Diamond apokelewa kama Rais Msumbiji, apewa heshima zote za kirais

Diamond apokelewa kama Rais Msumbiji, apewa heshima zote za kirais

Mnalipwa na huu ushabiki wenu wa kina kiba na MONDI au Ndio kupiga kelele huku unakufa masikini
 
Taarifa ya kishabiki,Fanya tafiti usikurupuke.Nipo huku waandaji wa show walipewa sharti la kwanza ni kukusnnya watu airport.Na salaam na quiz ndio walikuwa organizer wa hiyo kitu.
Msiwe mnaingia mkenge kijinga,Ukiona jambo ongeza na zako.
Hata la lissu tusingeongeza zetu ungekuta tunasubiri ripot ya polisi au bunge november.Ila tumestuka na sasa habari ya taifa ni Tundu lissu

Je hao watu wa kukusanyika Airport walipatikana?
 
Taarifa ya kishabiki,Fanya tafiti usikurupuke.Nipo huku waandaji wa show walipewa sharti la kwanza ni kukusnnya watu airport.Na salaam na quiz ndio walikuwa organizer wa hiyo kitu.
Msiwe mnaingia mkenge kijinga,Ukiona jambo ongeza na zako.
Hata la lissu tusingeongeza zetu ungekuta tunasubiri ripot ya polisi au bunge november.Ila tumestuka na sasa habari ya taifa ni Tundu lissu
Kwa jinsi mnavyosema basi huyo jamaa angekuwa ameshafilisika kwa kuhonga mashabiki.
 
Ungeambatanisha na hiyo picha ya rais ingependeza sn
 
kwenye huu uzi nimegundua kuna watu hawajielewi au hawajaelewa maana ya mleta uzi kutumia neno kama "Rais"...wengi wanauliza gwaride mara traffic mmoja,mara mizinga..huku wakisahau matumizi ya lugha katika huu uzi!

Alichokifanya mleta mada katika uwasilishaji wake ni matumizi ya lugha katika kipengele cha "Hyperbole/Mubaalagha" yaani kuongeza chumvi...si kawaida kwa msanii,hasa kutoka hapa kwetu tz, kwenda nchi za watu na kupokelewa kwa namna ambavyo diamond amepokelewa huko Mozambique..kwa mfano hata vingozi wengi mashuhuri wakitoka nje na kuja tz utakuta watu huwenda airport kuwapokea na hata kuwachezea ngoma za asili,na pia ulinzi unakuwepo,maana hata hao marais wa nchi wakienda nchi za nje hawapigiwi hiyo mizinga bali kuna heshima maalum wanapewa....

haya mambo yafuatayo ndiyo yaliyomfanya mleta uzi atumie kauli ya "kama rais" :-

1)kuwepo kwa watu wengi kiasi wanomsubiri kumpokea/kumuona kwa shauku
2)kuwepo kwa wamama wanaoimba na kucheza ngoma za asili
3)kuwepo kwa ulinzi wa kutosha..hapa mbali ya huyo traffic kuna na askari wengine wenye silaha wasiopungua 5...
4)uwepo wa sakina ya askari,yaani kimurimuri

Bado tu hamjaelewa hadhi waliyompa huyu kijana huko mozambique...au ndo chuki na vijiba vimewajaa,leteni ushahidi wa msanii mwengine ambae aliwahi kupatiwa heshima kama hiyo hasa toka tanzania .
 
Wewe team kiba tushakujua ..
Ujue haya mambo huwezi kuficha Mkuu.
Reply zako tuu hata mada za nyuma kuhusu Mond na kiba zinaonesha uko wapi
Hakika mkuu tena kuna moja alisema wazi kabisa
 
Wanabodi.
Hayo mapokezi ya Diamond ni makubwa sana amepewa heshima kubwa mno hakuna msanii tanzania aliewahi kupokelewa vile ngoja tusubiri na rekodi atayovunja ya kufanya show indigo london ambapo hakuna msanii wa bongo aliewahi kufanya show ya peke yake indigo.
amepigiwa mizinga mingapi au kaishia kupigwa vizinga!? amekagua gwaride la heshima kutoka kwa vikosi vyq ulinzi au wale ma bodybulder?
 
Watu wanafurahisha sana.. eti kahonga mashabiki waje kufurika kumpokea airport na wengine wa kuja kwny show...hebu piga hesabu ndogo tu.. assume amehonga watu 15,000 kila mmoja kapata 10,000 ili waje airport kumpokea na kuja kwny show itakua sh 150,000,000/= (milion 150).. sometimes najiulizaga hivi watu kichwani wana nini? Hamfikirii vitu vidogo kama hivi
 
Kwa taarifa yenu

DIAMOND NDIO MSANII WA KWANZA AFRICA KUFANYA SHOW KUBWA OFFICIAL PALE LAS VEGAS NCHINI MAREKANI KATIKA UKUMBI WA MGM ILIYOHUDHURIWA NA MASHABIKI WENGI ZAIDI.KWA TAARIFA ZAIDI NENDENI MILLARD AYO KISHA SEARCH SHOW YA DIAMOND MAREKANI.
DIAMOND SIO MARA YA KWANZA KUPATA MAPOKEZI KAMA HAYO.ULIZENI WAKENYA,WAMALAWI,WASAUZI,WAZIMBABWE NA SASA MSUMBIJI.KOTE AMEPOKELEWA KAMA MTU MWENYE KITU FULANI CHA ZIADA.
DIAMOND NI MSANII PEKEE EAST AFRICA MWENYE VIEWERS ZAIDI YA 100M+ KATIKA KAZI ZAKE ZA MUZIKI.
DIAMOND NI MSANII PEKEE EAST AFRIKA AMBAYE AKIFIKA SAUZI NA NIGERIA NCHI HIZO ZINATAMBUA KUNA MSANII TOKA EA KAINGIA NCHINI KWAO.WENGINE POROJO KIBAO.
DIAMOND NI MSANII PEKEE ANAEPIGA SHOW ULAYA NA MAREKANI KATIKA KUMBI ZINAZOELEWEKA NA KWA MKATABA MAALUMU.WENGINE WENGINE HAO UKISIKIA KAENDA ULAYA JUA WANAKWENDA KUPIGA SHOW KWENYE KITCHEN PARTY,HAPPY B/DAY ZA WABONGO NA KWENYE VISHEREHE NA VIBAA VYA WABONGO...

Nakaribisha mapovu maana ukweli UNACHOOOOMA KAMA PASI
Hapo umeingiza bei gan? Nenda kibaruan wanao watafukuzwa ada
 
Back
Top Bottom