Dogo mmoja alikwenda Amani, Miheza. TANGA kutafuta vibarua, mwenyeji wake alikua anakaa servant quarter ya mama mmoja. Basi dogo alipofika alimkuta mwenyeji Wake,wakala chakula vizuri baadaye mwenyeji wake akamwambia waende bar wapate mbili tatu kwa ajili ya baridi Kali kule Amani. Sita usiku wanarudi wako tila Lila wanamkuta mama mwenye nyumba Yuko nje. Mama mwenye nyumba akawaambia hataki kuona mgeni analala kwenye servant kwota, kwanini hawakumpa taarifa mchana? Kumbuka hiyo Ni saa sita usiku na baridi ya Amani inakaribia zero degrees. Mwenyeji kwa vile alikua amelewa akafungua mlango akaingia kulala. Mgeni Ni mgeni kweli kule Amani hajui pa kwenda.
Kipindi hicho Kuna baridi Makambako ikasome, dogo pombe zilikatika katu. Akaenda kwenye klabu ya mataptap kulala kwenye mabenchi. Ile swala swala ilimkuta njiani anarudi alikitokea. Huku akiapa akirudi Amani aitwe mbwa.