Diamond anafanya biashara gani?

Diamond anafanya biashara gani?

Kuna tetesi partner wake bi Zari pamoja na mumewe waliotengana walikuwa wakifanya biashara ya unga. Sasa sijui kama waliacha au vipi. Lakini naona huu mchezo umekuwa mkubwa hapa Tz. Wauza unga wanakuwa karibu na wasanii, alafu fedha za unga zinakuwa zinatakatishwa kana kwamba zinatoka kwenye mauzo ya wasanii hao n.k Aina hii ya Money Loundering naona iko juu sana.
 
Msisahau kwamba Mwandishi anaishi Dar
Na Dar ndio story zenu Kujadilia watu wenye mafanikio na kuomba wafilisike.Baadhi yenu lakini.

Maisha wakati unasoka watu hawakuangalii,ila muda umeotumia ku struggle pia watu hawauoni.Ila ukipata mafanikio tu basi utasikia watu aaahhh amepata hela juzi tu tena ghafla,sijui hata imeuwaje

Leo hii imefikia kwamba kila msanii mwenye mafanikio Dar basi ni muuza Unga
Na hii mentality imekaa kwenye vichwa vya watu,badala ya kufanyakazi na kujituma kwenye biashara wamekalia majungu tuuuuuuuuuu.Watu wanatoka Bush au Mkoa wanapiga hela wanasepa watu mnaendelea na majungu yenu.

Kama mwandishi ameshindwa kujipanga juu ya hili,hao wana jiji sijui vichwa vipoje.

Eti anadi mali zake.Kwani wewe mkeo hadi akuambie kila kitu?
Diamond ni Brand nyingie kabisaaa,aachweeeee
 
Kwa makala hio inadhihirisha umbumbumbu au ukanjanja FIRST CLASS wa mwandishi huyo wa gazeti la Raia Mwema.

Mwandishi gani ambae kwa dunia ya sasa unajua eti chanzo kikuu cha fedha kwa mwanamuziki ni mauzo ya album?? Hajui kama kuna mauzo ya ringtones, tours za kimuziki ambazo ndio zinalipa zaidi, matangazo ya kibiashara kutoka makampuni mbalimbali n.k

Ni dhahiri shahiri kuwa mwandishi ni mburula kwenye nyanja ya muziki na sanaa kwa ujumla..!!
 
-Kuuza Ringtones???? Statistic zipo???
-Kapiga show nyingi???? Statistic zipo???
-Endorsement Voda,Coca-Cola,GSM? ??? stats zipo??
Je hizo show alizopiga kuanzia 2009 za mil10 hadi sasa zinaweza kumpa mabanda yote hayo? Je nidhamu ya fedha ndio hiyo ya kufanya bday ya mil90? Kumbuka pia kuna fela,suka,tale na sallam ukiwaacha dancers na groupies.
 
Venye wivu wajinyonge sana {wenye wivu wajiinyongeee}
 
-Kuuza Ringtones???? Statistic zipo???
-Kapiga show nyingi???? Statistic zipo???
-Endorsement Voda,Coca-Cola,GSM? ??? stats zipo??
Je hizo show alizopiga kuanzia 2009 za mil10 hadi sasa zinaweza kumpa mabanda yote hayo? Je nidhamu ya fedha ndio hiyo ya kufanya bday ya mil90? Kumbuka pia kuna fela,suka,tale na sallam ukiwaacha dancers na groupies.

Kamw kanzu haifanani na dera [emoji23][emoji23]
 
Kwa makala hio inadhihirisha umbumbumbu au ukanjanja FIRST CLASS wa mwandishi huyo wa gazeti la Raia Mwema.

Mwandishi gani ambae kwa dunia ya sasa unajua eti chanzo kikuu cha fedha kwa mwanamuziki ni mauzo ya album?? Hajui kama kuna mauzo ya ringtones, tours za kimuziki ambazo ndio zinalipa zaidi, matangazo ya kibiashara kutoka makampuni mbalimbali n.k

Ni dhahiri shahiri kuwa mwandishi ni mburula kwenye nyanja ya muziki na sanaa kwa ujumla..!!

Unajua kaka tusimlaumu mwandishi bure. Anatafuta wanae waje kula. Cha msingi akae na afikirie tuu utumbo wenye maana.
Japo unaona huu kidogo hauelekei ila kuna mijitu imeshasimamia kwato za ngurue na kuamini
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Msisahau kwamba Mwandishi anaishi Dar
Na Dar ndio story zenu Kujadilia watu wenye mafanikio na kuomba wafilisike.Baadhi yenu lakini.

Maisha wakati unasoka watu hawakuangalii,ila muda umeotumia ku struggle pia watu hawauoni.Ila ukipata mafanikio tu basi utasikia watu aaahhh amepata hela juzi tu tena ghafla,sijui hata imeuwaje

Leo hii imefikia kwamba kila msanii mwenye mafanikio Dar basi ni muuza Unga
Na hii mentality imekaa kwenye vichwa vya watu,badala ya kufanyakazi na kujituma kwenye biashara wamekalia majungu tuuuuuuuuuu.Watu wanatoka Bush au Mkoa wanapiga hela wanasepa watu mnaendelea na majungu yenu.

