Iko hivi.
Unatakiwa ufike masaa 2 kabla ya ndege kuruka, kama unaondoka na ndege ya sa 4 kamili, inabidi ufike kuanzia sa 2 kamili. Ikifika sa 3 na dakika 20, yaani dakika 40 ifike sa 4 kamili ndege iruke hua wanafunga mlango wa kucheki in.
Maana yake kama hukufika ndani ya muda huo hadi muda wa kucheki in ukaisha, wewe hutaruka na hiyo ndege ya sa 4 kamili asubuhi.
Sasa, hua kuna watu unakuta hakukata tiketi kutokana na kuchelewa au safari imetokea ghafla inabidi asafiri, unaenda uwanja wa ndege pale mlango wa kwanza wa kucheki in unaruhusiwa kuingia bila tiketi maana unaweza kua ulibook na hukupata tiketi, hvyo jnaenda kupewa tiket ndani, unacheki in kama kawaida kisha unaenda kwenye dawati la wahudumu wa ndege husika, unawauliza kama kuna siti, wanakwambia subiri muda wa kucheki in uishe ili tujue nani hajaja tukuuzie tiketi yake.
Kweli muda ukiisha na hakuna waliotokea au walikuja wamechelewa unauziwa ile siti kisha unaungana na wasafiri wengine mnaruka na ndege.
Masaa mawili kabla ndege haijaruka hua mfumo wa kuuza tiketi unajifunga automatically, hata kama siti zipo mfumo unajifunga kuanzia mtandaoni hadi kwa wakala wale wa nje, ila wale wa ndani wanaweza kukuuzia tiketi kama abiria husika hakuja au kuna siti nyingine za wazi.
Hvyo watu wengi waliokosa au waliochelewa kubook tiketi na wana ulazima wa kusafiri muda huo hua wanafanya hvyo, wanaenda kubahatisha na kuwaombea wenzao wenye tiketi halali wachelewe au wapate dharula wasije ili wao wasafiri. Hvyo mtu kama huyo huwahi kucheki in ndani ya muda wa kucheki in hata kama hana tiketi.
Natumai umepata mwanga.