Diamond aibuka na kupinga wimbo wake kufungiwa, asema nchi ina wenyewe

Diamond aibuka na kupinga wimbo wake kufungiwa, asema nchi ina wenyewe

Ukristo ni upendo, upendo hudhihirika wakati wa kukwazana kama sasa.....so far kama mkristo Niko ok na zuchu na diamond kwa chochote walichokifanya...
 
Ukristo ni upendo, upendo hudhihirika wakati wa kukwazana kama sasa.....so far kama mkristo Niko ok na zuchu na diamond kwa chochote walichokifanya...
Yesu mwenyewe alifukuza wafanyabiashara hekaluni. Diamond alichokuwa anakifanya kanisani humo ni biashara zake binafsi. Simlaumu kwa kukosea kwani hilo ni la kibinadamu. Shida yangu ipo anapokomaa kuwa yuko sawa na hajakosea chochote. Kama anaamini yuko sawa basi hiyo video akashoot huko anakofanya ibada zake.
 
Kama mkristo mpotezee....hii ndio asili yetu upendo juu ya upendo...
Hata akizidi kushupaza shingo na kutudharau....kama wakristo twatakiwa tuzidi kumwonesha upendo.

Be very careful hasira zisikutoe uweponi mwa Yesu
 
Kosa moja halihalalishi kosa lingine
Hajamaanisha kuhalalisha bali BASATA wanaangalia jina la msanii maana kama ni kosa linalofanana na mmoja kuachiwa na mwingine kufungiwa panapaswa kuwa na ufafanuzi.
Mimi ni muumini wa kanisa Katoliki na wimbo ulirekodiwa katika kanisa Katoliki kwa ruksa ya masista baada ya kuridhika na maudhui ninawapongeza kwani hata mimi sioni tatizo lolote, naamini the majority of the catholics hawana tatizo na kile kipande kilichorekodiwa kanisani na wala hawana tatizo na wimbo wote kwa ujumla wake.
 
Wakati mwingine wakafanyie hayo maigizo yao kwenye misikiti! Kwa nini kanisani kila siku? Yeye na huyo mwezi wake, wote ni waislam! Iweje wasiende kufanyia hiyo shooting msikitini, au kwenye Madrasa?

Hongereni sana BASATA. Angekuwa ni Mkristo akaenda kufanya hayo maigizo msikitini, muda huu zingekuwa kelele nchi nzima.
Japo sina tatizo kabisa na wimbo husika lakini nakubaliana na sentensi yako ya mwisho.
 
Huo utamaduni wa hawa wasanii kukimbilia makanisani kufanyia maigizo yao uliletwa na nani?

Kanisa ni nyumba ya ibada, inaheshimiwa na wanaoabudu mahali husika, unapokwenda kufanyia maigizo yako pale kisa kuna fulani aliwahi kufanyia huko haiwezi kuwa defence.

Huyo director wake alikosa sehemu nyingine yoyote ya kufanyia hilo igizo lao? au walichagua kanisani kwasababu wanaamini Kanisani ndio delicate place itawavutia watu kutazama?

Hao watu watakaovutiwa kuona nyumba yao wanayoiheshimu kwa ajili ya ibada zao inafanyiwa maigizo ni watu wa aina gani? wajifunze kuheshimu vitu vya watu, waache kufanya mambo kwa mazoea.

Naamini huu uamuzi wa Basata utakuwa fundisho kwa wajinga wengine waliokuwa na mipango ya aina hiyo. Diamond kama anaona ameonewa na Basata next time akaombe kufanyia maigizo yake msikitini.
Wakristo hatujaona kama hilo ni tatizo.Waislam wasitusemee na kulinganisha msikiti na kanisa.Sina haja ya kuweka namna kila dini inavyochukulia majengo yake ya ibada ila naona kuna juhudi ya kufananisha visivyofanana.
 
Naomba nitoke nnje ya mada kidog!

Hivi BASATA wanauona Diamond peke yake tu? Mbona kama wapo kishabiki sana

Hizi nyimbo za singeli wanaziona kweli?, sio audio wala video hovyooo tu ila sijawah sikia msaani wa singeli kafungiwa
 
Wakati mwingine wakafanyie hayo maigizo yao kwenye misikiti! Kwa nini kanisani kila siku? Yeye na huyo mwezi wake, wote ni waislam! Iweje wasiende kufanyia hiyo shooting msikitini, au kwenye Madrasa?

