Diamond amempa nini shetani mpaka kapata pesa nyingi sana na umaarufu wote huo?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Wasanii wakubwa tena wakongwe wanalalamika mziki wa bongo fleva haulipi k.v Chidi benz, Veemoney na Dudubaya, Diamond amewezaje kupata hela hadi ya kununua rolls royce na kulipa bodyguards? Diamond anafahamika hadi Nigeria, Na Afrika nzima, hakuna msanii wa kibongo anayefahamika kama Diamond.

Kama Diamond anatumia uchawi kufanikiwa, mbona wasanii wengine Wakubwa wa bongo fleva Wanaoaminika kutumia uchawi, kama kina Jide na Kiba hawajafanikiwa kama Diamond? Kiumaarufu na kipesa? Pamoja kwamba Diamond ni mpambanaji mwenye bidii, Diamond anatoaga kafara gani la kichawi?

 
Stori za mtaani na vijiwe vya kahawa ni kwamba jamaa ni filiimathoni kitengo cha bones and skulls. Ofisi yake ina vinyago vya mafuvu na mifupa.Ndio maana anavaa mapete/macheni yenye mifupa na mafuvu. Nenda kagugo bones and skull secret society
 
Duh kwa hiyo na Bwana Bilgates, Elon Musk, Ambhan, na wale mabilionea wote wamepata kupitia shetani?
Maana diamond sio bilionea kwa kipimo cha kimataifa.
Tuache fikra potofu, tupambane
 
Fanya kazi kwa bidii, diamond analala masaa manne kwa siku jiulize wewe ubalala masaa mangapi na masaa mnagapi unatumia kwa shughuli ambazo hazikuingizii hela
 
Kufanikiwa kwa Diamond Platnumz kupo kwenye siri ya kufanya vitu ambavyo wasanii wenzake wameshindwa kufanya, kuweka self-interest zao pembeni.
 
Diamond anafanya kazi kwa bidii wakati wote na hakuna mganga atakaekumbia ukakae home hela zikufuate, Diamond ni role modo wa vijana wengi watanzania kwa sababuhakuna hata wakati mmoja unaweza kupata fedha ukiwa umekaa tu, lazima uhusike mahali ndipo fedha ziingie.
 
Haya pita pale wasafi media utume salamu maana umezunguka weeee mwisho umeonesha rangi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…