja unaweza kusema ni maneno/sababu za kawaida kabisa, lakini ukichunguza katika mantiki ya hoja pana utapata maswali fikirishi ambayo ndiyo yatakuwa akisi la CHADEMA kama chama cha kisiasa nchini hasa ikichukuliwa kuwa, Prof. Safari mpaka sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Ieleweke kuwa, unaposema unaenda kupambana na jambo fulani ina maana umeliona lipo ndiyo maana ukatafuta silaha za kwenda kupambana nalo. Kama una akili timamu huwezi kwenda kupambana na adui ambaye hayupo!

Prof. Safari anaposema ameombwa kugombea ili kupambana na dhana/matatizo ya ukanda na udini ndani ya CHADEMA, kwa lugha nyingine anatuambia kuwa ndani ya CHADEMA kuna ukanda na udini!. Kama hakuna, kuna umuhimu gani wa kumchagua kiongozi anayetaka kupambana na matatizo ambayo hayapo!.

Kubwa zaidi, kiongozi makini katika chama au taifa lisilo na dini au ukanda hawezi kuchaguliwa kwa msingi wa dini au ukanda. Prof. Safari anapotaka achaguliwe kwa misingi ya dini au ukanda ina maana anaingia kwenye ulingo wa kisiasa ndani ya chama ambacho mchezo wake ni udini na ukanda. Hii inanipeleka kwenye msingi wa hoja yangu inayouliza, ni kweli ndani ya CHADEMA kuna udini na Ukanda

Kama udini na ukanda upo ndani ya CHADEMA, ataweza kuuondoa kama akichaguliwa hasa ikichukuliwa kuwa, mpaka sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama.

Kwa mantiki hii, anataka kutueleza kuwa Mzee Said Arfi alishindwa kuuondoa au hakuuona baada ya kuwepo kwenye nafasi hiyo.


[video=youtube_share;dqrIQV6x8eU]http://youtu.be/dqrIQV6x8eU[/video]

Unaweza kutokubaliana na Mwl. Nyerere lakini huwezi kukataa mantiki ya hoja yake aliposema, chama au nchi endelevu haiwezi kumchagua mtu kwa msingi wa dini yake, au sehemu anayotoka nchini. Chama au nchi inayofanya hivyo inakuwa imefirisika kifikra na kimtazamo.

Ni kweli CHADEMA imefirisika kifikra na kimtazamo? If CHADEMA is about fair and equal opportunities for all, why Prof. Safari is playing religion and zone card?


[video=youtube_share;pKscF5wA5jM]http://youtu.be/pKscF5wA5jM[/video]

Tutasikia na kuona mengi kabla ya uchaguzi wa viongozi wakuu ndani ya CHADEMA!.
Unauliza vumbi store, uchaguzi wa baraza la wazee wa Chadema kashinda Ntagazwa lakini ushindi kapewa mpemba unadhani kwa sababu gani.
 
Wafuasi wa Boko haram, Alshababu na Aqaeda ni nduguzako?
Nimesema binadamu wote ni ndugu zangu. Hayo mengine yako chini ya uwezo na mtazamo wako katika kudadavua maana yake.

Kama unaamini vitabu vya dini za Kikristo au Kiislamu utakuwa unafahamu kuwa Mungu aliwaumba binadamu wote na matendo ya hao binadamu hayawezi kumfanya Mungu awakane kama ni wanae(Binadamu aliowaumba).
 

Prof. Safari ameainisha mambo makuu matano anayoenda kupambana nayo kama atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa-Bara.
1) Ukanda
2) Udini.
3) Ubaguzi wa rangi na jinsia.
4) Kuondoa umasikini, ujinga na Maradhi.
5) Ubadhirifua,

uu ndani ya CHADEMA!.

Umeanza vema, kwamba Safari ameanza safari na kachagua aina ya vipaumbele vyake ambavyo umenukuu. Mlolongo wote wa maelezo mengine ni mawazo yako binafsi. Ungekuwau umemtendea haki Safari kama ungemdodosa undani wa vipaumbele vyake badala ya kusema "ukiangalia kwa mapana. ........." unamsemea yasiyo yake
 
Nimesema binadamu wote ni ndugu zangu. Hayo mengine yako chini ya uwezo na mtazamo wako katika kudadavua maana yake.

