Diamond asema "Nipo tayari kumsaidia collabo Ali Kiba"

Diamond asema "Nipo tayari kumsaidia collabo Ali Kiba"

Inawezekana Diamond alimaanisha jambo zuri tu ila sijapenda alivyosema yuko tayari ''kumsaidia'' Alikiba, kwani Alikiba ni underground hadi aombe kusaidiwa? Kama ningekua Alikiba kwa kauli ya kitoto kama hii nisingethubutu kufanya kazi na Diamond hata siku moja maana hizo ni kauli za wanawake wa pwani.

Unajua kuna neno likitumiwa kwenye muktadha Fulani linaonekana si zuri! Hili neno kama kweli kalitumia halikupaswa kulitumia ukizingatia uhusiano alio nao kwa sasa na Alikiba!

Hili neno linamaanisha Alikiba hajiwezi kabisa pengine si kimziki tuu bali hata kifedha!

Pengine hakujua kama hili neno linaweza kuwa baya lakini si la kutafuta suluhu kabisa au Amani!
 
Hamumjui diamond jamani???anakaribia kutoa single mpya hapo anatafuta kick...
 
Unajua kuna neno likitumiwa kwenye muktadha Fulani linaonekana si zuri! Hili neno kama kweli kalitumia halikupaswa kulitumia ukizingatia uhusiano alio nao kwa sasa na Alikiba!

Hili neno linamaanisha Alikiba hajiwezi kabisa pengine si kimziki tuu bali hata kifedha!

Pengine hakujua kama hili neno linaweza kuwa baya lakini si la kutafuta suluhu kabisa au Amani!

Noted. Elimu yake ndogo.
 
Hivi Diamond ndio nani ? Au yule kijana alikua anaomba kufanya matamasha shule za sekondari Dar mi namjua Ali Kiba ndio ana tenzi za maana thats why i wonder kama Diamond amsaidie Ally tena kuna wasanii na ma mc.
 
Hahahaaaaa,alafu aliimba vibaya sijapata ona hasa pale mwishoni sauti iligoma kabisaaa
Prof.J angemtumia Q Chillah ule wimbo ungekua hatari sana

pepo la chuki litakutafuna mwana kondoo
 
Wema alipomfunza tu kizungu, anafikiri yupo juu ya wa TZ wote.
Shame.

Huyu mtoto bado hajajua maisha......ipo siku atajua kuishi na watu.Kuna kauli ni tata sana kutoa mbele ya watu kwa maana wapo mashabiki wapo pande zote sasa unapotoa kaul ya kebehi na dharau basi ujue mwisho wake umekaribia
 
Nahisi kuna maneno kwenye hii habari kama kweli kayasema kama alivyo nukuliwa yatazidisha uhasama!
Hilo neno kumsaidia lilikuwa halina sababu kutumika badala yake lingetumika neno kuwa Niko tayari kufanya nae Collabo kama ikitokea....

Neno "kumsaidia" linasikika vibaya sana kwenye hii habari na sijui kama ni kweli kalisema sijui Kiba atalitafsiri vipi?

Ni kama hii kauli ya Kiba alipoulizwa na Spora kuhusu yeye kurudi wakati Diamond yupo juu

“Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa
tu na kukaa tena , labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma ."
 
domo ni domo na atabaki kuwa domo sikujua kama ana busara nukta.... nlikua napenda interview zake ila kwa maneno hayo... si bure ukubwa wa mdomo umezidi akili hafikirii anaropoka tu mfeeeewwwwww siku akiporomoka sijui ataficha wapi sura yake limbukeni tu.
" be good to people on your way up, u may need them on your way down"
 
Kama kimataifa Mbona Kiba kaimba hadi na R kelly? kama shoo za nje mbona kiba kafanya sana?..na wewe Kiba ulishindwa nini kuomba collabo na R kelly na Ipupa na amani wakati ulikua nao muda mwingi mkifanya mazoezi ya kuimba na kurekodi?..ona sasa hata washamba wanakudharau!..acha tuu waendelee kukudharau umezubaa sana wewe Kiba!.. huyu mshamba ataendelea kukunyanyasa sana kwa ujinga wako!...

kumashabikia kiba ni headache..hata video ya mwana inaingia mwezi wa 4 huu kashindwa kutoa...nigga yuko slow kama konokono..watu watamchoka soon
 
Huyu mtoto bado hajajua maisha......ipo siku atajua kuishi na watu.Kuna kauli ni tata sana kutoa mbele ya watu kwa maana wapo mashabiki wapo pande zote sasa unapotoa kaul ya kebehi na dharau basi ujue mwisho wake umekaribia

., huyu dogo atapotea kama upepo.

Hakuna mtu duniani anaweza pingana na kuishinda 'DISCIPLINE'. Structured and formal knowlege.

Sidhani,, hata WEMA hana uwezo huo.
 
Back
Top Bottom