FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hakika sio jambo dogo na hii inawezekana kwa Serikali inayokumbatia na kulea shughuli haramu, wizi na kila aina ya uchafu ndani ya jamii. Kama wahudumu wa ndani wanapata fursa ya kugeuzwa punda wa kubebeshwa sembe itashindikana vipi kwa wao kumiliki magari ya mitumba....
Ama kweli tumelaaniwa na kukosa uwezo wa kufikiri kwani hata mkuu wa kaya aliwahi kutamka wazi kuwa foleni na msongamano wa magari jijini Dar ni ishara ya maendeleo na kukua kwa uchumi...
Kubeba sembe ni tamaa ya mtu.
Mimi nna hausigeli nilitoa kisa chake humu, aliniomba nimdhamini kununua bodaboda moja kwa mkopo, naam, sikufanya ajizi nikamdhamini. Ndani ya miaka miwili akawa na bodaboda 5 naye still anafanya kazi kwangu. Hivi sasa ana bodaboda kama 20 na ni mjasiriamali wa kusifiwa na hakubeba sembe wala ngano.