Diamond anafanya biashara gani?

Diamond anafanya biashara gani?

Tuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
 
Anafanya biashara ya muziki
-Kuuza Ringtones???? Statistic zipo???
-Kapiga show nyingi???? Statistic zipo???
-Endorsement Voda,Coca-Cola,GSM? ??? stats zipo??
Je hizo show alizopiga kuanzia 2009 za mil10 hadi sasa zinaweza kumpa mabanda yote hayo? Je nidhamu ya fedha ndio hiyo ya kufanya bday ya mil90? Kumbuka pia kuna fela,suka,tale na sallam ukiwaacha dancers na groupies.
Kwa hiyo unataka akifanya show akwambie ameingiza sh ngp....akiingia ubia na makampuni na penyewe aseme ampewa shi ngp

Kumbuka akifanya ivo mtasema ana show off za kijinga wa tz cjui tukoje
 
Piga majungu tu ukimaliza unywe chai na kiporo cha ubwabwa maharage ujiandae kujamba,mwenzio anafanya yake,mijitu.mingine bwana, wewe hujiulizi kwanini unaishi chumba kimoja AKA STOO na baba na mamaako huko shimo la udongo, unakalia majungu
 
Piga majungu tu ukimaliza unywe chai na kiporo cha ubwabwa maharage ujiandae kujamba,mwenzio anafanya yake,mijitu.mingine bwana, wewe hujiulizi kwanini unaishi chumba kimoja AKA STOO na baba na mamaako huko shimo la udongo, unakalia majungu
Acha kashfa wewe
 
Hivi una taarifa Bahresa ana kiwanda Rwanda?
Mkuu Bakhresa sio Rwanda tu hadi Zambia ,DR Congo huko kote ana viwanda vyake vipo so hata hiko cha Rwanda pia hiyo taarifa ninayo Labda uniulize Manji anakiwanda wapi siwezi kujua kwa kweli?
 
Makala ya Raia Mwema lina habari ya kufikirisha kidogo:

Mwandishi anauliza " Diamond ana fedha, lakini anauza nini?"
Hata mimi nimejikuta nikiuliza swali hili mara nyingi tu bila majibu. Wengine wanasema anauza matangazo, wengine ana studio nk. Lakini vipi ile biashara yake ya msingi : Muziki?

soma mwenyewe hapa chini:

Diamond ana fedha, lakini anauza nini?
SEP 29, 2016by MWANDISHI WETUin BURUDANI & MICHEZO
NASEEB ABDUL ‘Diamond Platnumz’ ananivutia sana miongoni mwa wasanii wa muziki wa nyumbani. Ananivutia kumsikiliza na kumtazama kwenye TV.

Akiwa ananengua jukwaani unaweza kujisemea kwanini asiwe ananengua na aachache na kuimba. Akianza kuimba bado utajisemea tena kwanini asiwe anaimba pekee na si kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja?

Huyu ndiye Diamond ambaye anafanya vitu viwili kwa wakati mmoja na kuvutia wengi. Wapo wanaompenda kwa kuimba na wako wanaompenda kwa kucheza.

Amejivutia mashabiki wengi kwenye maeneo hayo mawili jukwaani. Kazi zake zimemfanya hivi sasa atajwe kama msanii anayetengeneza fedha nyingi zaidi hapa nchini.

Wingi wa fedha hizo zimefanya afungue kampuni ya WCB, inayofanya kazi za kusimamia wasanii mbalimbali.

Lakini mpaka unapoweka umakini wako kusoma andiko hili, fahamu Diamond amewahi kutoa albamu moja tu ya Nenda Kamwambie mwaka 2009.

Hii ni albamu yake ya kwanza na ya mwisho mpaka wakati huu 2016. Ni takribani miaka saba sasa imepita tangu atoe albamu hiyo ambayo haikuwa na idadi kamili ya nakala alizouza.