Kama unaamini vitabu vya dini za Kikristo au Kiislamu utakuwa unafahamu kuwa Mungu aliwaumba binadamu wote na matendo ya hao binadamu hayawezi kumfanya Mungu awakane kama ni wanae(Binadamu aliowaumba yeye).

Siku zote kwa nini waislam wawe wasaidiz tu wa mbowe. prof.safari atabwaga manyanga kama arfi
 
Ndiyo, Interahamwe ni ndugu zangu kama binadamu kwa sababu mwanadamu hamchagulii Mungu mapenzi yake na utendaji wake hasa ikichukuliwa kuwa binadamu wote ni sawa.

Nilitaka nikueleze ili uelewe kuwa upuuzi wako hauna nafasi katika mantiki za hoja.

Sasa una apo address salama ya ndugu zangu,huna budi ku specify kuwa hao nduguzo ni Intarahamwe na majini
 
Ukitaka kujua kama Chadema Waislam hawatakiwi muulize Said Arfi na Zitto Kabwe leo hii wapo wapi.
 
Nimesema binadamu wote ni ndugu zangu. Hayo mengine yako chini ya uwezo na mtazamo wako katika kudadavua maana yake.

Kama unaamini vitabu vya dini za Kikristo au Kiislamu utakuwa unafahamu kuwa Mungu aliwaumba binadamu wote na matendo ya hao binadamu hayawezi kumfanya Mungu awakane kama ni wanae(Binadamu aliowaumba yeye).
Assalamu Alaikhum Ndugu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu adhimu.

Ama mimi sina budi ila kumshukuru Allah alietuumba na kutupa elimu yakuweza kujua nini kibaya na nini kizuri. Katika habari za Siri ambazo tumezipata kutoka ndania ya CCM ni Kwamba Mh Othman Masoud ameekewa Kikao cha Siri ili Kufukuzwa kazi baada yakutoka katika Bunge hilo kama Muandishi wa Katiba Mpya ya CCM ambayo ina lengo lakuendelea na Serikali 2 kueleka 1.

Nasikia katika kikao hicho Muazizi Sefu Ali Iddi alikatishwa ziara yake ya campeni dhidi ya CUF na Ukawa katika Mikoa na Vijiji vya Tanganyika. Msiri wetu alitwambia katika Mkutano huo ulihudhuriwa na Vigogo 4 wa CCM kutoka Tanganyika na 2 kutoka Zanzibar. Nasikia ushauri wa vigogo wawili kutoka Zanzibar walitaka Mh. Sefu Ali Iddi amshinikize Raisi Kumuhamisha Ofisi Othman Masoud, badala ya kumfukuza kazi.

Wanaona kufanya hivo kutaisaidia CCM kuficha uovu wake juu ya wale wote wanao tetea haki na maslahi ya Zanzibar . Na nafasi ya Othman imependekezwa apewe Mkusa Isaac Sepetu ili awe mwanasheria mkuu wa Zanzibar atakae andika Katiba mpya ya Muungano.. Lakini nasikia Makamo wa pili wa SMZ amesema atakua ameisaliti CCM na Serikali ya SMZ kushiriki mchakato huo na mwisho kuisaliti SMZ.

Nasikia CCM wengine ( Vigogo) walikua wana wasiwasi na Othman tokea zamani, hasa kwavile na yeye alikuwemo katika kutoa Elimu ya juu ya Rasimu ya Tume na nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano.. Nasikia hata Jaji Warioba alikua anajuiluza kwanini baadhi ya Wazanzibari ambao walikua mbele kuchambua matatizo ya Muungano na kutaka Mamlaka kamili ya Nchi zilizounda Muungano sasa wamo ndani ya Bunge hili kuifumua Rasimu..

Habari kutoka kwa CCM wanasema kwamba hata katika hizo kamati 12 ambazo zimepeleka maoni ya Rasimu zilizochambuliwa sio zote kwamba zilipata Theluti 2 za pande zote ktk kamati kama inavodaiwa na Wajumbe waliowakilisha reporti.. Wanasema kwamba Walikua wakiwaona Watanganyika wengi wakutoka kundi la 201 ambao ni CCM kuingia na kupiga kura.. Lakini hii ni Siri..

