Maajabu ya Mussa serikali ya Samia kuja na program uchwara kwa jina: "madaktari wa mama."
Madaktari bingwa hao hupiga kambi kwenye hospitali za mikoa na wilaya moja baada ya nyingine, kwa danganya toto ya kuwafikishia wanyonge huduma. Leo wako huku, kesho kule.
Angalia posho zao za kujikimu na safari wanazokomba sasa. Mbona zilitosha mno kuajiri madaktari wa kutosha na wakakaa kwenye hospitali hizo huko siku zote?!
Hii nchi kila kitu ni siasa + upigaji kwa kwenda mbere?!
Kwa kufikia kutaka kuwa mabingwa kwenda kujitolea hivi; kwa nini kwa kuanzia, mpango uchwara huu wa ulaji na hawa "madaktari wa mama" usisitishwe mara moja?
Iko kama vile serikali hii, wanatuona kama manyani tu.
Tate Mkuu,
johnthebaptist,
Lucas Mwashambwa kwa utambuzi.