Kama mwandishi ameshindwa kujipanga juu ya hili,hao wana jiji sijui vichwa vipoje.

Eti anadi mali zake.Kwani wewe mkeo hadi akuambie kila kitu?
Diamond ni Brand nyingie kabisaaa,aachweeeee


Kwa kifupi tuu wanakofosi liwe haliwezi kua. Baada ya wao kujaribu kila mbinu kutoka imekua ngumu sasa wanaoaka ili wote tubaki huku huku chai na kitumbua. Ndo wabongo tulivo
 
Si vibaya tukipata burudani kutoka studio,tukirudi tutaendelea na mjadala wetu kuhusu Icon wetu.



Kumbukeni na nyinyi kujitolea kwa kidogo mlichonacho.


Tokea haonyeshe hiki "kibanda" ndio yote haya yanakuja,lakini aliposema ana MALI ZINAZOFIKIA THAMANI YA $ 4M WATU WALIBEZA HAPA.

Angeonyesha na "kibanda" hiki alichonunua wiki moja na hiyo ya sauzi,basi wengi wangeshajinyonga humu.



Nimekuja kugundua kuna watu wanataka uwe chini tuu kila siku. Ili waseme flani mvivu flani hajiongezi flani hafikirii.... Ila ukipata badala ya kuja kukusuport na kukuuliza umetoboaje ili na wao wapae kama wewe, basi wataanza kubeza na kuchafua saabu tu umefanikiwa
"YE NI MTI WENYE MATUNDA, MILELE HAOGOPI KUPIGWA MAWE"[emoji445][emoji445][emoji445][emoji445]
 
Si unajua ni mwanamziki wetu nyota pia yuko karibu sana na Kinje.
Kama Bado hujasingiziwa wewe ni shoga au una ukimwi, au unauza unga au unatembea na mke/mme wa mtu basi bado huna pesa au jina au vyote
 
Nategemea waandishi wa hizi habari ni wasomi either wana Masters, Degree or Dip.

Nasikitika kuona mwandishi anatoa hoja isiyo na utafiti wa kisomi, kumvutia msomaji.

Waandishi wa sasa msidhani elimu ya darasan tu inatosha kupima idea za hoja zenu mnazotuletea.

Nategemea kuona waandishi mnafanya taaluma kulingana na mabadiliko ya technology. Huwezi kumpima msanii wa sasa kwa kulinganisha na wa mwaka 2005 or back, mziki wa sasa sisi wa kuuza albamu kama fikra za huyu mwandishi.
 
Nilijua tu Chanzo lazima kitakuwa DAR.

Waandishi na Aibu ya Taaluma.
Waandishi wengi wa habari wanashindwa kuielewa,wao waangalie mfano kwa Madaktari
Wote wataitwa Madokta,ila kila mmoja ana specific profession yake.
Ila waandishi wetu hawa,unakuta mwandishi kama daladala,yaani yeye anaandika chochote tu bila kujua uwezo wake.

Mwaandishi wa Taaluma ya Michezo na Burudani(Sanaa kwa ujumla)lazima awe amesomea Sanaa,na Chuo Kikuu cha Dar wanatoa Degree ya masuala hayo kama sikosei,na kama nakumbuka vizuri Marehem Mzirai alikuwa anasoma Pale.Na Chuo cha Bagamoyo kinatoa Kozi nzuri sana ya masuala ya Sanaa na Uchumi,ambapo utashangaa pale unakuta Wazungu wanasoma ila waswahili na waandishi na wasanii wanapita kama polisi,wanenda kwa warsha tu na vi seminar vya kuzugia ili wapate certificate of attendance

Sasa Mwandishi lazima awe na taaluma.Sasa kwa akili ya kawaida,hivi unashindwa kufanya analysis tangu alipotoka Diamond mpaka leo hii na mafanikio yake?
-Na sio lazima kila biashara mtu aweke wazi,yale ni maisha binafsi,kuna watu humu hata wake zao na waume zao hawajui anapokea kiasi gani kama Mshahara.Na ni mwili mmoja,sasa itakuwa Diamond?

Maisha yanaanza kwa Shilingi moja,then inategemea umeiwekeza vipi.Wapo watu walianza na pesa za madafu tu tena milioni moja tu,leo hii ni milioneaz wakubwa na tunawaheshim.

Diamond ana nidham kubwa sana ya Pesa tena Sana.
Kwa mtizamo wa haraka unaweza kushangaa kwanini Diamond Jina kubwa halafu anahitaji Management?Jibu moja tu ni kwamba anajtambua na anajifunza kwa Wenzie Nje ya Nchi

Hivi Unajua Billionea Dangote,ni maarufu sana Nigeria,ila kuna watu wanaishi Lagos-Nigeria,hawajui kwamba Anakiwanda cha Cement Tanzania.
Sasa maisha ni akili,sio kila kitu mtu anadi.
Big UP Diamond,licha ya kwamba kanikera kuimba Nyimbo ya matusi matupuuu ya Salome(usiingie huku Diamond,matusi matupu hayo jua ni soft copy na mungu yupo na unaiacha milele).
Hahaha! Hata bakhresa kuna watanzania kobao hswajui kuwa ana kiwanda cha ngano zambia
 
Haya mamizikiziki anayotoa kila uchao, yapo katika mfumo gani? Inamaana hayamwingizii kipato chochote?
Kwa hiyo, mapato katika tasnia ya muziki hutokana na mauzo ya albamu pekee?
Mbona unatuchanganyia habari nawee nae?
 
