buyegiboseba
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 535
- 145
Binafsi sina shida na ukabila wala mtoto wa nani kawekwa wapi,swali la msingi kwa thinker makini yoyote ni "Je wamedeliver vema kama wabunge? tuwapime kwa perfomance na sio kabila,kuleta hoja ya ukabila ni sawa na kuturudisha zama za feudalism,Hakuna hatia kwa watu wa kabila moja kuwa na nafasi za uongozi,cha msingi wanaweza na wana sifa?Kumbuka pia wale wanaokuwa karibu na wanasiasa ndio hujishugulisha zaidi na siasa,unategemea chadema waweke mgogo viti maalumu wakati hana sifa,si mwanachama hakijui chama vizuri,hii si sawa,mimi natoka kabila kubwa kuliko yote barani Africa na pengine duniani lakini siwezi kuanza kushabikia issue ya ukabila,hii ni dalili ya wivu na uvivu wa kufikiri,tujenge hoja kwa mtazamo wa kisasa na si wa ujima na ukabaila.
Ya Rwanda na Burundi yanatosha kutufundisha
Ya Rwanda na Burundi yanatosha kutufundisha
godsenior hapa umenena kero yangu kubwa kuhusu Chadema. Binafsi nawafagilia sana Chadema, lakini kwenye suala la ukabila wananipa wasiwasi mkubwa. Kusema kweli bila ushabiki hili ni doa kubwa sana la Chadema, na watu kibao wanalisema japo kwa kunong'onanong'ona.
Angalizo: wahusika wasilifanyie mzaha bali walifanyie kazi ili watu wawe na imani kubwa na chama. Wasipofanyia kazi hili, kwenye uchaguzi ujao siwapi kura ya Urais honestly, ila nitawapa ya mbunge na diwani. Ilivyo sasa inajenga picha kwamba Chadema ikichukua nchi, ikulu watajaa wachaga tupu!