Umeenda mbali sana kwa kuwataja watoto wa vigogo kujitolea. Hoja ya msingi hapa ni kwamba serikali haina uhitaji wa madaktari bingwa? Kama inahitaji nao kwanini isiwaajili hadi wakajitolee?
Je, serikali hawana pesa za kuwaajili hao mabingwa? Hizo posho za kujitolea na matumizi ya anasa wanayofanya viongozi wa kisiasa na shughuli za kipuuzi za kuzurula zurula za kina Bashite kwanini wasiyapeleke huko? Wanajua kwa mwaka wanatumia kiasi gani kwa mambo yasiyo na faida kwenye jamii?
Nchi yetu haiendelei si kwasababu haina wataalamu wala rasilimali. Haiendelei kwasababu ya dharau ya kutothamini taaluma za watu
Huu mfumo wa kukabidhi wanasiasa kufanya maamuzi ya msingi ndio unaotugharimu. Inatia kinyaa kuwaruhusu wanasiasa kuamua mambo ya msingi ya nchi
Leo ukipita mitaani huku shule zinajengwa kila sehemu kwasababu tu kuna sera ya kujenga shule kwenye kila kata.
Hawazingatii population ya eneo, hawaangalii ukubwa wa eneo, viwanja vya michezo , makazi ya watu,...kuna shule zinageukiana yaana moja upande huu, nyingine upande mwingine ilimradi tu kila diwani ajisifu amepigania shule kwenye kata yake.Hakuna maabara, library, ofisi, wao wanajali madarasa hawanashida na ubora wala ufanisi
Wanaotumia akili wangeweza kukubaliana kata hata mbili, tatu au nne ambazo nyingi zamani zilikuwa kata moja (ziko eneo moja hilo hilo) wajenge shule moja kubwa ya maana, yenye viwango na ubora, iliyokamilika kila kitu tena ya ghorofa ili kusevu eneo badala ya kupoteza hela kwa kila kata kutandaza mabanda yake halafu baada ya miaka mitano yote yameshachakaa wakati huo bado tunashuhudia shule zilizojengwa enzi za mkoloni zikiwa bado na majengo yenye ubora kuliko hizi zetu mpya!
Hapa ndipo utakapojua akili ya Mwafrika anaijua Mwafrika mwenyewe. Unasomesha wataalamu bingwa halafu unawaambia wakajitolee ndani ya nchi yako hiyo hiyo ambayo wataalamu wanazagaa mtaani wakati huo huo raia wanakufa kwa kukosa huduma yao na wanasiasa wanagonga mvinyo mtaani bila shida yoyote