Mkuu hao Wanigeria wasiojua umiliki wa kiwanda cha Cement cha huyo Tajiri wa Africa labda wale wasiokuwa na mitandao ya kijamii.Especially wale waishio Kwa Mtogole ya Lagos. Ila sio wale wanaofuatilia latest news every time.
Hivi una taarifa Bahresa ana kiwanda Rwanda?
 
Makala ya Raia Mwema lina habari ya kufikirisha kidogo:

Mwandishi anauliza " Diamond ana fedha, lakini anauza nini?"
Hata mimi nimejikuta nikiuliza swali hili mara nyingi tu bila majibu. Wengine wanasema anauza matangazo, wengine ana studio nk. Lakini vipi ile biashara yake ya msingi : Muziki?

soma mwenyewe hapa chini:

Diamond ana fedha, lakini anauza nini?
SEP 29, 2016by MWANDISHI WETUin BURUDANI & MICHEZO
NASEEB ABDUL ‘Diamond Platnumz’ ananivutia sana miongoni mwa wasanii wa muziki wa nyumbani. Ananivutia kumsikiliza na kumtazama kwenye TV.

Akiwa ananengua jukwaani unaweza kujisemea kwanini asiwe ananengua na aachache na kuimba. Akianza kuimba bado utajisemea tena kwanini asiwe anaimba pekee na si kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja?

Huyu ndiye Diamond ambaye anafanya vitu viwili kwa wakati mmoja na kuvutia wengi. Wapo wanaompenda kwa kuimba na wako wanaompenda kwa kucheza.

Amejivutia mashabiki wengi kwenye maeneo hayo mawili jukwaani. Kazi zake zimemfanya hivi sasa atajwe kama msanii anayetengeneza fedha nyingi zaidi hapa nchini.

Wingi wa fedha hizo zimefanya afungue kampuni ya WCB, inayofanya kazi za kusimamia wasanii mbalimbali.

Lakini mpaka unapoweka umakini wako kusoma andiko hili, fahamu Diamond amewahi kutoa albamu moja tu ya Nenda Kamwambie mwaka 2009.

Hii ni albamu yake ya kwanza na ya mwisho mpaka wakati huu 2016. Ni takribani miaka saba sasa imepita tangu atoe albamu hiyo ambayo haikuwa na idadi kamili ya nakala alizouza.

Inakuwaje Diamond, anayetajwa kuwa msanii mwenye fedha nyingi, awe ametoa albamu moja tu kwa zaidi ya miaka saba?

Ina maana Nenda Kamwambie ndio imemlipa kiasi hiki mpaka sasa aamue asitoe albamu nyingine?

Wanamuziki, bendi na vikundi duniani kote wanaonyesha na kutangaza utajiri wao kupitia mauzo ya kazi zao ambazo zinakuwa albamu.

Hata Ali Kiba, anayekinzana naye kimuziki aliwahi kusema albamu yake ya kwanza ya Cinderella ilivunja rekodi na kuuza ‘double platinum’ kwa kuuza nakala milioni mbili.

Mauzo ya nakala hiyo anadai yalimuingizia shilingi milioni 200. Kiba aliwahi kusema hata ukimya wake kwenye sanaa haukumfanya apumzika bure, bali alikuwa na ‘jembe’ lililofanya akae pembeni kidogo.

Kwenye dunia ya sasa, wasanii wa muziki wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao na ndiyo maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.

Hii ni sheria inayotumika kwa baadhi ya nchi duniani, japo nyumbani haijaanza kutumika. Inawezekana sheria hii ingekuwepo nyumbani Diamond, angeingiza fedha zaidi.

Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili; Diamond na wasanii wetu wengine ambao hawajawahi kutoa albamu wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao ya kifahari wakati mauzo ya albamu zao ni sifuri?

Biashara ya muziki ni sawa na nyingine yoyote iwe ya kuuza barafu, mikate, machungwa au magari. Mfanyabiashara wa magari, hesabu yake hutokana na idadi ya magari anayouza. Vivyo hivyo kwa biashara nyingine.

Hawa wasanii wetu ambao hawauzi muziki, wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao? Muziki bila kutoa albamu ni biashara gani?

Nafahamu kuna maonyesho mbalimbali ambayo baadhi yao wana

Ngada
 
tuache uvivu wa kufikir... album hazilipi.... ela zipo kwenye tour, matangazo, shows...... jamaa sehem zote yuko vizuri
 
Back
Top Bottom