Baadhi ya CCM kutoka Zanzibar wanaunga mkono Othman Masoud kujitoa nafasi hiyo kama utakua ushahidi wa wazanzibari kutoshirikishwa Kisiasa katika Uandishi huu wa Katiba ya Tanganyika.. Wanasema wapo wanafuata Kundi na kupata posho ya bure ., lakini hawana imani na rasimu ya CCM isipokua Wanalazimishwa tu.
Kila Mzanzibari alie CCM ambae ni kiongozi anaeonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM mwisho wake huwa mbaya na huvuliwa nyadhifa zote za uongozi na kutupwa kama mzoga na huonekana si lolote si chochote katika jamii ya wanaCCM. Na hili zaidi hutendewa WaZanzibari tu ,angalia Akina Seif na wenziwe wakati wa Nyerere walitimuliwa ,ni juzi tu Mansor Yousef nae katimulia ,hata haukujatulia Yule Mwanasheria Mkuu nae anaundiwa zengwe afukuzwe habari zipo huku Othman Masoud kufukuzwa nafasi ya MMWZ na Kupewa Mkusa Sepetu..Bado iko siri - Mzalendo.net

Mbona huku Tanganyika hakuna afukuzwae kuna mambo kibao ,hatusikii Mtanganyika kufukuzwa lile la Mwigulu kama angelisema Mzanzibar ndani ya bunge la Katiba bai ingelikuwa ameshapata la kumpata ,mbali ya viongozi wakuu waliohusishwa na mambo mbalimbali ikiwemo rushwa na mikataba mibovu kama wangekuwa wazenji wangelikwisha fukuzwa chamani na kutolewa ndani ya serikali .ila tunawaona akina Lowasa wavijisenti. wanapeta ndani ya CCM mbali waliojitangaza kugombea uraisi ndani ya CCM ,kama wangelikuwa wazenji basi wangekwishatimuliwa.
309768_233135676822252_1487420977_n.jpg


Wakati serikali ikiendelea kupiga vita waganga wa kienyeji matapeli hali imekuwa tofauti huko Geita ambapo diwani wa CCM Mawazo Wiliam wa kata ya ya Bugarama Wilayani Geita amekamatwa akiwa na matunguri anayoyatumia nyumbani kwake kupiga ramli chonganishi na kuosha wakataji wa mapanga .

Wakiongea kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi wa kata hiyo kwa sharti la kutotaka kutajwa majina yao walisema diwani huyo amekuwa ni kero kwa watu kwani amekuwa akiwatapeli watu kwa kuwapatia tiba za uongo na kuwachonganisha watu bila kuona kuwa yeye ni kiongozi.

Walisema diwani huyo amekuwa akiwapigia ramli chonganishi watu wanaokwenda kwake kwa ajili ya kupata tiba ya kienyeji hivyo kuwaomba wanaohusika kuchukua hatua dhidi ya diwani huyo.

"Jamani huyu diwani wa CCM ni tapeli anawachonganisha wananchi mpaka wanafika hatua ya kuuana ,kwanza si mganga bali ni tapeli ni mganga gani ufike unaambiwa kiasi kikubwa cha fedha ",walisema.

Afisa mtendaji wa kata hiyo Juma Choba alikiri kukamatwa kwa diwani wake lakini akasema kuwa alikamatwa kwa tuhuma za kuwaosha wakataji wa mapanga katika kata hiyo.

Hata hivyo alisema hajui kama ni kweli anafanya kazi hiyo kwani hajawahi kuona ila anasikia kutoka kwa wananchi kuwa diwani wake anawapigia ramli chonganishi.

"Mimi nasikia kama wewe unavyosikia lakini sijawai kumuona ila amekamatwa yuko Polisi Wilayani inawezekana ni kweli kwa kweli siwezi kukataa",alisema Mtendaji huyo.

Akizungumza na malunde1 blog iliyotaka kujua zaidi kuhusu tuhuma hizo za kukamatwa kwake na kupiga ramli chonganishi , diwani Mawazo alisema kuwa yeye hana lolote la kujibu juu ya hilo.

Jeshi la polisi Mkoani Geita limethibitisha kukamatwa kwa diwani Mawazo na uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.


MwanaDiwani, hayo yanajadilika?
 
Ukitaka kujua kama Chadema Waislam hawatakiwi muulize Said Arfi na Zitto Kabwe leo hii wapo wapi.

