Kuna Propaganda nyingine za Kitoto kbs na sijui km wanaozitoa wana "akili timamu". Mtu anatoka mapovu kupotosha CHADEMA ni chama cha wachaga.. hivi kweli amereason?
Chama kina wabunge kila kona ya nchi lakini kinaitwa cha wachaga. Chama kina wabunge Musoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Singida, Dar, Kigoma, Iringa kinaitwa cha Wachaga. Chama kina madiwani Songea, Shinyanga, Singida, Moshi, Tanga, Morogoro, Pwani, Geita, Simbawanga, Mpanda eti still ni cha wachaga.
Uchaguzi mdogo wa udiwani uliopita CHADEMA ilishinda kiti cha Idiwani Njombe mjini kilichokuwa chini ya CCM. Eti bado kinaitwa cha wachagga. Hivi hadi wabena nao siku hizi ni wachaga? Akili ndogo bhana.!!
Mbona hamsemi UDP ni chama cha wasukuma kwa sababu kipo Bariadi tu?? M/kiti UDP- John Cheyo (Bariadi), Makamu Isaac Cheyo (Bariadi), Viongozi wa juu wote wa Bariadi..
Chama kina mbunge mmoja tu wa Bariadi, chama kina madiwani wilaya moja tu ya Bariadi, Structure iliyokamilika ya chama iko eneo moja tu Bariadi,
Chama kina kiongozi mmoja tu wa Halmashauri Bw.Benjamin Stephen wa Bariadi....Mtaji mkubwa wa chama kwenye uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo upo Bariadi...
Mbona pamoja na hayo yote hamsemi UDP ni chama cha Wasukuma, mnang'ang'ana tu kuwa Chadema ni cha wachaga?? Hivi ukiwa CCM lazima uwe na akili ndogo ya kushindwa kureson hata vitu vyepesi hivi?? Shameee.!!