Diamond ashindwa kupanda Mlima Kilimanjaro, Steve Nyerere azitapika Tsh. Milioni 2

Diamond ashindwa kupanda Mlima Kilimanjaro, Steve Nyerere azitapika Tsh. Milioni 2

Kupanda mlima Kilimanjaro kunataka maandalizi.

Hizi si habari za kutaka kupanda kwa kuigaiga tu bila maandalizi. Huko juu kuna thin air, lack of oxygen na altitude sickness.

Nakumbuka miaka ya nyuma sana kuna kaka zetu walikuwa wanasoma Arusha School walienda kupanda mlima Kilimanjaro kama kundi la shule, mmoja wao alifariki.
 
Wanaume wa dar hawawezi kufika kileleni hadi kwenye mlima?

Diamond na umaarufu wake naye kashindwa kufika kileleni ila angebust ile dawa ya kumkomesa semeji probably angefika
Hili la wanaume wa Dar naona limeibua wanaume wa kinondoni,
 
Na kule si lelemama kama mwili hauko vizuri unaweza rudishwa maiti chini.
Huwa nakumbuka sana stori yako ya kukwea kileleni, juu mawinguni.

Kwa hali yangu hii ya kuchechemea/mgogoro/goigoi/dhaifu inahitajika maandalizi yasiyopungua miaka 5 ndipo niweze kujaribu kukwea huko.

Steve angefika kileleni huenda angeomba parachute ajitupe kama yule MCanada juzi.

Nampongeza sana kutambua kuwa hawezi na hawezi kujilazimisha kwani hata akina MwanaFA walipomshawishi kwa kumpa ngawira akatambua kuwa uhai ni bora kuliko ngawira, uhai ukipotea huwezi kuutafuta tena ila ngawira zinatafutwa endapo zikipotea
 
Wewe uliweza hongera, ila utalii wa kupanda mlima kwangu hapana ile ni adhabu kwangu.

Asante.
Mimi nilitoboa ila ilikua shughuli mpaka kwenda na kurudi salama. Mtu akikwambia kafika kileleni inabidi umpongeze kwa kweli.

Hawa wasanii wengi kama nawaona watakavyokua wanabakia hawaendelei mbele na safari
 
ilianza kama safari,twende mawenzi wakaone
kumbe ni ngumu safari,utajachoka wakuone

Mungu aliumba dunia na maajabu ya eeh
Ya mulima sikia omba usiipande eeh

kizai zai,kizai zai,kizai zai.
 
Wakuu, binafsi nilifuhia sana, Waziri Hamis alivyohamasisha wasanii wengi kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Mara moja, kwa kauli mbiu Twende Zetu Kileleni...

Safari ilianza Jana Jumamosi Tarehe 28/09/2019, Ilikuwa ya siku sita.

Lakini Diamond, Steve Nyerere na Dogo Janja wamerudi leo Jumapili baada ya kuchoka sana... Walifika kituo cha kwanza Mandara wakarudia mbele kidogo ya Mandara.

Changamoto kubwa ni kupanda Mlima kwa mhemko, na pia nilishasema tena hapa kwenda gym kila siku hakukupi uwezo wa kupanda mlima Kilimanjaro. Na pia jamaa walionekana wakienda kwa kasi sana, Kosa kubwa... Kilimanjaro ni Polepole.

Bado nina wazo la kupanda Mlima Kilimanjaro na WanaJF walioko committed.

Na wote tutatoboa...

Wasanii waliobakia, wajitahidi sana ili watoboe.
 
Back
Top Bottom