laki si pesa.
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 10,003
- 9,755
Tuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WIVU +POVU.Tuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
Anafanya biashara ya muziki
Kwa hiyo unataka akifanya show akwambie ameingiza sh ngp....akiingia ubia na makampuni na penyewe aseme ampewa shi ngp-Kuuza Ringtones???? Statistic zipo???
-Kapiga show nyingi???? Statistic zipo???
-Endorsement Voda,Coca-Cola,GSM? ??? stats zipo??
Je hizo show alizopiga kuanzia 2009 za mil10 hadi sasa zinaweza kumpa mabanda yote hayo? Je nidhamu ya fedha ndio hiyo ya kufanya bday ya mil90? Kumbuka pia kuna fela,suka,tale na sallam ukiwaacha dancers na groupies.
Acha kashfa wewePiga majungu tu ukimaliza unywe chai na kiporo cha ubwabwa maharage ujiandae kujamba,mwenzio anafanya yake,mijitu.mingine bwana, wewe hujiulizi kwanini unaishi chumba kimoja AKA STOO na baba na mamaako huko shimo la udongo, unakalia majungu
Mkuu Bakhresa sio Rwanda tu hadi Zambia ,DR Congo huko kote ana viwanda vyake vipo so hata hiko cha Rwanda pia hiyo taarifa ninayo Labda uniulize Manji anakiwanda wapi siwezi kujua kwa kweli?Hivi una taarifa Bahresa ana kiwanda Rwanda?
Ahahaha Mkuu umetisha sana. Huyu Baba Tiffa ana maujumbe sana.MI NAMUOMBA MUNGU WANAKESHA WAKI WANGA -BABA TIFFA
maandishi wa habari nae anajiuliza maswali wakati kazi yake ina mruhusu kufatilia kwa kina na kumuhoji muhusika.....otherwise makala kaiandika kwa majungu na kichochezi......makanjanja bado hawajisha.Makala ya Raia Mwema lina habari ya kufikirisha kidogo:
Mwandishi anauliza " Diamond ana fedha, lakini anauza nini?"
Hata mimi nimejikuta nikiuliza swali hili mara nyingi tu bila majibu. Wengine wanasema anauza matangazo, wengine ana studio nk. Lakini vipi ile biashara yake ya msingi : Muziki?
soma mwenyewe hapa chini:
Diamond ana fedha, lakini anauza nini?
SEP 29, 2016by MWANDISHI WETUin BURUDANI & MICHEZO
NASEEB ABDUL ‘Diamond Platnumz’ ananivutia sana miongoni mwa wasanii wa muziki wa nyumbani. Ananivutia kumsikiliza na kumtazama kwenye TV.
Akiwa ananengua jukwaani unaweza kujisemea kwanini asiwe ananengua na aachache na kuimba. Akianza kuimba bado utajisemea tena kwanini asiwe anaimba pekee na si kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja?
Huyu ndiye Diamond ambaye anafanya vitu viwili kwa wakati mmoja na kuvutia wengi. Wapo wanaompenda kwa kuimba na wako wanaompenda kwa kucheza.
Amejivutia mashabiki wengi kwenye maeneo hayo mawili jukwaani. Kazi zake zimemfanya hivi sasa atajwe kama msanii anayetengeneza fedha nyingi zaidi hapa nchini.
Wingi wa fedha hizo zimefanya afungue kampuni ya WCB, inayofanya kazi za kusimamia wasanii mbalimbali.
Lakini mpaka unapoweka umakini wako kusoma andiko hili, fahamu Diamond amewahi kutoa albamu moja tu ya Nenda Kamwambie mwaka 2009.
Hii ni albamu yake ya kwanza na ya mwisho mpaka wakati huu 2016. Ni takribani miaka saba sasa imepita tangu atoe albamu hiyo ambayo haikuwa na idadi kamili ya nakala alizouza.
Inakuwaje Diamond, anayetajwa kuwa msanii mwenye fedha nyingi, awe ametoa albamu moja tu kwa zaidi ya miaka saba?
Ina maana Nenda Kamwambie ndio imemlipa kiasi hiki mpaka sasa aamue asitoe albamu nyingine?
Wanamuziki, bendi na vikundi duniani kote wanaonyesha na kutangaza utajiri wao kupitia mauzo ya kazi zao ambazo zinakuwa albamu.
Hata Ali Kiba, anayekinzana naye kimuziki aliwahi kusema albamu yake ya kwanza ya Cinderella ilivunja rekodi na kuuza ‘double platinum’ kwa kuuza nakala milioni mbili.
Mauzo ya nakala hiyo anadai yalimuingizia shilingi milioni 200. Kiba aliwahi kusema hata ukimya wake kwenye sanaa haukumfanya apumzika bure, bali alikuwa na ‘jembe’ lililofanya akae pembeni kidogo.
Kwenye dunia ya sasa, wasanii wa muziki wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao na ndiyo maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.