Inakuwaje Diamond, anayetajwa kuwa msanii mwenye fedha nyingi, awe ametoa albamu moja tu kwa zaidi ya miaka saba?

Ina maana Nenda Kamwambie ndio imemlipa kiasi hiki mpaka sasa aamue asitoe albamu nyingine?

Wanamuziki, bendi na vikundi duniani kote wanaonyesha na kutangaza utajiri wao kupitia mauzo ya kazi zao ambazo zinakuwa albamu.

Hata Ali Kiba, anayekinzana naye kimuziki aliwahi kusema albamu yake ya kwanza ya Cinderella ilivunja rekodi na kuuza ‘double platinum’ kwa kuuza nakala milioni mbili.

Mauzo ya nakala hiyo anadai yalimuingizia shilingi milioni 200. Kiba aliwahi kusema hata ukimya wake kwenye sanaa haukumfanya apumzika bure, bali alikuwa na ‘jembe’ lililofanya akae pembeni kidogo.

Kwenye dunia ya sasa, wasanii wa muziki wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao na ndiyo maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.

Hii ni sheria inayotumika kwa baadhi ya nchi duniani, japo nyumbani haijaanza kutumika. Inawezekana sheria hii ingekuwepo nyumbani Diamond, angeingiza fedha zaidi.

Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili; Diamond na wasanii wetu wengine ambao hawajawahi kutoa albamu wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao ya kifahari wakati mauzo ya albamu zao ni sifuri?

Biashara ya muziki ni sawa na nyingine yoyote iwe ya kuuza barafu, mikate, machungwa au magari. Mfanyabiashara wa magari, hesabu yake hutokana na idadi ya magari anayouza. Vivyo hivyo kwa biashara nyingine.

Hawa wasanii wetu ambao hawauzi muziki, wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao? Muziki bila kutoa albamu ni biashara gani?

Nafahamu kuna maonyesho mbalimbali ambayo baadhi yao wana
maandishi wa habari nae anajiuliza maswali wakati kazi yake ina mruhusu kufatilia kwa kina na kumuhoji muhusika.....otherwise makala kaiandika kwa majungu na kichochezi......makanjanja bado hawajisha.
 
Kwa hiyo unataka akifanya show akwambie ameingiza sh ngp....akiingia ubia na makampuni na penyewe aseme ampewa shi ngp

Kumbuka akifanya ivo mtasema ana show off za kijinga wa tz cjui tukoje
Watanzia wa Dar ndivyo mlivyo hasa wanaume
 
Hahaha,mkuu we acha,yaani aibu tupu
Hii ni taswira ya wandishi wetu wa Tanzania wanaoishi kwa mihemko
We si unakumbuka wale walioandika kwamba PEMBA wananchi wanakimbilia msitu wa Ngezi na wanalala huko kwa kukimbia Polisi.Cha kuchekesha waandishi kibao walioandika Pemba na Mazingira ya huko hawajui,walichofanya wlatafuta mwandishi kajanja akawa anawarushia habari za uongo.

Alichofanya Waziri,alichukua Ndege na kuwapakia waandishi wote kwenda huko,na wakakuta watu wapo makwao,na wakaambiwa kwamba Msitu wa Ngezi unalindwa na haishi mtu kule.Ikawa Aibu wakaka kimyaa.

Bado kuna tatizo sana kwa Wanataaluma wa Habari hapa kwetu.
Napenda Sana Citizen Kenya,yaani hawakurupuki
Ni wasanii wachache sana ambao wamewahi nufaishwa na albums hapa Tanzania na ni kipindi kilee cha nyuma kabla ya kukua kwa teknolojia kipindi ambacho ilikuwa ngumu sana kunyonya wimbo bure kutoka mtandaoni,kipindi hicho hata zile nakala chache zilizouzwa asilimia kubwa ya ingizo liliishia mfukoni kwa msambazaji(MAMU akiwa mnufaika mkubwa wa kipindi hicho).

