Propaganda za Chadema kwa sasa zimejikita katika kudai "Watendaji waliitwa Ikulu" na wanachama wao kwa kutokujua wamelishikia bango.
Kwa kutotaka kuelimisha wanachama wao, kumepelekea kutojua uchaguzi wa serikali za mitaa hausimamiwi na Tume ya uchaguzi bali unasimamiwa na Tamisemi, wizara iliyoko Ikulu chini ya Ofisi ya Rais. Wala hawakuwaelimisga kanuni mpya za uchaguzinwa Serikali za mitaa zilizoanza kutumika mwaka huu.
Sasa sijui hao watendaji wangesimamiaje uchaguzi bila ya kupatiwa semina ya kanuni za usimamiaji ukizingatia Wakurugenzi waliokuwa wakitoa semina hizo walizuiliwa na Mahakama kuu, kusimamia uchaguzi?