Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Hata sitaki kukumbuka dah! Wenye wtoto jitahidini kulea watoto wenu wenyewe na sio kwa kuwaacha kwa ndugu au jirani . Mambo mengine hata nikikumbuka ni kama childhood trauma. Very disturbing kwa kweli.
Ongea ili yaishe
 
Beki tatu aligoma kunifungulia mlango. Na mabegi yangu nikatamani nigeuze sema ilikua mbali mkoa.
Kaniambia boss wake kamwambia asimruhusu mtu kuingia ndani.
Nilikaa nje ya fence mpaka mwenyeji wangu alivyorudi kutoka job ndio nikazama ndani.
 
Ugenini Jamani kuna mambo Mengi sana. Na si ajabu unapoenda ugenini ukakutana na majanga tofauti tofauti.
Ugenini kuna watoto waliokosa adabu, ugenini kuna watu wasiopenda wageni anaweza kuwa mume au mke.
Unaweza kufika ugenini kumbe mmoja hana taarifa ile tu unaingia unaona watu Hawana furaha.
Kuna ndugu yangu aliwahi kunisimulia kuwa alikwenda mahali kumsalimia Shangazi yake.Mawasiliano yote alikuwa akifanya na Shangazi yake.
Mara baada ya kuwasili tu nyumbani na hata hajaingia ndani mume wa Shangazi yake anauliza huyu kijana amekuja kufanya nini hapa?
Chagua moja niondoke mimi au aondoke shangazi yako?
Mwenye Shangazi yake akakaa Kimya na kuendelea kumwandalia mgeni Chakula.
Anaeleza kuwa hakujisilia vizuri.
Wewe ulikumbana na nini ugenini?
Na huyo ndugu yako ndiyo wewe sasa , au sio mkuu ?
 
Beki tatu aligoma kunifungulia mlango. Na mabegi yangu nikatamani nigeuze sema ilikua mbali mkoa.
Kaniambia boss wake kamwambia asimruhusu mtu kuingia ndani.
Nilikaa nje ya fence mpaka mwenyeji wangu alivyorudi kutoka job ndio nikazama ndani.
Duuu pole 😅
 
Kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia kipindi akiwa dogo hivi mzee wake alikuwa mkoloni kweli alikuwa haangalii ni ndugu zake (mzee) au wa mke wakija ni wanalala kwenye mkeka na kila siku nguna ngumu na dagaa , unaambiwa ndugu walikuwa wakikaa siku nyingi ni mbili wanaaga 😁
 
Kuna jamaa yangu akiwahi kuniambia kipindi akiwa dogo hivi mzew wake alikuwa mkoloni kweli alikuwa haangalii ni ndugu zake (mzee) au wa mke wakija ni wanalala kwenye mkeka na kila siku nguna ngumu na dagaa , unaambiwa ndugu walikuwa wakikaa siku nyingi ni mbili wanaaga 😁

😁😁😁😁
 
Ile siku niliyoambiwa tafadhal huku usije hatuna hela ya wali na nyama dah niliapa sitokanyaga na siku nilipoenda kutembelea ndugu nikalazwa guest za buku tano tukakesha tunakimbizana na kunguni nikasema kuanzia leo sina ndugu niko mwenyewe kivyangu vyangu ukifa ntakuja kufukia kabur kiroho mvaya ila sio kuja kwako kukutembelea
 
Wanawake wa kipare shikamooni popote mlipo na roho zenu mbaya. Alikwenda binti kwa ndugu yake aliyeoa mpare. Asubuhi wakati wa chai mgeni kaambiwa hebu kaa hapo getini mpaka gari la shule liwachukue watoto. Alivyorudi ndani chai imekwisha kila mtu na hamsini zake, mchana mama wa kipare kapiga desh anajua mwenyewe alikokula. Chakula kilipikwa usiku wakati mume amerudi,na siochakula Cha kushiba MTU, unawajua wapare Tena kwenye kubana matumizi. Ile jioni ndio Mara ya kwanza binti mgeni anatia kitu tumboni. Kumuambia Kaka yake kwamba tangu asubuhi amepishana na chakula hawezi.
Siku tatu nyingi, binti alirudi kwao.
 
Ugenini Jamani kuna mambo Mengi sana. Na si ajabu unapoenda ugenini ukakutana na majanga tofauti tofauti.
Ugenini kuna watoto waliokosa adabu, ugenini kuna watu wasiopenda wageni anaweza kuwa mume au mke.
Unaweza kufika ugenini kumbe mmoja hana taarifa ile tu unaingia unaona watu Hawana furaha.
Kuna ndugu yangu aliwahi kunisimulia kuwa alikwenda mahali kumsalimia Shangazi yake.Mawasiliano yote alikuwa akifanya na Shangazi yake.
Mara baada ya kuwasili tu nyumbani na hata hajaingia ndani mume wa Shangazi yake anauliza huyu kijana amekuja kufanya nini hapa?
Chagua moja niondoke mimi au aondoke shangazi yako?
Mwenye Shangazi yake akakaa Kimya na kuendelea kumwandalia mgeni Chakula.
Anaeleza kuwa hakujisilia vizuri.
Wewe ulikumbana na nini ugenini?
Hakuna dharau ya ugenini ilikuwa inanikera sana kama kuzungushwa zungushwa huku na kule kwa taksi, kumbe safari yangu ilikuwa ni mtaa wa nyuma tu hapo.

Ova
 
Dogo mmoja alikwenda Amani, Miheza. TANGA kutafuta vibarua, mwenyeji wake alikua anakaa servant quarter ya mama mmoja. Basi dogo alipofika alimkuta mwenyeji Wake,wakala chakula vizuri baadaye mwenyeji wake akamwambia waende bar wapate mbili tatu kwa ajili ya baridi Kali kule Amani. Sita usiku wanarudi wako tila Lila wanamkuta mama mwenye nyumba Yuko nje. Mama mwenye nyumba akawaambia hataki kuona mgeni analala kwenye servant kwota, kwanini hawakumpa taarifa mchana? Kumbuka hiyo Ni saa sita usiku na baridi ya Amani inakaribia zero degrees. Mwenyeji kwa vile alikua amelewa akafungua mlango akaingia kulala. Mgeni Ni mgeni kweli kule Amani hajui pa kwenda.
Kipindi hicho Kuna baridi Makambako ikasome, dogo pombe zilikatika katu. Akaenda kwenye klabu ya mataptap kulala kwenye mabenchi. Ile swala swala ilimkuta njiani anarudi alikitokea. Huku akiapa akirudi Amani aitwe mbwa.
 
Back
Top Bottom