Sasa hivi wamegundua njia ambayo angalau wanakula jasho lao nayo ni kutoa wimbo kuutangaza kisha kufanya matamasha mbalimbali.

Sasa kama mwandishi wa habari tena za michezo na burudani anashindwa kugundua jambo jepesi kama hilo sijui inakuaje!
 
huyu mwandishi uchwara,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,jamaa anafanya matangazo ya hela ndefu,anapiga shoo,ana mke tajiri n.k
 
huyu mwandishi uchwara,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,jamaa anafanya matangazo ya hela ndefu,anapiga shoo,ana mke tajiri n.k
Mwandishi ni kanjanja yeye anajua pesa inaingia kwa kuuza albamu tu, hajui kwamba digital system ndo inaingiza pesa nyingi mfano
- youtube views unalipwa
- miito kwenye simu unalipwa
- mirabaha nyimbo ikipigwa redioni hasa nje
- kufanya shows
- kufanya matangazo
- kuwa balosi wa kampuni
Vyanzo ni vingi sana ambavyo mwandishi hajui
 
"WANAJENGA MAJUNGU MI NAJENGA VIBANDA" - Platinum a.k.a Baba Tifa.
Unakunywa bia gani.??
Eti wanauliza anafanya biashara gani?...jina lake tu tyr biashara tosha...
Wajaribu kumkodi akawapigie kwenye harusi zao km saida karoli wanavyomfanya[emoji13] [emoji13]
Wamjaribu akawatangazie magazeti yao ....
Watamlipa sh ngapi....km hawajachemka
Majungu majungu tu
 
Huyu naye ni mwandishi? yani akili yake ameiaminisha msanii kupata hela hadi auze album, huyu ni mwandishi hewa.
Waandishi wengi wa siku hizi ni failure...yn anaenda uandishi tu coz hana marks za kusoma advanced level...so bora akasome kicetificate Dsj...tsj
 
Hivi mkuu Dangote unaweza ukamfananisha na huyo Waziri wa Tanzania. Huyu jamaa mali zake zote zinapatikana kwenye mitandao so huwa hamiliki mali kwa uficho kama huyo waziri mwenye hiyo hotel huko Zanzibar. Kwanza akijipambanua ataambiwa fisadi unadhani ni rahisi kihivyo kujua mali za Magufuli kuliko kujua mali za Bill Gates.
Kama unawajua hao viongozi wenye hizo hotel huenda umeyaona hayo majengo na umepata kujua hivyo kipindi cha ujenzi ulisikia tetesi tu kuwa hili ni jengo la mtu fulani ila hakuna media iliyotangaza kama ilivyotangazwa kiwanda cha cement cha Dangote ambacho Africa mashariki na kati wote wanajua kuwa kipi sisemei nchi za mbali ya hapa maana BBC waliripoti kuhusu hiki kiwanda.
watu bongo hii hii hawamjui Mo Dewji, uyo dangote mwenyewe naigeria huko kunawatu hawamjui pia acha kujua biashara zake.
 
Mwandishi ana uwezo mdogo wa kufikiria, watu wanauza nyimbo sio ablam tena siku hizi
 
watu bongo hii hii hawamjui Mo Dewji, uyo dangote mwenyewe naigeria huko kunawatu hawamjui pia acha kujua biashara zake.
Mkuu kama ulinisoma vizuri sidhani kama kuna haja ya kuendelea na huo mjadala. Huyo asiyemjua Mo kwa hapa Tanzania labda kwa wale waishio vijijini na tena hawafuatilii habari ya aina yoyote ile. Kwa wale waishio mijini hata kama hawajamuona kwa sura ila habari zake watakuwa wanazijua.
 
Kuna kitu kwenye hii makala ambacho mwaandishi hajakifafanua tusiishie kusema mwaandishi hajui kama album hailipi,hata yeye amesema kuwa kuna vyanzo mbalimbali ambavyo vinaweza kumpatia msanii hela na pamoja na show.
 
Back
Top Bottom