Dhuluma na wizi viwanda vya Mabati Dar, TBS oneni haya

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,605
Reaction score
1,085
Miaka ya nyuma mabati yalipigwa mhuri kuonyesha gauge au viwango (mf G32, G28), sasa hivi sio hivyo. Unanunua mabati ya mgongo mpana na kofia kwa bei ghali.

Haipiti muda kutu tayari. Unaende kiwandani unalipia mabati ya kukunja, wanakunja na kusababisha uharibufu (kuchanika), bado unalazimishwa kuchukua, wizi mtupu!. TBS na Wizara mko wapi? Ruhusu mabati toka nje.
 
Ukiwaona TBS na vitambulisho vyao vikubwa vile unaweza kudhani wanapiga mzigo kumbe hamna kitu wao wapo kukwamisha vitu vibali na kuweka kwa malipo kwa Dollar na kuruhusu vitu feki viendelee kutumika...
 
Bati za Versatile Kampuni ya Alaf ni bei Gani hapo dar?
 
Kwenye chuma ndo usiseme.
Jamaa wamepinguza urefu wa chuma kutoka mita6 Hadi mita Tano(square pipe,black pipe,flat bars,nondo yani Kila aina ya chuma na plates za mabati.

Ubora nao wamechakachua vibomba vyepesii, plate bati nyepesii yani ukitegeneza gate la France ndani ya miaka 2 inabidi ubadilishe. Nondo zenyewe zimechakachuliwa nondo ukiikunja inavyunjika kama ukuji mkavu.

Kiukweli hii nchi mamlaka zimejisahau sana, sasa wafanya biashara wanatumia uzaifu huo kuzalisha ma bidhaa yasiyokuwa na viwango maana hakuna wa kufuatilia.

TBS tokeni maofsini nendeni viwandani muone watu wanavyo chapisha bidhaa zisizo na ubora, hasa viwanda vya wachina.
 
Kweeeli. Mfano Kiwanda Mwenge kinaajiri watu kugonga ncha (ends) za squire pipes zionekane zina unene mkubwa. Stipido. Chumvi hewani inazitoboa haraka sawa "Tangi bovu" Mbezi beach
 
Kwenye bati ndio tunapigwa parefu sana aisee!

Ila nilichojifunza vitu vizuri vipo sema hela yako tu.

Nilienda kununua bati kwenye kiwanda kimoja kipo hapo vingunguti kwa nyuma, yani bati la rangi migongo mipana bei sawa na ya bati jeupe ila ukishika iko kama karatasi.

Yani ile bati fundi akipiga inabidi asirudi nyuma kukanyaga tena, akirudi mle alimokanyaga mnajikunja kama nguo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wabongo Mungu atuhurumie hatuna viongozi ila tuna takataka tu.
 
Rushwa na Umasikini

Ukiweka ubora watu wanataka bei ndogo
 
Tusubiri kilio baada ya miaka 10,kila paa linavuja,maana mabati poa yamezagaa kila kona ya nchi...
 
Bati za Aluminium ni shilling gap
 
Kanunue kiboko migongo mitano hautauta,,,bati zingine unakuta zina migongo 6 lakini feki hatari
 
Back
Top Bottom