Hongereni sana BASATA. Angekuwa ni Mkristo akaenda kufanya hayo maigizo msikitini, muda huu zingekuwa kelele nchi nzima.
Wengine waislam jina tu. Ila matendo km Sio waislam.

Of course hawezi kutumia msikiti kufanyia masuala ya mziki. Lkn kitendo cha kuwaza kufanya shooting kanisani basi inawezekana sn na yeye/wao wapo kwenye mrengo wa dini hio hio ya kanisani. (wanalipenda kanisa)

Maana Kwa nini wasitumie scene nyengine km shuleni labda au arusini!!!
 
Kwanza nikwambie waislam hawawezi kuruhusu upuuzi ukafanyika msikitini, pili hao mondi na zuchu waliangalia wapi panaweza kuchezewa chezewa kati ya msikiti na kanisa wakaona kanisa ndio sehemu unaweza fanya chochote, mwisho kabisa hili la kufungia video wapo walioreact hadi video kufungiwa basata katumika tu. Narudia tena uongozi wa kanisa hautakiwi kuruhusu mambo ya kipuuzi kufanyika kanisani.
 
Wengine waislam jina tu. Ila matendo km Sio waislam.

Of course hawezi kutumia msikiti kufanyia masuala ya mziki. Lkn kitendo cha kuwaza kufanya shooting kanisani basi inawezekana sn na yeye/wao wapo kwenye mrengo wa dini hio hio ya kanisani. (wanalipenda kanisa)

Maana Kwa nini wasitumie scene nyengine km shuleni labda au arusini!!!
Ishu sio kupenda bali waliangalia wapi wanaweza fanyia ujinga wao
 
inshu au point yangu ni yule sister kupokea simu alafu anaongea nae ni msela fulan brazameni wa mtaani sio muumini wa kanisa na sio kiongozi wa kanisa mbaya zaidi wanaongelea mapenzi sio neno la mungu navyojua au kufahamu kwamba masister wa kanisa ni mabikira wenye hofu . Kwamfano ile scene angefanya msikitini au madrassa waislamu wangemchukuliaje.kwa ufupi diamond ameshaishiwa
sasa anakurupuka kurupuka tu
 
Yesu Kristo alienda msalabani ili mimi na wewe tusihukumiwe. Alifanyika laana ili sisi tuwe baraka. Kupitia yeye tunao uzima wa milele.

Kuna siku utauhitaji sana msamaha wa Yesu Kristo na itakuwa too late kwako. Nakuombea rehema za Mungu na roho ya unyenyekevu ili uipokee neema hii wakati ukiwa bado na nafasi.

Asubuhi iliyo njema inakuja, hapo wote waliomkubali Bwana Yesu watakapokuwa pamoja naye milele mbali na shida na mateso ya dunia hii.

Yesu anakupenda sana FaizaFoxy
Acha kutulisha matango pori wewe, ule mstari unaosema "Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe " huwa kinamaanisha nini ikiwa kuna mtu alitundikwa msalabani ili sisi tuokoke?
 
inshu au point yangu ni yule sister kupokea simu alafu anaongea nae ni msela fulan brazameni wa mtaani sio muumini wa kanisa na sio kiongozi wa kanisa mbaya zaidi wanaongelea mapenzi sio neno la mungu navyojua au kufahamu kwamba masister wa kanisa ni mabikira wenye hofu . Kwamfano ile scene angefanya msikitini au madrassa waislamu wangemchukuliaje.kwa ufupi diamond ameshaishiwa
sasa anakurupuka kurupuka tu

Tangu 2010 huyu mjomba mnasema kaishiwa tu
 
Alikuwa anafanya sacrifice Abraham na aliyekuwa anatakiwa kuwa sacrificed ni mwanaye (Isaka) na ndipo Mungu akamzuia Abraham asimchinje mwanaye bali achukue yule kondoo aliyekuwa amenaswa kwenye kichaka.

Sasa hiki ndio Mungu amefanya kwa Kristo Yesu, ametuepusha sisi na kuangamia kwa kumleta mwanaye achukue nafasi ambayo tunastahili. Yesu ndio sawasawa na huyo kondoo na damu yake ndio imeleta ukombozi.
Mkuu kwani yesu sio mungu? Mbona maelezo yako yanaonyesha sio
 
Back
Top Bottom