Unafiq na Usaliti wao ndio umewaponza,bila kuwasahahu Mwigamba na Kitilla
 
Na mimi narudia huna akili kwa maana kile unachoongea hakilinganishwi na mtu mwenye akili timamu. Halafu cha ajabu unataka kuigawa Chadema ili wasimchague Prof. Safari ili baadae uje na hiyo akili ya kipuuzi kuwa hakuchaguliwa kwa sababu ya udini na ukanda. Yeye anachosema hapa anakwenda kupambana na watu wanaosema Chadema kuna udini na ukanda ili waproove wrong sasa wewe unakuja na akili ya kijinga kuwa kasema ndani kuna udini na ukanda
Ondoa upuuzi wako, wewe ni wa kuuza kama wapuuzi wengine[
QUOTE=MwanaDiwani;10535597]Ndugu,
Neno huna akili ni relative term. Wewe unaweza ukadhani sina akili lakini kuna mwingine atadhani tofauti na mtizamo wako.

Wajumbe watakaomchagua Prof. Safari watakuwa na informed decision na siyo kama bendera fuata upepo!

Kama huwezi hata kusoma na kuelewa maandiko, basi unaweza kuangalia video ya mahojiano.[/QUOTE]
 
Unauliza vumbi store, uchaguzi wa baraza la wazee wa Chadema kashinda Ntagazwa lakini ushindi kapewa mpemba unadhani kwa sababu gani.
Ndugu Ritz,
Kwa hiyo una maanisha CHADEMA wanachofanya ni sawa na kupaka rangi ya nyumba kwa nje inayovutia wapita njia lakini kwa ndani kuna uchafu mwingi!
 
Ndugu,
Hii akili ya watu wa CCM ndiyo iliyokufanya kutoa comment!.

Suala la kumuua Nyerere ni suala ambalo liko chini ya utaratibu wa makosa ya jinai, otherwise unaweza kuwa kuwasaidia polisi kuhusiana na ushahidi wako.

Suala la mimi kupotea wala lisikusumbue kwa sababu liko juu ya uwezo wako!

Jikite kwenye mada iliyoko mezani.

Ni kweli liko juu ya uwezo wangu ndiyo maana unajigamba now coz mlishammaliza. Get it on coward, mnachokitafuta mtakipata
 
Ndugu,
Neno huna akili ni relative term. Wewe unaweza ukadhani sina akili lakini kuna mwingine atadhani tofauti na mtizamo wako.

Wajumbe watakaomchagua Prof. Safari watakuwa na informed decision na siyo kama bendera fuata upepo!

Kama huwezi hata kusoma na kuelewa maandiko, basi unaweza kuangalia video ya mahojiano.

hivi KUMBE , WE JAMAA UWEZO WAKO NDIO HUU ?
 
Licha ya kwamba Profesa Safari ametaja sababu za kugombea Umakamu Mwenyekiti, nadhani huyu msomi hakutafakari kwa umakini na kwa kina, eti anataka kukomesha Ukanda, Udini, Ubaguzi wa rangi au Ukabila na Kijinsia, Umaskini na Ujinga pamoja na Ubadhirifu.

Kwanza kuhusu Ukanda, CHADEMA kilianzishwa na Mtei wa Kanda ya Kaskazini, lakini kwa juhudi kubwa za huyu Muasisi, akisaidiwa na waliomrithi na wanachama wengine, kimeenea nchi nzima: Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Mtwara, Lindi na mikoa yote ya Pwani, Kati na Kaskazini kwao Mtei.

Kuhusu Udini, yeye mwenyewe Muislamu, na mgombea uenyekiti taifa ni Mkristo. Anataka nini cha zaidi ya
kushirikisha dini zote? Labda CHADEMA washirikishe wasio na dini (atheists) zaidi?

Ukabila na Rangi haviko Chadema. Hata sijui kabila la Prof. Safari, na nikiwa mpiga kura katika jimbo lake, namhakikishia kura yangu. Ubaguzi wa kijinsia hauko kabisa CHADEMA. Uliza wakina mama wa Chama.

Umaskini, Ujinga na Maradhi vinatushinda sisibsote, kutokana na ufinyu wa fedha na zana za kukabiliana navyo. Hilo ni tatizo la kitaifa kwa chama chochote cha siasa, hata CCM chama tawala, licha ya kwamba Ubadhirifu na Rushwa vikitokomezwa tutamudu zaidi majukumu hayo.

Kwa hiyo kwa jumla, Profesa ni vema ujue matatizo na kiini chake. Nina hakika uongozi wa sasa wa CHADEMA utanufaika, endapo juhudi zako za kujiunga nao kama Makamu Mwenyekiti, zitafanikiwa. Kila la kheri.

 
Back
Top Bottom