Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Free of speech mazafakas.
Msilete ujinga wa kupangia mtu nn cha kupenda na kusema.
Pumbaaf

Ujinga ni pale tunapogundua hata kile unachokisema huwezi kukisimamia kwa sababu kuna mtu kafikiri badala yako! [HASHTAG]#umaskini[/HASHTAG] wa mawazo ni mbaya kuliko wote#
 
The threat is really and struggle like wise... we need to wake as a wise person once said, "Tanzanians are dead body who can never wake up from their sleeping" lets prove them wrong by waking up and put things straight!!!
 
Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa.



Wimbo huo hata hivyo umepokelewa kwa hisia tofauti.

Hizi ni sababu zake kwanini ameamua kuuachia:

Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo linaweza likawa haliko sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima na Busara kwenye kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke sawa…Busara na Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi tuyatakayo tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha Clouds360 cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi asubuhi maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima na busara kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa ruksa na sasa hivi maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi hadi usiku mnene… hivyo tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki, wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo hayo hawaishi Tanzania wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija kutokea bahati mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko walipo…halafu sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu usiku kucha.. Hatutaki makelele ya Uchonganishi mitandaoni, kama mtu kweli anauchungu na nchi na kweli akisemacho anamaanisha aje, na kwa pamoja twende sehemu husika kupeleka malalamiko sio kukaa kitandani kupost kuchochea Ugomvi kumbe anatuchora na kutufanya kama sie mataahira wake, anatupeleka mara kushoto mara kulia… Akikaa pekeake anatucheka kuwa sie wajinga wake katueka mkononi…
 
Me naona Domo yuko sahihi kwasababu hakuna ulazima wa yeye kuongelea au kuingilia mambo yasiyomuhusu.
Tena bora akae kimya kabisa.
 
Dogo hajielewi..Anazidi kukimbiza mashabiki wake. Eti anasema ugomvi wa Gwajima na Bashite kausababisha Mange. Njaa mbaya sana,anawaza leo tu badala ya kufikiria miaka kumi ijayo. To hell diamond
Unakimbia wewe sungura sie bado tuna furah nay3
 
Ninachosikitika siasa zimetugawa, yaani imekuwa kama uadui, na hii sumu wanaisambaza watu wa upinzani ni sumu mbaya sana, itafika kipindi utashindwa kumsaidia mtu tu kisa itikadi zenu tofauti, sasa kosa la diamond platnumz lipo wapi, hii inchi kila mtu yupo free kuchagua anachokitaka ili mradi asivunje sheria, diamond kawasilisha maoni yake kupitia mziki. Kuwa na itikadi tofauti isiwe tatizo, ila Ninachosikitika sana wanasiasa na mitandao ya kijamii inatugawa vibaya sana, mpaka inafikia Kipindi tunaomba mabaya yatokee kwa nchi yetu, ili kuikomoa serikali, yaani mpaka kwenye kusifia tunakosoa na kwenye kukosoa tunasifia.Watu wanaomponda diamond platnumz ndio hao wanalalamika kila siku inchi haina demokrasia, lkn hawajui diamond platnumz ametumia haki yake ya msingi ya demokrasia kawasilisha mawazo yake kupitia mziki wake. Tanzania kwanza, tusilichukulie hili swala la ROMA kisiasa eti ni la upande fulani. Nammlaani sana kimambi, kwani hii sumu anayoisambaza, haina tofauti na kile kituo cha radio Rwanda kilichorusha habari za kibaguzi, mwisho wake kukawa na mauwaji ya Kimbari. Watanzania tuwe makini sana tusiruhusu mitandao ya jamii na wanasiasa watugawe.
 
Dogo hajielewi..Anazidi kukimbiza mashabiki wake. Eti anasema ugomvi wa Gwajima na Bashite kausababisha Mange. Njaa mbaya sana,anawaza leo tu badala ya kufikiria miaka kumi ijayo. To hell diamond
We na yeye nan dogo kwanza? Huna pesa bata za mawazo kusafir kwa lift bado unajiita mkubwa?
 
Diamond kauimba huu wimbo kwa akili vizuri sana nilicho gundua ndani ya wimbo huu ni direct and iderect themes. Bt wengi hawajausikiliza kwa kuutafakari
 
Mimi napenda sana nyimbo za diamond ila huu kwangu hapana
 
Katumwa na mlezi wake amchafue Bishop Gwajima.Ni nani asiye jua Gwajima alianza kuongelea bashite wa kalomije baada ya kutajwa kwenye vita hewa ya madawa ya kulevya?Mvulana huyu atakumbushwa kwa picha Mizigo ya sembe alizowahi kubeba.huyu punda angekaa kimya kama wimbo wake ulivyo.
 
Its better kuwa neutral hizo ndo akili zenye busara......watu wanajua jinsi ya kuishi na kuendeleza maisha yao bila kujihusisha kwenye mambo ya hatar na yasiyokuwa na msingi...kujitoa kwenye vita haina maana kwamba umeshindwa.....suala ni kwamba hyo vita yaweza kuwa haina maslahi upande wako....so kuji engage bila kutumia akili utakufa tuu mapema.....sorry kwa high tempered pes.
 
At least mkuu umeuelewa wimbo asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…