Dharau za Serikali ya CCM sasa zimezidi; Daktari Bingwa anatakiwa kujitolea

Dharau za Serikali ya CCM sasa zimezidi; Daktari Bingwa anatakiwa kujitolea

Hili ni tangazo likimuhitaji Daktari Bingwa katika hospitali ya serikali!

Hivi kweli serikali imeshindwa kuajiri na sasa inataka watu wafanye kazi kwa kujitolea?
Kwamba mtoto wa Rais, au Waziri au hata Mkuu wa Mkoa na wilaya angekuwepo mwenye sifa angetakiwa kujitolea?
Kwamba sasa serikali inataka kusambaza umaskini kwa watoto wa walala hoi!

Hakika mwenye shibe hamjui mwenye njaa! Badala ya kuajiri wataalam ambao watawasaidia wananchi serikali inaamua kununua mashangingi na magari ya anasa ya bei mbaya!

Tujifunze kwa Gen Z wa Kenya muda unakwenda kasi na hapa kwetu yanakuja!

HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA KUSINI TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA WA KUJITOLEA

Kumb. Na. HB.207/327/03/50

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini unatangaza nafasi 54 za Ajira ya Mkataba wa kujitolea kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) kama ifuatavyo: -

1.0. Daktari Bingwa Daraja la II - (NAFASI 02)

KITUO CHA KAZI: Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini MASHARTI YA AJIRA: Kujitolea, Mkataba wa Mwaka 1

1.1 SIFA

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

KAZI

Daktari Bingwa

MWAJIRI

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini

MUDA WA MAOMBI

28/06/2024-14/07/2024

ΚΑΖΙ ΝΑ ΜAJUKUMU

Kufanya kazi zote za matibabu ya Kibingwa.

Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa

Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.

Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.

Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake

Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement)

Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake
Ni kipimo cha uzalendo
 
Back
Top Bottom