Dharau: Airtel wameanza kufungia laini zisizosajiliwa

Dharau: Airtel wameanza kufungia laini zisizosajiliwa

me mwenyewe muhanga mkuu Jana ucku niliwasiliana vzuri tu na watu nashangaa Leo napiga wakataa halafu kuna kihela changu nimehifadhi kwenye line yao

me nadhani wameamua kutuonyeshea example namna gani wameikamata nchi
 
kaka kwanini hukusajili kwa alama za vidole kwq msisitizo wote ule...
mbaya zaidi airtel huwq wanatukumbusha wateja wao kuzisajili hizi lain zetu kila siku ukipiga tu simu kwa mtu kabla simu haijapokelewa unakumbushwa na mhudumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilihangaika na foleni za vitambulisho vya uraia mwanzoni kabisa lakini sikupata kitambulisho wala namba ya nida,na kimsingi wahanga wa hili ni wengi tukaambiwa turudie tena tuka tiii tukaanza upya mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia,lakini mpaka sasa sina kitambulisho wala namba ya NIDA.

Hitimisho,
Sio kila asiye sajali ni mkaidi wapo wengi sana wanateseka na hili zoezi kwasababu ya uzembe wa NIDA,kama wewe umefanikiwa usiwaone wengine wajinga.
 
ETI WANAFUNGA HUDUMA ZA KUPIGA SIMU, LAKINI SMS UNATUMA KAMA KAWAIDA.
 
Wanaosema eti kwanini hatujasajili.
Napenda niwambie kwamba nyie Ni wabinafsi, mnajiangalia wenyewe.
Mnahisi Kuna mtu hapendi kuwa na kitambulisho Cha utaifa?
Kama upo karibu na ofisi za NIDA hebu jaribu kuchungulia kwa mbali uone foleni iloko pale, na hai watu wanafatilia namba tu.
Watu waliandikisha 2 years ago lkn mpaka leo hhawajapata namba,
Alafu from no where unasema kutosajili laini Ni dharau?
Jiangalie Mara mbili
 
Mimi wamenifungia , nimejaza fomu mpka leo sijapata no na muda wa kuzunguka Sina nalea 😥😥😥
 
Nawahama mazima subiri nifufue line yangu ya Ttcl
 
Back
Top Bottom