Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Kwa hiyo unataka kusema udin , na ukabila wa chadema sio kweli ni propaganda za CCM . Hata mapungufu yenu wenyewe mnasingizia ccm . Ccm inahusikaje kwenye ubaguzi wenu wa waziwazi?
Ndugu,
Hata mimi pia huwa ninawashangaa sana baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA. Kila matatizo ndani ya CHADEMA wanadai yanasababishwa na CCM.

Mimi nadhani hizi ni hoja za kuukimbia ukweli wanaoufahamu vizuri. Madai kama hayo yanapaswa kusemwa na wakosefu wa fikra pana au walevi wa fikra pana, otherwise, wanataka tuamini kuwa wao pia ni walevi wa fikra pana au wakosefu wa fikra pana.
 
Unauliza vumbi store, uchaguzi wa baraza la wazee wa Chadema kashinda Ntagazwa lakini ushindi kapewa mpemba unadhani kwa sababu gani.
 
Wafuasi wa Boko haram, Alshababu na Aqaeda ni nduguzako?
Nimesema binadamu wote ni ndugu zangu. Hayo mengine yako chini ya uwezo na mtazamo wako katika kudadavua maana yake.

Kama unaamini vitabu vya dini za Kikristo au Kiislamu utakuwa unafahamu kuwa Mungu aliwaumba binadamu wote na matendo ya hao binadamu hayawezi kumfanya Mungu awakane kama ni wanae(Binadamu aliowaumba).
 

Umeanza vema, kwamba Safari ameanza safari na kachagua aina ya vipaumbele vyake ambavyo umenukuu. Mlolongo wote wa maelezo mengine ni mawazo yako binafsi. Ungekuwau umemtendea haki Safari kama ungemdodosa undani wa vipaumbele vyake badala ya kusema "ukiangalia kwa mapana. ........." unamsemea yasiyo yake
 

Siku zote kwa nini waislam wawe wasaidiz tu wa mbowe. prof.safari atabwaga manyanga kama arfi
 
Ndiyo, Interahamwe ni ndugu zangu kama binadamu kwa sababu mwanadamu hamchagulii Mungu mapenzi yake na utendaji wake hasa ikichukuliwa kuwa binadamu wote ni sawa.

Nilitaka nikueleze ili uelewe kuwa upuuzi wako hauna nafasi katika mantiki za hoja.

Sasa una apo address salama ya ndugu zangu,huna budi ku specify kuwa hao nduguzo ni Intarahamwe na majini
 
Ukitaka kujua kama Chadema Waislam hawatakiwi muulize Said Arfi na Zitto Kabwe leo hii wapo wapi.
 


MwanaDiwani, hayo yanajadilika?
 
Ukitaka kujua kama Chadema Waislam hawatakiwi muulize Said Arfi na Zitto Kabwe leo hii wapo wapi.

Unafiq na Usaliti wao ndio umewaponza,bila kuwasahahu Mwigamba na Kitilla
 
Na mimi narudia huna akili kwa maana kile unachoongea hakilinganishwi na mtu mwenye akili timamu. Halafu cha ajabu unataka kuigawa Chadema ili wasimchague Prof. Safari ili baadae uje na hiyo akili ya kipuuzi kuwa hakuchaguliwa kwa sababu ya udini na ukanda. Yeye anachosema hapa anakwenda kupambana na watu wanaosema Chadema kuna udini na ukanda ili waproove wrong sasa wewe unakuja na akili ya kijinga kuwa kasema ndani kuna udini na ukanda
Ondoa upuuzi wako, wewe ni wa kuuza kama wapuuzi wengine[
QUOTE=MwanaDiwani;10535597]Ndugu,
Neno huna akili ni relative term. Wewe unaweza ukadhani sina akili lakini kuna mwingine atadhani tofauti na mtizamo wako.

Wajumbe watakaomchagua Prof. Safari watakuwa na informed decision na siyo kama bendera fuata upepo!

Kama huwezi hata kusoma na kuelewa maandiko, basi unaweza kuangalia video ya mahojiano.[/QUOTE]
 
Unauliza vumbi store, uchaguzi wa baraza la wazee wa Chadema kashinda Ntagazwa lakini ushindi kapewa mpemba unadhani kwa sababu gani.
Ndugu Ritz,
Kwa hiyo una maanisha CHADEMA wanachofanya ni sawa na kupaka rangi ya nyumba kwa nje inayovutia wapita njia lakini kwa ndani kuna uchafu mwingi!
 

Ni kweli liko juu ya uwezo wangu ndiyo maana unajigamba now coz mlishammaliza. Get it on coward, mnachokitafuta mtakipata
 

hivi KUMBE , WE JAMAA UWEZO WAKO NDIO HUU ?
 
Licha ya kwamba Profesa Safari ametaja sababu za kugombea Umakamu Mwenyekiti, nadhani huyu msomi hakutafakari kwa umakini na kwa kina, eti anataka kukomesha Ukanda, Udini, Ubaguzi wa rangi au Ukabila na Kijinsia, Umaskini na Ujinga pamoja na Ubadhirifu.

Kwanza kuhusu Ukanda, CHADEMA kilianzishwa na Mtei wa Kanda ya Kaskazini, lakini kwa juhudi kubwa za huyu Muasisi, akisaidiwa na waliomrithi na wanachama wengine, kimeenea nchi nzima: Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Mtwara, Lindi na mikoa yote ya Pwani, Kati na Kaskazini kwao Mtei.

Kuhusu Udini, yeye mwenyewe Muislamu, na mgombea uenyekiti taifa ni Mkristo. Anataka nini cha zaidi ya
kushirikisha dini zote? Labda CHADEMA washirikishe wasio na dini (atheists) zaidi?

Ukabila na Rangi haviko Chadema. Hata sijui kabila la Prof. Safari, na nikiwa mpiga kura katika jimbo lake, namhakikishia kura yangu. Ubaguzi wa kijinsia hauko kabisa CHADEMA. Uliza wakina mama wa Chama.

Umaskini, Ujinga na Maradhi vinatushinda sisibsote, kutokana na ufinyu wa fedha na zana za kukabiliana navyo. Hilo ni tatizo la kitaifa kwa chama chochote cha siasa, hata CCM chama tawala, licha ya kwamba Ubadhirifu na Rushwa vikitokomezwa tutamudu zaidi majukumu hayo.

Kwa hiyo kwa jumla, Profesa ni vema ujue matatizo na kiini chake. Nina hakika uongozi wa sasa wa CHADEMA utanufaika, endapo juhudi zako za kujiunga nao kama Makamu Mwenyekiti, zitafanikiwa. Kila la kheri.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…