Mkuu mimi ni mwanamke mwenye 60+ katika kuishi kwangu nimeona matukio mengi sana ya kina mama wanapo gombana na wenza wao kazi kubwa wanayo fanya ni kuotesha chuki kati ya baba na watoto wake, hasa kipindi watoto wakiwa bado wadogo, kwa hivyo watoto wanajua baba ni mtu mbaya na asiyefaa!! Kwa hili, bi Sanura amefaulu, ila Nassib kama ana akili anatakiwa atambue kuwa mama yake ana walakin. Amtambue mama yake kama mwanamke mwenye ndimi mbili. Ulimi mmoja unatamka Abdul, na mwingine unatamka Nyange!!! Jambo la kuchekesha Abdul alitamkwa tangu akiwa mdogo, utu uzima anatamkwa Nyange!!!