Hii ni sheria inayotumika kwa baadhi ya nchi duniani, japo nyumbani haijaanza kutumika. Inawezekana sheria hii ingekuwepo nyumbani Diamond, angeingiza fedha zaidi.
Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili; Diamond na wasanii wetu wengine ambao hawajawahi kutoa albamu wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao ya kifahari wakati mauzo ya albamu zao ni sifuri?
Biashara ya muziki ni sawa na nyingine yoyote iwe ya kuuza barafu, mikate, machungwa au magari. Mfanyabiashara wa magari, hesabu yake hutokana na idadi ya magari anayouza. Vivyo hivyo kwa biashara nyingine.
Hawa wasanii wetu ambao hawauzi muziki, wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao? Muziki bila kutoa albamu ni biashara gani?
Nafahamu kuna maonyesho mbalimbali ambayo baadhi yao wana
Watanzia wa Dar ndivyo mlivyo hasa wanaumeKwa hiyo unataka akifanya show akwambie ameingiza sh ngp....akiingia ubia na makampuni na penyewe aseme ampewa shi ngp
Kumbuka akifanya ivo mtasema ana show off za kijinga wa tz cjui tukoje
Ni wasanii wachache sana ambao wamewahi nufaishwa na albums hapa Tanzania na ni kipindi kilee cha nyuma kabla ya kukua kwa teknolojia kipindi ambacho ilikuwa ngumu sana kunyonya wimbo bure kutoka mtandaoni,kipindi hicho hata zile nakala chache zilizouzwa asilimia kubwa ya ingizo liliishia mfukoni kwa msambazaji(MAMU akiwa mnufaika mkubwa wa kipindi hicho).Hahaha,mkuu we acha,yaani aibu tupu
Hii ni taswira ya wandishi wetu wa Tanzania wanaoishi kwa mihemko
We si unakumbuka wale walioandika kwamba PEMBA wananchi wanakimbilia msitu wa Ngezi na wanalala huko kwa kukimbia Polisi.Cha kuchekesha waandishi kibao walioandika Pemba na Mazingira ya huko hawajui,walichofanya wlatafuta mwandishi kajanja akawa anawarushia habari za uongo.
Alichofanya Waziri,alichukua Ndege na kuwapakia waandishi wote kwenda huko,na wakakuta watu wapo makwao,na wakaambiwa kwamba Msitu wa Ngezi unalindwa na haishi mtu kule.Ikawa Aibu wakaka kimyaa.
Bado kuna tatizo sana kwa Wanataaluma wa Habari hapa kwetu.
Napenda Sana Citizen Kenya,yaani hawakurupuki
Mwandishi ni kanjanja yeye anajua pesa inaingia kwa kuuza albamu tu, hajui kwamba digital system ndo inaingiza pesa nyingi mfanohuyu mwandishi uchwara,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,jamaa anafanya matangazo ya hela ndefu,anapiga shoo,ana mke tajiri n.k
Unakunywa bia gani.??"WANAJENGA MAJUNGU MI NAJENGA VIBANDA" - Platinum a.k.a Baba Tifa.
Waandishi wengi wa siku hizi ni failure...yn anaenda uandishi tu coz hana marks za kusoma advanced level...so bora akasome kicetificate Dsj...tsjHuyu naye ni mwandishi? yani akili yake ameiaminisha msanii kupata hela hadi auze album, huyu ni mwandishi hewa.
watu bongo hii hii hawamjui Mo Dewji, uyo dangote mwenyewe naigeria huko kunawatu hawamjui pia acha kujua biashara zake.Hivi mkuu Dangote unaweza ukamfananisha na huyo Waziri wa Tanzania. Huyu jamaa mali zake zote zinapatikana kwenye mitandao so huwa hamiliki mali kwa uficho kama huyo waziri mwenye hiyo hotel huko Zanzibar. Kwanza akijipambanua ataambiwa fisadi unadhani ni rahisi kihivyo kujua mali za Magufuli kuliko kujua mali za Bill Gates.
Kama unawajua hao viongozi wenye hizo hotel huenda umeyaona hayo majengo na umepata kujua hivyo kipindi cha ujenzi ulisikia tetesi tu kuwa hili ni jengo la mtu fulani ila hakuna media iliyotangaza kama ilivyotangazwa kiwanda cha cement cha Dangote ambacho Africa mashariki na kati wote wanajua kuwa kipi sisemei nchi za mbali ya hapa maana BBC waliripoti kuhusu hiki kiwanda.
Huu ni wivu+chuki wa kiwango cha lamiTuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
Mkuu kama ulinisoma vizuri sidhani kama kuna haja ya kuendelea na huo mjadala. Huyo asiyemjua Mo kwa hapa Tanzania labda kwa wale waishio vijijini na tena hawafuatilii habari ya aina yoyote ile. Kwa wale waishio mijini hata kama hawajamuona kwa sura ila habari zake watakuwa wanazijua.watu bongo hii hii hawamjui Mo Dewji, uyo dangote mwenyewe naigeria huko kunawatu hawamjui pia acha kujua biashara zake.